Sipingi darasa zima kuitwa kwenye interview ila kama wana MERITS au sifa husika cha ajabu creteria zilizowekwa za kuomba kazi hiyo hawana kama uzoefu wa miaka miwili.Nyegezi haiwezi kuifikia UDsm HATA iwe vipi?fuatilia UNIVERSITY LEAGUE TABLE kwa Africa utaona Udsm ina nafasi gani na Nyegezi hakuna anayeijua.
NYEGEZI haiwezi kupambana na Tumaini acha Udsm.labda ijipime na Kairuki au Bukoba University.
Hapa sioni tatizo kabisa.
Mimi mwenyewe nime apply kwenye kazi ambayo requirement ikisema experience miaka mitano ,tena nikiwa mwanafunzi na nimeitwa na makapuni makubwa na nikiwa short listed baadhi ya makapuni hayo ni ALCATEL-LUCENT,Atos origin n.k.
Na kiwango cha kufaulu wajili wajanja hawaangalii sana wanachoangalia je nini unakifahamu kuhusiana na kazi waliyokuitia.Pia experience mwajuwa je? hawo jamaa hawana experience?? kumaliza shule 2008 si kigezo kabisa.
Mtu iga first class yako andika CV yako shagharabala nenda kwenye interview ushindwe kuwakilisha uone jinsi utakavyopigwa bao na watu wa third class.
Hapa kwa kweli mimi sioni hoja mpaka hapo baadae mtakapotumwagia data za uhakika
..st augustine ipo rwanda na kenya?..wahitimu hao ni watanzania????...sasa lazima watu wa UD ...ambako wengi tumepita mjuwe soko la ajira sasa lina ..mzumbe,dodoma,stjohn,augustine,Tumaini,kairuki,IFM, arusha,.meru,muslim...st.joseph,dar tech...etc
NIMEONGEA NA WAAJIRI WENGI ...WANASEMA WAHITIMU WA VYUO VINGINE ...WANAJIANDAA VEMA ZAIDI KWA INTERVIEWS NA MARA NYINGI HUWAZIDI WATOTO WA MUJINI UD.......nadhani watot wa UD wanakuwa na overconfidence...
Pamoja na kuwa ukweli UD inachukuwa wanafunzi wenye makzi nzuri zaidi ....lakini ujuwe mnapoingia chuo kikuuu ....mnakuwa kwenye mazingira tofauti...kuna ambao hawakupata devision one za kuingia THE PREMIUM Ud...just kwa kuwa wamesoma kwenye shule duni....lakini wanapokuwa kwenye mazingira sawa ukichanganya na akili zao za asili ...uwezo wao hukua kwa kasi ya ajabu!!
......
Ulikuwaje mwanafunzi na ukaomba kazi? ni part time au kazi ya usiku?wewe umewahi kutuambia hapa JF kuwa unataka kuwapeleka ulaya wachezaji wa ila huna contact zao viongozi wa club na timu ya Taifa wanakufanyia hiyana.tukakupa contact zao wote nini kiliendelea? natilia mashaka kuwa umefanya kazi ALCATEL ukiwa na status ya uanafunzi.
Hao wa UDSM ,Tumaini na vyuo vingene hawakupewa nafasi ya kuitwa kwenye interview wakafanye vitu vyao.ndio maana wakajazwa Nyegezi ili wasije UDSM kuwaharibia.Kashishilah angewapa nafasi aone kama watu wake wa ST.AUGUSTINE kama wangepita.
Kwa mujibu wa barua ya malalamiko kwa DR.Kashishilah Thomas majina ya waliomaliza NOV 2008 na hawana uzoefu hata wa miezi sita baadhi yao ni TUSAJINGWE,MUNGILE,CATHERINE MWIHULU,SALVATORY MKUDE,JOSEPHAT QORRO,MTAKI,EVARIST,JASMINI BABLIA,MORORO,WAMBURA,CATHELINE,IRINE,MWIHULA hao wote ni darasa moja wamehitimu NOV 2008.
