Bunge lamjadili Masaburi

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Kamati ya bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeanza kujadili pamoja na mambo menginekauli ya Meya wa jiji la Dsm Dr DIDAS MASABURI baada ya kutukana baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam kuwa wanafikiria kwa kutumia makalio.

Naibu spika wa bunge Job Ndugai amekiri kamati hiyo kukutana jana na leo kujadili suala hilo.

Meya huyu amekuwa maarufu sana hapa JF ambapo wana jukwaa wamekuwa wakitumia msemo huo kuwakejeli wenzao.

source:Habari leo.
 
Tamuchungu...unazungumzia kale kausemi ka wana JF kwamba watu wanafikiria kwa kutumia Masaburi.
 
Masaburi imekuwa kamsemo ka kuficha neno halisi sasa ie kuficha neno husika ambalo ni kali
 
Lakini BUNGE na KAMATI YA BUNGE ni vitu viwili tofauti sana!

usipotoshe umma wa JF.kamati imetumwa na bunge,ndio maana ile kamati ya bunge iliyoundwa kufatilia mgogoro wa madaktari iliwakilisha bunge zima,au ww unafuata sheria na taratibu za afghanistan nn
 
Kujadili na kuchukua hatua ni vitu viwili tofauti. Tumeona managapi yamejadiliwa na kuekewea mapendekezo lakini mpaka leo kimya ! Tunataka bunge lenye meno sio hili la blah blah.
 
Duh! Kwa kweli alitoa tusi lisilo la kitaasisi na anastahili kufundishwa nidhamu ya kiuongozi. Kama mimi nilisema ukweli tu niko mbioni kufukuzwa chamani, iweje kwa huyu kigogo aliyesema watu wanafikiria kwa kutumia 'Masaburi?'

Maana watu hufikiria kwa kutumia brain, na ukiambiwa tu kwamba unafiiria kwa kutumia spinal cord (ambayo ni mfumo huo huo wa fahamu) unaweza kupigana, vipi ukiambiwa unatumia 'muscles za makalio' kufikiri??? Nadhani ni sawa na mtu kukuambia hauna ubongo kabisa!
 
Ingekuwa vema ukaweka na picha ya Masaburi tukamjua

Prince+Charles+of+Wales+%2528kulia%2529+akisalimiana+na+Meya+wa+jiji+la+Dsm+Dr.+Dida+s+Masaburi+alipowasili+ktk+viwanja+vya+karimjee+le.jpg
 
Bunge siku zote lilikuwa wapi wameeona neno masaburi limepata umaarufu hapa JF ndio wameanza kujitutumua.
 
Back
Top Bottom