Bunge linapopendekeza kununua mafuta ya "Kidebe" baharini, Waziri January usikubali huo uharamia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,441
147,151
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa hatuhitaji magumashi katika kuendesha shughuli zetu binafsi na zile za Serikali.

Kulikoni kununua mafuta ya kidebe huko baharini basi ni heri mumuombe Asas awauzie mafuta kutoka kwenye visima vyao huko Arabuni kama kweli hamtaki tena kufanya bulk procurement.

Mafuta ya kidebe? Nchi ngumu sana hii.

Maendeleo hayana vyama!
 
Njia zote 2 zitumike
na ndicho alichosema mtoa mada, mbunge wa Gairo, kwamba hiyo bulk procurement inayoibana nchi kuwa na mfumo wa pamoja wa kuagiza mafuta waendelee nao kwa watakaotaka kujiunga nao, lakini pia tuachie waagizaji wengine walete kutoka kokote watakapoyapata.... hata kama watafaulisha kutoka kwenye meli nyingine baharini ambako huwa yanapatikana kwa robo ya bei ya soko la dunia...

Kazi ya serikali, amesema mbunge wa Gairo, iwe kuleta TBS wayapime ubora pale yanaposhukia mafuta yote nchi hii, kwenye flow meter ya bandari. Mafuta yatashuka bei kwa sababu kutakuwa na ushindani wa kuingiza mafuta. Na kabla ya kuanzishwa mfumo wa bulk procurement, amesema mbunge huyo, mafuta yalikuwa bei ya chini.
 
C6C95445-95CF-4FAC-B91C-315913519892.jpeg

Iran na Venezuela ndio sehemu pekee utakayopata hayo mafuta duniani. Sio Shabiby pekee anaejua; it’s common knowledge kwa wanunuaji wote wa mafuta hasa hao wanao nunua in Bulk Procurements.

Ndio maana kuna vigezo luluki kabla ujasajiliwa kuweza ku bid BPS Tanzania. Moja wapo ni certificate ya kuweza kununua mafuta na mahala unapoyatoa ili nchi isiingie kwenye migogoro ya kimataifa kwa kuchukua mafuta ya magendo. Shabiby anapendekeza tuachane na utamaduni huo, serikali ifanye mambo kiholela.

Lakini sio dunia aijui kuna ghost tankers, tatizo hiyo ni illegal business kutokana na vikwazo walivyowekewa hizo nchi.

Sasa unapoona mmbunge anashauri hadharani serikali ijikite kununua hayo mafuta ya magendo kinyemela bila kufikiria implication za diplomatic relations kwenye international community inakuonyesha ufinyu na ulimbukeni wa watu tunaochagua kutuwakilisha.
 
na ndicho alichosema mtoa mada, mbunge wa Gairo, kwamba hiyo bulk procurement inayoibana nchi kuwa na mfumo wa pamoja wa kuagiza mafuta waendelee nao kwa watakaotaka kujiunga nao, lakini pia tuachie waagizaji wengine walete kutoka kokote watakapoyapata...
Tuna mifumo ya hovyo sana.
 
View attachment 2180245


Iran na Venezuela ndio sehemu pekee utakayopata hayo mafuta duniani, sio Shabiby pekee anaejua; it’s common knowledge kwa wanunuaji wote wa mafuta.

Tatizo ni its illegal business kutokana na vikwazo walivyowekewa hizo nchi, sasa unapoona mmbunge anashauri serikali ijikite kununua hayo mafuta kinyemela bila kufikiria diplomatic relations na international community inakuonyesha ufinyu na ulimbukeni wa watu tunaochagua kutuwakilisha.
Ahsante sana bwashee!
 
Back
Top Bottom