UNAPOCHUKUA WATU WA DARASA MOJA KAMA WANA WEAKNESS BASI NI WOTE ILA UKIWEKA MCHANGANYIKO WANAWEZA KUJIFUNZA KWA WENZAO AU WAKAWAFUNZA WENZAO.
CHANZO CHENYEWE KUNA DADA MHITIMU WA ST.AUGUSTINE AMBAYE YUKO HR BUNGENI, AKISHIRIKIANA NA DAP NOMBO KWA BARAKA ZA DR.KASHISHILAH WAMEKUWA WAKIFANYA MAZINGAOMBWE HAYA KWA MUDA MREFU.
ST.Augustine hawako juu kuwashinda UDSM au Tumaini University.waliochukuliwa wana kiwango kidogo cha kufaulu.nimebahatika kuona vyeti vya walioachwa na waliopita kwenye interview,wameachwa wengi wenye uzoefu na uwezo.mfano sharti la kazi lazima uwe una uzoefu wa miaka miwili hao wa ST.AUGUSTINE hata mmoja hana sifa hiyo.huwezi kuchukua watu wa darasa moja Hansard Repoter wameitwa watu 15 kwenye interview na wa ST.AUGUSTINE wako 14. nafasi zinazotakiwa ni saba.ST.Augustine hawawezi kuwa juu ya UDSM hata kwa nini.inaonekana wewe ni mmoja ya hao walioitwa kwenye Interview wakiwa wahitimu wa ST.Augustine utasema vipi majungu wakati Hard Facts zipo na unapewa.
Tatizo lako unapenda ligi zisizo na miguu na kichwa ,lawachezaji linatokezea wapi? kifupi chansi zilitokea mimi kama mtanzania nikiwapigia debe wazangu waje wasakate kabumbu lakini ndivyo hivyo tena.
Sijakwambia nimefanya kazi alcatel ila nimeitwa kwenye interview tena nikiwa mwanafunzi na kazi yenyewe zilikuwa zinastate experience miaka mitano.
Ungekuwa wewe ungesema nimetowa rushwa teh teh teh teh kwa sababu tu udsm wamebwagwa.
Waitweje kwenye shortlist kama hao jamaa wa AUG wameshaonyesha wanatisha ktk CV.
kwa mfano.
Ngoja nikupe siri moja wale jamaa wanaofanya usaili ukishaweka tu sijui umesoma chuo gani 90% umeshamwagwa.Na ukiweka sijui ma vyeti yako nayo unaongeza 9% zinakuwa zimefika 99% za kumwagwa.
Mwezako anakuwekea tu mimi nina first digrii ktk uandishi wa habari bila kutia mbwembwe nyingi. Huyooo yupo ktk shortlist.
Na hili ndilo tatizo la wahitimu wa Tanzania, wote wanataka kufanya kazi za kuajiriwa... ona sasa vyuo vingine vinavyonyanyapaliwa!
Elimu ya kujitegemea iko wapi?
Mnakumbulka shairi hili?
Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ya sasa, yawafaa wananchi
Kama ni kweli elimu yetu ya sasa yatufaa wananchi, kilio cha kuajiriwa kinatoka wapi?
MKAMAP.
Hakuna cv unaweza kuandika bila kutaja chuo ulichosoma, mimi sijawahi kusikia labda wewe ulipoomba kazi huko ALCATEL.Obama asingetaja wapi kasoma lakini kila mtu anajua HARVARD.kutaja chuo ni jambo la wajibu kwenye CV inaonekana hata CV kwako ni mtihani.
Sema utakavyo lakini huwezi kufananisha status ya Udsm na Nyegezi.kwenye ajira HR lazima azingatie ubora wa chuo alichosoma muombaji.
