Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,768
- 41,011
Ukisikia watu wanasema sijui Magufuli anasema sana, anaropoka, hajali anachosema, ni mkali mkali, ujue wanamsingizia...
Hii si mara ya kwanza mimi kuandika juu ya hili. Na nina uhakika wapo watu wanajiuliza ni watu gani huwa wanaenda huko Bungeni. Wakati mwingine ukiangalia sana Bunge utadhani ni filamu ya Kichina au za Martial Arts kama Enter the Dragon, Fist of Fury, Crouching Tiger Hidden Dragon, au Kung Fu Hustle na The Drunken Master
Kwenye filamu hizo mara nyingi - kama siyo zote - hata yule ambaye mwisho atapigwa hadi ashindwe kujitetea kuna wakati unaweza ukadhani na yeye ni stelingi Yaani kwenye filamu hizi kila mtu mbabe tu! Tatizo huwa linakuja mwishoni kabisa ambapo mtu ambaye alikuwa anazipiga vizuri kweli sehemu nyingine ati anashindwa kabisa anapigwa hadi anapepesuka mwenyewe! Unajiuliza huyu jamaa si na yeye alikuwa gangwe? Ndivyo ukiangalia kinachoendelea Bungeni wakati mwingine!
Embu angalia kama hutaona jinsi gani kila mmoja anajifanya (au anaamini) ana Mkanda Mweusi Ngazi ya Tano! (black belt fifth degree)