Bunge letu linapoteza mwelekeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu linapoteza mwelekeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by regam, Jun 26, 2011.

 1. regam

  regam JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa jinsi nielewavyo mimi nchi inasimamiwa na mihimili mikuu mitatu(Bunge, Mahakama na Serikali kuu). Kili mhimili unafanya kazi zake "independently" ili kutekeleza majukumu yake. Kazi ya bunge ni kupanga maamuzi na sheria mbalimbali zitakazo simamiwa ili kutekeleza majukumu ya serikali. Kazi ya mahakama pamoja na mambo mengine ni kusimamia sheria mbailimbaili zilizotungwa na bunge ili kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake. Na kazi au jukumu la serikali ni kuhakikisha inatekeleza majukumu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi na taifa kwa ujumla.
  Kwa sasa kila mmoja anaweza kuona kwamba, majukumu ya hii mihimili ni kama hayaeleweki. Kinachotokea sasa ni kana kwamba hakuna mipaka ya utendaji wa kazi. Niovyo mimi ni kana kwamba sasa ni ushabiki tuu wa kiitikadi ndio unachukua nafasi yaani chama tawala dhidi ya upinzani. Hili liko wazi kabisa na hakuna mtu yeyote anayethubutu kilipigia kelele. Hii inadhihirika pale hata spika wa bunge anapokuwa akishabikia mambo ya kijinga yanayopelekea upotevu wa msingi wa majukumu ya bunge. Kianachoonekana ni kwamba, serikali(inayoongozwa na raisi na mawaziri) inajitahidi kiwaziwazi kushirikiana na wabunge (hasa wa chama tawala) na mahakama ili kufanya mambo ambayo ni aibu mbele ya wananchi wake.
  Mytake:
  Wanajf kama mojawapo wa "change agents" tufanye nini ili kulinusuru taifa letu hasa kwa kuhakikisha mihimili hii mitatu inafuata majukumu yake?
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Play your part... wewe umepanga kufanya nini?
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,918
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Hivi we mpaka leo unategemea serikali ya CCM kutuletea maendeleo?? we wawapi??
  Hii ni trick ya CHADEMA bana..inaitwa ''delay techniq''...CCM hawajaijua bado...pakimbazuka 2015 hiyo...CCM
  inabaki na madeni ya ahadi...wakti CDM inaingia Ikulu....!! Hii inapendeza sana...na naomba Bunge
  liendelee hivihivi...
  Tufanyaje: Tuendelee kupigwa na maisha magumu hivihivi hadi kieleweke!!
   
 4. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuwaelimishe wabunge wa upinzani ili wajue kanuni za bunge.
   
Loading...