Wakuu,
Hii hoja ina mambo mengi sana na ngumu kuchangia bila kujikanyaga. Kuna mambo mengi yamejadiliwa na mengi yanapingana.
Je ni lazima kuweka chuo ulichosoma kwenye kila CV? Hapana sio lazima ila ni muhimu. CV ni picha ambaye unampelekea dada anayetaka kuchagua mume wa kumuoa. Sifa za kuwa mume bora ziko nyingi sana na katu haziwezi kujulikana kwa kutumia hii picha moja. Lakini utakuwa kichaa kama utatuma picha ambayo unaonekana ni kituko. Inategemewa kwamba utajaribu kupeleka picha nzuri zaidi ili angalau uwe kwenye shortlist ya kuonana na huyu dada na hapo ndipo sifa zingine zitajulikana.
Chuo ulichosoma kinasaidia kuonyesha/kutoonyesha sifa uliyonayo. Kwa kutokuweka jina la chuo unaweza kuonekana umeficha makusudi, hivyo hufai, unaweza kumpa hamu huyo mtu atake kujua zaidi juu ya wewe na hivyo kukuingiza kwenye shortlist.
Kiujumla nitasema kwa kazi ambayo ni professional, nategemea kuona jina la chuo ulichosoma. Ukisema umemaliza form four lazima useme umemaliza wapi? Ukiandika umemaliza chuo kikuu, nitategemea useme ni chuo gani.
Kwa wengine chuo ulichosoma na kupasua kwako vinaishia kwenye shortlist. Ukija kwenye interview nitataka zaidi kujua unajua nini. Kila mtu ninayemwita kwenye interview ninakuwa na uwezo wa kumpa kazi. Ni kwamba katimiza minimum requirements ya kazi husika. Kwahiyo kuniambia umemaliza na A+ hainisaidii, ninataka kujua shuleni umefanya nini, umefanya projects zipi, mwisho wake ulikuwaje, ulipambana na matatizo gani, uliyatatua vipi nk. Mtu ninayempa kazi ni kwasababu amenionyesha anajua nini.
Je inawezekana kuchukua wanafunzi wa chuo kimoja tena darasa moja? Ningelikuwa mimi nisingelifanya hivyo hata siku moja hata kama hicho chuo kingelikuwa bora sana. Diversity ni jambo muhimu sana, kwa kuwa na interviewees toka vyuo mbalimbali unaweza kujifunza mengi na hivyo kufanya uchaguzi ambao ni wa maana zaidi. Hata probability inakataa kwamba katika vyuo 10, chuo kimoja tena watu wa mwaka mmoja wanaweza kuwa wazuri kuliko hawa wengine wote.
Haya mambo ya chuo kipi bora, nafikiri yapo toka miaka na miaka. Nakumbuka wakati wengine tupo mlimani, kulitokea vita kali kati ya UDSM na Mzumbe. Mwenyekiti wetu alitamka kwenye vyombo vya habari kwamba inakuwaje wanafunzi wa junior colleges kama Mzumbe wapate allowances kubwa kuliko sisi. Mzumbe walikuja juu sana.
Sidhani kama mijadala kama hii inasaidia sana jamii. Uzuri wa jambo unatokana na mambo mengi sana. Inawezekana UD ni brand kubwa na inapata wanafunzi wengi wazuri kwasababu ya jina lakini je output yake pia ni nzuri? Ni vizuri kumwangalia kila mtu individually na kumpima kama anafaa au la. Tukianza kuajiri watu kwa kufuata amesoma wapi, inaweza kutuletea matatizo mengi sana.
