Bunge lataka Serikali kuchukua hatua kali kwa waliohusika sakata la madini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.

Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na Bunge.

"Bunge linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla," amesema Mkuchika.

Kukubaliana na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.
 
mamaa weeeeeee
kuna watu hawana haya duniani humu!
eeh rabi weee mbona uliwanyima akili hawa wabunge wetu
eti
"bunge lataka wahusika wawajibishwe"
bunge hili linamtaka nani awajibishwe?
leo situkani.
 
  • Thanks
Reactions: mwl
Mambo mengine yanaleta kinyaa. Bunge la mapoyoyo linajitekenya lenyewe na kucheka lenyewe. Ni Bunge hilohilo lililopitisha mikataba hiyo kwa hati ya dharura, na ni Bunge hilohilo leo linameza matapishi yake kwa vigelegele! Ama kweli, wabunge wetu uwezo wao ni wa kusoma na kuandika tu basi!
 
Mkuchika ni kiongozi asiye na haya.. Juzi wamemfungia Bulaya Mdee kisa haya ha mambi..
 
Mkuchika eti Mtaalamu wa Lugha ndo alitake Bunge na yake......Ukistaajabu ya Acacia hujayajua ya [HASHTAG]#Williamson[/HASHTAG] Diamond......Kamati sahihi na kw a wakati sahihi haipaswi kutokana na Bunge hill hili la Ndiooooooooooooooooo then tutegemee mawazo mbadala
 
Bunge lingemuunga mkono rais kwa kuanzakumvua uwenyekiti wa bunge na Dalal wa madini Kafumu uwenyekiti wa kamati ya nishati na madini
 
In short ccm wote ni wanafiki.
Jpm kwa mfano ageuke aanza kuwasifia wawekezaji basi wabunge wote wataanza kushangilia
 
Ni aibu kubwa kwa bunge hili,leo mwenyekiti wa bunge A chenge achukuliwe hatua kali,
 
Back
Top Bottom