Bunge latungiwa wimbo wa majibizano

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Nimebahatika kuusikia wimbo huo kutoka kituo kimoja cha radio ukiwa umeingizwa clips za majadiliano ya mabishano bungeni kati ya spika,mwenyekiti,mawaziri na wabunge katika hoja mbalimbali...aibu!
 
sasa mbona wewe mchoyo hivyo....kwanini usiweke hako ka clip tuka-enjoy haka ka weekend japo kwenye cm naana umeme mgogoro
 
sasa mbona wewe mchoyo hivyo....kwanini usiweke hako ka clip tuka-enjoy haka ka weekend japo kwenye cm naana umeme mgogoro
Mkuu bahati mbaya hata mimi nimeusikia juu kwa juu ktk radio ya gari nadhani ulikuwa unapigwa kwa mara ya kwanza so stay tuned utausikia tu
 
Haya asante Mpwa, natafuta sehemu ya kitimoto
Mkuu bahati mbaya hata mimi nimeusikia juu kwa juu ktk radio ya gari nadhani ulikuwa unapigwa kwa mara ya kwanza so stay tuned utausikia tu
 
ha ha ha ha ha! hata mimi niliusikia, bonge la wimbo, ila nahisi spika ataupiga marufuku, si mnamjua mama yetu yule....mama wa .....''so what.....''...nani kawaruhusu mushike hizo maiki?.................''nasema kaeni chini...''
 
Nimebahatika kuusikia wimbo huo kutoka kituo kimoja cha radio ukiwa umeingizwa clips za majadiliano ya mabishano bungeni kati ya spika,mwenyekiti,mawaziri na wabunge katika hoja mbalimbali...aibu!


e
MBONA tumeshazoea sasa..Bunge letu limekuwa kama SOKONI vile! Kweli wakiwezeshwa wanaweza.........!! where is SITA?
 
Mama anaekalia kiti si alisema wanleta fujo kama watu wa kariakoo? sijui aliwarate vipi watu wa k,koo
 
Wabunge wa ccm wamegeuka wanaitetea serikali,bunge limekuwa kero na hako ka mama kiroboto mikwara mitupu bora aliesema fungeni mlango tupigane.
 
huu wimbo uliiimbwa na jamaa mmoja (mi mbaya sana kukumbuka majina ya waimbaji...sijui dogo Dito...aaah sijui mm) kisha DJ 'Vencha' nadhani akauongeza makorombwezo...looh!


Mama kanituma niende gongo la mboto.....
Oooh ooh kkoo!
 
bora huyo aliyewatungia wimbo make bunge la sasa ni vituko vitupu na vichekesho tu jana kuna mwingine nilisikia akiseme ye ni ndo handsome boy tu badala ya kusema nini katumwa na wananchi wake
 
Ni Dj Venture wa Clouds Radio ndiye aliye mix majibizano ya hovyo ya bungeni na wimbo wa Kariakoo wa msanii Mataruma. Umetoka bomba sana. Kwa mujibu wa radio hiyo singo hiyo itapatikana hivi karibuni mitaani.
 
Tbc napo unasikika? Uweke na hapa jf basi!!
Kupata clip ya muziki uliopigwa redioni ni ngumu kidogo na hasa kama mimi ambaye niliusikilizia kwenye radio ya gari. Labda kama kuna mwenye uhusiano na watu wa hiyo radio tunaomba watuwekee hapa jamvini.
 
Sijausikia lakini nadhani utakuwa una maudhui mazuri sio kama ule unoitwa R1.
 
Leo nilidamka asubuhi sana nikawatumia Power Breakfast ujumbe wa kuwaomba wapige huu wimbo. Nawashukuru kwani mara tu baadA ya kumaliza jingle wakafanya kweli.

Kiujumla wimbo una maudhui na unatoa picha ya Buunge tulilonalo sasa. Bunge la vioja na miongozo ya spika isiyokuwa na mwongozo.

Style hii ya kuchukua vipande vya hotuba au matukio ya kisiasa na kuunganisha kuwa wimbo kwa mara ya kwanza niliisikia/niliiona Uganda mwaka jana. Kuna mwanamuziki (jina nimesahau) alichukua hotuba ya Mu7 na kuikataka akaifanya wimbo ambao ume-heat mwaka jana, mwaka mzima.

Heko kwa Mataluma na Dj Venture
 
Back
Top Bottom