Kuitwa kwenye interview ni hatua kubwa kuelekea kupata kazi. Ukisoma chuo ambacho brand yake inajulikana unakuwa umejirahisishia njia ya kwenda kwenye interviews nyingi na hivyo kupata kazi kirahisi. Chuo kikiwa na brand kama vile Oxford, Havard nk. kinakuwa kinapata wanafunzi wazuri zaidi, kinavutia walimu wazuri zaidi, research nyingi muhimu zinapelekwa kwao, ni rahisi kupata pesa nyingi zaidi, hivyo mara nyingi hata output yake inakuwa graduates wenye uwezo zaidi.
cha ajabu wahitimu zaidi ya 15 toka chuo kimoja,darasa moja, ST.AUGUSTINE UNIVERSITY ambao wamehitimu NOV 2008 walitakiwa wawe na uzoefu wa Miaka miwili, wote wamekuwa short listed na wameitwa kwenye interview.Wengi wenye sifa toka vyuo vingine kama UDSM hawakuitwa.
kwanza si vyema kutaja majina ya watu bila idhini japokuwa unahoja. Pili kuitwa interview watu wa darasa moja siyo ajabu, mimi nilifanya interview pale TBL DSM mwaka 2006 na alikuwa anatakiwa maintenance engineer tukakutana watu tisa wote darasa moja na mmoja wetu akachukuliwa. Nadhani acha vijana wenzetu wachape kazi cha msingi wasijiingize kwenye ufisadi.
It is hard to believe kanda2's posting, unless we are provided with more evidence.
Though everyone has the right to post anything, it'll be stupid for us to just jump affimatively into any postings, even if its validity is seemingly doubtful.
P'se, don't just relax with your popcorn, do some thinking.
Eti niulize hakuna hata mzanzibar mmoja aliyeomba nafasi hizo ukizingatia bunge ni chombo cha muungano?
Sasa kama nafasi say ni 14?? 20?? na maombi ni 2000 na ni Bunge la Muungano- kweli hakuna haja ya kuwa na quota ya nafasi hata 1 zu 2 toka visiwani kama kati ya waliiomba wanaqualify??
Hii ya kuchukua tu wanafunzi wa chuo kimoja kutakuwa kuna walakini!
Eti niulize hakuna hata mzanzibar mmoja aliyeomba nafasi hizo ukizingatia bunge ni chombo cha muungano?
Standards zetu ziko chini sana.Sikupenda walivyowavunjia privacy waomba kazi hapo.Kuna watu wengine wana mind business zao ziwe private, sasa kibongo bongo watu washawekwa mijina kwenye migazeti ya mtandaoni.
Nilipoanza sikuweka majina nikaambiwa muongo, nimeweka majina standards ziko chini, nimemsikilize nani?yako mengi ya private sijayaweka juu yao kama pass zao n.k kwenye kujenga au kurekebisha lazima maumivu yatokee ili turekebishe.
Wewe umeweza kuweka majina haya kutokana na system mbovu inayoruhusu kutoa majina haya katika files za HR.
What's next, watatoa mishahara yao pia?
Kama kuna ufisadi mtuhumiwa namba moja ni HR, kama kuna mtu wa kusakamwa na kutolewa jina ni hao watu wa HR.
Unless una ushahidi concrete kwamba hawa waomba kazi walitoa rushwa au kuhusika na ufisadi ili kupata kazi, kuwatoa majina ni kuwa expose unnecessarily.
Game Theory, Dar es salaam wamawazo kuwa waislam wamebaguliwa kwenye hii selection... Ndio maana unaona statement kama "...ohoo ngoja nipige simu kwa first lady" .. akitegemea JK na first lady i.e. waislam wenzao watawasaidia). OK?
MY TAKE: Tutetee haki bila kungalia kwanza dini ya "victim".
Mkamap.
Wamekuja watu wawili kukuelekeza jinsi ya kuandika CV.mimi nimekuwekea link ujifunze kuandika cv.
Nakuuliza ule mpango wako uliotutangazia kuwapeleka majuu wachezaji wetu umefikia wapi?umemuona Yusuph Bakhressa anayejua kuandika CV kijana Ngassa anakwenda west ham united.
wewe umeshindwa hayo utazijua hoja zangu? BUNGE sio jeshi walikojazwa wakurya watupu enzi za Mwalimu.
unajua kuwa shrika la Bima liliwahi kuundiwa Tume ya kuchunguza ajira za ubabaishaji kama hizi?ilikuwa kila atokae Mbeya anapata kazi, sawa na bunge kwa kila atokae Nyegezi.hakuna lisilo na mwisho za mwizi arobaini Nombo na kashilillah wako kikaangoni.
by the way vipi box ALCATEL leo?kule kwa michuzi blog kuna mjadala wa box tunaomba mchango wako.