Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,486
- 13,087
Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni mbalimbali za uchimbaji na uchakataji madini inatarajia kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati itakayohusisha mnyororo mzima katika Sekta ya Madini.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema kuwa Wizara ya Madini inaahidi kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha Kampuni zinakamilisha taratibu za ulipaji wa fidia kwa wananchi pamoja na kuendeleza miradi husika na kusimamia utekelezaji wake.
Waziri Mavunde ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushauri wake makini ambao imekuwa ikiutoa katika nyakati tofauti na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri wote wa Kamati hiyo katika kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi na hatimaye kuchangia ipasavyo katika ukuaji wa uchumi wa Taita, mesema hayo, Agosti 13, 2024 jijini Dodoma
Mhandisi Lwamo amesema kuwa Tume ya Madini ilitoa Leseni za Uchimbaji wa Madini wa Kati na Mkubwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo yamekuwa yakihitaji taratibu za kuhamisha wananchi ili kupisha utekelezaji wa miradi husika.
Aidha, Mhandisi Lwamo ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa uchimbaji madini ya nikeli wa Kabanga, Mradi wa uchimbaji mkubwa wa SMCL mkoani Mwanza, Mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe wa Faru Graphite mkoani Morogoro, Mradi wa uchimbaji madini ya mchanga mzito wa Baharini (Heavy mineral sands).
Vilevile, Mhandisi Lwamo ameitaja miradi mingine ni pamoja na Mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe wa Bunyu, Nachu na Chilalo mkoani Lindi na Epanko mkoani Morogoro.