- Thread starter
- #61
Wakuu,
Hii hoja ina mambo mengi sana na ngumu kuchangia bila kujikanyaga. Kuna mambo mengi yamejadiliwa na mengi yanapingana.
Je ni lazima kuweka chuo ulichosoma kwenye kila CV? Hapana sio lazima ila ni muhimu. CV ni picha ambaye unampelekea dada anayetaka kuchagua mume wa kumuoa. Sifa za kuwa mume bora ziko nyingi sana na katu haziwezi kujulikana kwa kutumia hii picha moja. Lakini utakuwa kichaa kama utatuma picha ambayo unaonekana ni kituko. Inategemewa kwamba utajaribu kupeleka picha nzuri zaidi ili angalau uwe kwenye shortlist ya kuonana na huyu dada na hapo ndipo sifa zingine zitajulikana.
Chuo ulichosoma kinasaidia kuonyesha/kutoonyesha sifa uliyonayo. Kwa kutokuweka jina la chuo unaweza kuonekana umeficha makusudi, hivyo hufai, unaweza kumpa hamu huyo mtu atake kujua zaidi juu ya wewe na hivyo kukuingiza kwenye shortlist.
Kiujumla nitasema kwa kazi ambayo ni professional, nategemea kuona jina la chuo ulichosoma. Ukisema umemaliza form four lazima useme umemaliza wapi? Ukiandika umemaliza chuo kikuu, nitategemea useme ni chuo gani.
Kwa wengine chuo ulichosoma na kupasua kwako vinaishia kwenye shortlist. Ukija kwenye interview nitataka zaidi kujua unajua nini. Kila mtu ninayemwita kwenye interview ninakuwa na uwezo wa kumpa kazi. Ni kwamba katimiza minimum requirements ya kazi husika. Kwahiyo kuniambia umemaliza na A+ hainisaidii, ninataka kujua shuleni umefanya nini, umefanya projects zipi, mwisho wake ulikuwaje, ulipambana na matatizo gani, uliyatatua vipi nk. Mtu ninayempa kazi ni kwasababu amenionyesha anajua nini.
Je inawezekana kuchukua wanafunzi wa chuo kimoja tena darasa moja? Ningelikuwa mimi nisingelifanya hivyo hata siku moja hata kama hicho chuo kingelikuwa bora sana. Diversity ni jambo muhimu sana, kwa kuwa na interviewees toka vyuo mbalimbali unaweza kujifunza mengi na hivyo kufanya uchaguzi ambao ni wa maana zaidi. Hata probability inakataa kwamba katika vyuo 10, chuo kimoja tena watu wa mwaka mmoja wanaweza kuwa wazuri kuliko hawa wengine wote.
Haya mambo ya chuo kipi bora, nafikiri yapo toka miaka na miaka. Nakumbuka wakati wengine tupo mlimani, kulitokea vita kali kati ya UDSM na Mzumbe. Mwenyekiti wetu alitamka kwenye vyombo vya habari kwamba inakuwaje wanafunzi wa junior colleges kama Mzumbe wapate allowances kubwa kuliko sisi. Mzumbe walikuja juu sana.
Sidhani kama mijadala kama hii inasaidia sana jamii. Uzuri wa jambo unatokana na mambo mengi sana. Inawezekana UD ni brand kubwa na inapata wanafunzi wengi wazuri kwasababu ya jina lakini je output yake pia ni nzuri? Ni vizuri kumwangalia kila mtu individually na kumpima kama anafaa au la. Tukianza kuajiri watu kwa kufuata amesoma wapi, inaweza kutuletea matatizo mengi sana.
Kuitwa kwenye interview ni hatua kubwa kuelekea kupata kazi. Ukisoma chuo ambacho brand yake inajulikana unakuwa umejirahisishia njia ya kwenda kwenye interviews nyingi na hivyo kupata kazi kirahisi. Chuo kikiwa na brand kama vile Oxford, Havard nk. kinakuwa kinapata wanafunzi wazuri zaidi, kinavutia walimu wazuri zaidi, research nyingi muhimu zinapelekwa kwao, ni rahisi kupata pesa nyingi zaidi, hivyo mara nyingi hata output yake inakuwa graduates wenye uwezo zaidi.
Umemaliza kila kitu,Thomas kashilillah na NOMBO ambaye ana kaimu ukurugenzi wa utawala na utumishi kwa upuuzi huu hahitajiki kukaimu atafutwe mtu mwingine, labda watajifunza.