Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Mpita Njia

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
6,999
Reaction score
1,189
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

__________

TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

______________​

Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge.
Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.

Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwakuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti.
Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kunaRadio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD,BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.

Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendeleakutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazokwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazoyatakayotolewa na mitandao ya Bunge.
Utaratibu huu unatokana na uamzi wapamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bungevitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwajuu ya mawasiliano TCRA. Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahirikwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio auTecknohama, bali linatarajia kuboreshaupatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pandezote, yaani Bunge na Wananchi.

Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayokwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupatafeedtoka katika mitambo ya Bunge, napale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursahiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajirihiyo.


Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati.
Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.

Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).


Hivyo basi, wakati zoezi la maboreshohayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwambatunaendelea kusisitiza tena, Wananchiwasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitishamatangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima lamaboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge.


Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.

Dr. Thomas D.Kashililah

KATIBUWA BUNGE​
 
huyu jamaa kauli zake zinautata!..hivi Nape alipotoa maoni yake juu bunge kurushwa live. Hapa kunajambo
 
Si huyo huyo aliongea kuwa wana mpango wa kusitisha. Au alikuwa anapima upepo unaelekea wapi akakuta hauwezi kuzuiliwa akaamua kusema mengine
Nguvu ya wananchi ni kubwa sana na wala hili hakutegemea wananchi wangestuka ila alijua litapita tuu akajikuta kumbe upepo ni wa kimbunga haufai kuzuia
 
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

__________

TAARIFAMAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

______________​

Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitikotaarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa,Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge walaKamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa mojakama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katikaUendeshaji bora wa Shughuli za Bunge. Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwampango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionaoaweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.

Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwakuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA,kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanzakurusha live video striping kupitiatovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitiamajadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti.
Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezowa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bungekatika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafayanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kunaRadio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD,BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa nauwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada yamitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.

Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendeleakutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazokwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazoyatakayotolewa na mitandao ya Bunge.
Utaratibu huu unatokana na uamzi wapamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bungevitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwajuu ya mawasiliano TCRA. Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahirikwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio auTecknohama, bali linatarajia kuboreshaupatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pandezote, yaani Bunge na Wananchi.

Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayokwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupatafeedtoka katika mitambo ya Bunge, napale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursahiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajirihiyo.


Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati.
Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.

Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).


Hivyo basi, wakati zoezi la maboreshohayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwambatunaendelea kusisitiza tena, Wananchiwasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitishamatangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima lamaboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge.


Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.

Dr. Thomas D.Kashililah

KATIBUWA BUNGE​
Ina maana KASHILILAH ULINUKULIWA VIBAYA?
 
Dr. kama madakta wengine au ni walewale , kamera ipo kila sehemu siku hizi . Kuanzia kwenye miwani, kalamu,simu,ipad, saa na nguoni. Anatamani kumeza mawazo na kukurupuka kwake awali
 
Lakini ukiisoma vema hiyo statement yao bado kuna mtego. Watakachokuwa wanafanya ni wao wenyewe Bunge kupiga picha na kurekodi sauti na kisha kuwapa waandishi link ya kurusha watakavyo. Trick ipo hapo kwenye kupiga p[icha na kurekodi, tuna uhakika gani watapiga picha zile ambazo watu watataka kuziona? Si ajabu Chadema watakapoamua kusimama tena kushinikiza hoja zao hatutaziona picha hizo, au Tundu Lissu atakapokuwa anampa Spika vidonge kwa kusigina kanuni, tunaweza tusiwekewe hiyo sauti
 
Walikuwa wanapima upepo;hata hivyo bado nia yao ni mbaya tumeshawastukia tutaendelea kuwabana ili haki yetu tusidhurumiwe
 
nchi ya Mazingaombwe...siji kuiamini tena kauli ya serikali ya jk.!
 
Back
Top Bottom