Bunge lapitisha bajeti ya Serikali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Dodoma. Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania limepitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni.

Akitoa matokeo ya shughuli ya upigaji kura ulivyokuwa, bungeni leo Jumanne Juni 25 2019, Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai amesema jumla ya wabunge waliopiga kura ni 380.
Amesema wabunge ambao hawakuwepo walikuwa ni 12 na hakuna mbunge ambaye hakuamua.

Kagaigai amesema wabunge waliosema hapana walikuwa ni 83 sawa na asilimia 21.8 ya wabunge waliopiga kura wakati wabunge 297 sawa na asilimia 78.2 walipiga kura za ndio.

Baada ya Kigaigai kutangaza matokeo hayo, Spika wa Bunge Job Ndugai ametangaza kuwa Bunge limekubali kupitisha makadirio hayo kwa asilimia 78.2.
 
Huo ndio mwanzo wa kuanzia kutafuta pesa na sijui wanaanzia wapi maana milango yote ya waliokuwa wanawategemea imekaza.ukikaza vyuma na wenzio wanakukazia vile vile.
 
Back
Top Bottom