Haiwezekani mtu aliyesoma Udsm akafundishwa Accounting na DR.Assad akawa sawa na mwanafunzi aliyemaliza nyegezi akafundishwa na kijana aliyehitimu hapo akapata First class akabakizwa kuwa mhadhiri.
Ubora wa chuo unatizamwa kwenye mambo mengi kama tafiti n.k na hivi vyuo vipya vina matatizo mengi kuanzia library,walimu n.k huwezi kusema mtu aliyesoma medicine KAIRUKI atakuwa sawa na mtu aliyesoma medicine MUHIMBILI university, wa muhimbili ana walimu na ana hospital ya rufaa yenye madaktari mabingwa, Muhimbili ina link na university au taasisi mbali mbali duniani.
Mhadhiri wa Kairuki atakuwa ni part time akitoka kufundisha muhimbili then aingie wodini halafu ndio aende Kairuki.kuna masomo hayafundishwi jioni kama Bio chemistry n.k
maktaba ya Udsm ina past papers toka 70s jee Nyegezi watakuwa na vitu kama hivyo?
Oxford University haiwezi kuwa sawa na Makelele university,mtu aliyesoma Oxford atakuwa na exposure kubwa kwa kusoma na watu tofauti tofauti na facilities za chuo ni advantages kwake,ubora wa wahadhiri, research zilizofanywa n.k si sawa na Makelele,
pia mtu wa Udsm atakuwa na exposure kubwa kuliko wa Nyegezi.Obama kusoma Harvard digrii ya sheria hatokuwa sawa na Mwakipesile aliyesoma law Tumaini university,Obama atakuwa amekutana na watu wa mataifa mbali mbali akiwa Harvard,Mwakipesile atakuwa na watu wanaofanana nae tu. kuna on line journals mbali mbali ambazo Harvard itakuwa inazo.ambako Tumaini hakutakuwa na facilities kama hizo.
Mkamap akija DR.slaa,DR.Nchimbi,DR,Kamala,dr.Nagu na PhD zao ambao wamesoma vyuo zisivyotambulika halafu akaja DR.Kawambwa shukuru,Dr.Mwakyembe,Professor Lipumbana DR.batilda Burian utawaweka pamoja bila kuona ubora wa vyuo walivyosoma?nikupe namba za wachezaji uwapeleke ulaya?
Rafiki yangu hili ni tatizo kubwa kuelimika kunatokana na mtu na sio chuo.Haya mwakyembe ndiyo aliyasema kwa namna moja ama nyingine akija mweupe mkopo anapata akija mswahili blah blah
Hiyo ndiyo mentality na yakwako kuhusu elimu zinafanana sana na mfano wa mwakyembe.Kama chuo ndio kuelimika kwisha kazi Angalia hao viongozi wengi wa Tanzania wamesoma vyuo gani? 80% wametoka vyuo unavyovitaja yani.
UDSM - Havard - oxford .Angalia walivyo mafisadi.Mkuu mwajili mjanja anaangalia una nini kichwani na si umetoka wapi.
Mkamap, hio CV isiyokuwa n Jina la Chuo...duh mara ya kwanza kusikia...!! au ndio CV za kupika!!!
na Hao wanaofanya shortlist nao magumashi au wamegumikwa wimbi la UFISADI....
Katibu wa Bunge elewa sasa Tanzania inajitajidi kuwa Macho, mambo ya Ajira ni mambo sensitive sana. unapofanya ukiritimba huu usione kuwa utaachwa,pia elewa ufisadi wa style hii unaweza fananishwa na ule unaofanywa na Vibaka barabarani ambao at the end huishia Kuchomwa MOTO...
......usijeingizwa ktk hilo kwani wale waliokosa hizo nafasi wasije kukufanya sivyo wakielewa kuwa Hukutumia Strong Vigezo kufanya selection yako....
issue hapa ni jinsi watu walivyodhulumiwa na ofisi ya Bunge kwenye uajiri
au hilo nalo tatizo kwako?