Bunge lajadili malori kukwama bandarini

Ndugu zangu,

Wabunge wa CCM wanapiga kotekote

========

Bunge lajadili malori kukwama bandarini Dar​

Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Dodoma. Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hoja ya kuahirishwa kwa mjadala imewasilishwa leo Jumatano Mei 12, 2021 na mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi.

Chumi amesema Bandari hiyo ndio chanzo kikubwa cha kuendeleza nchi na kufanikisha miradi, “malori hayashushi wala kupakia mizigo kwa maana uchumi kwa namna fulani umesimama. Na tunazungumzia ushindani kati ya bandari yetu na nchi jirani.”

“Katika hali hii hatuwezi kukaa kimya na kuacha mambo ya namna hii yaendelee ndio maana ninajenga hoja tuahirishe mjadala ili tujadili jambo hili nyeti.”

Amesema kuna mizigo inayokwenda kwenye miradi mbalimbali ikiwemo wa uzalishaji wa umeme wa maji katika bwawa la mwalimu Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), lakini imekwama katika bandari hiyo.

Amesema mizigo inayokwenda nchi jirani imekwama wakati Taifa linatarajia bandari hiyo kuwa na ushindani.

Baada ya hoja hiyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliruhusu hoja hiyo ijadiliwe kwa muda wa dakika 20 ambapo wabunge saba walipata nafasi ya kuchangia.

Akijibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekwenda Dar es Salaam kushughulikia suala hilo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma>> Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba na rushwa kurudi kama zamani
Siyo kuijadili tu hata ujinga huu haungefanyika mama awe makini na hao ccm
 
Which kind of managerial issues.we want to know it otherwise is a political issue
 
Hisia zangu zinanipeleka kufikiri tofauti kwamba, huu ni mpango wa makusudi kutibua upakiaji na ushushaji wa mizigo ili baadaye waje na sababu pamoja na suluhisho. Watasema kwamba, bandari ya sasa inachangamoto sana kwa sasa, suluhisho ni kujenga bandari ya Bagamoyo ili kuondokana na changamoto hizi.
 
Wakati wa mwendazake msingejadili chochote!
Mmekomaa kumponda mwendazake. Huyu ashafariki. Haisaidii. At the end of the day bado wananchi wata question perfomance ya serikali. Sasa kumpiga vita mwemdazake haisaidii. Hapa ni vita vya wananchi against umasikini ujinga na malazi. Sio vita ya mwendazake vs other group
 
Hisia zangu zinanipeleka kufikiri tofauti kwamba, huu ni mpango wa makusudi kutibua upakiaji na ushushaji wa mizigo ili baadaye waje na sababu pamoja na suluhisho. Watasema kwamba, bandari ya sasa inachangamoto sana kwa sasa, suluhisho ni kujenga bandari ya Bagamoyo ili kuondokana na changamoto hizi.
Mkuu

Hiyo sababu haina nguvu kwa sababu bandari ya Dar Es Salaam imepanuliwa sana, suala hapo ni changamoto ya ujenzi wa barabara ya Kilwa-Mbagala kwa mwendo kasi pale makutano ya Uhasibu ni balaa usipime. Miundo mbinu ya ya barabara baada ya daraja la Nyerere nyembamba sana na hata mzani uliowekwa sambamba na barabara umeongeza ufinyu kiasi kinacho fanya mjongea wa kuingia na kutoka badarini kususua.

Upakiaji wa mizigo unafanyika TPA, TICTS na mizigo mingine inahamishiwa ICD hapo kurasini au kwingine hivyo mizunguko inakuwa mingi isiyonatija kwa ufanisi wa kazi.
 
Ahaa!
 
Mnaogopa. Mnahisi mda wowote mnaweza kua challenged. Tatizo mnakua sana paranoid, natamani sana lema, lissu na wanachadema waache kuongea tuone mtalaumu nani
 
Ndugu zangu,

Wabunge wa CCM wanapiga kotekote

========

Bunge lajadili malori kukwama bandarini Dar​

Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Dodoma. Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hoja ya kuahirishwa kwa mjadala imewasilishwa leo Jumatano Mei 12, 2021 na mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi.

Chumi amesema Bandari hiyo ndio chanzo kikubwa cha kuendeleza nchi na kufanikisha miradi, “malori hayashushi wala kupakia mizigo kwa maana uchumi kwa namna fulani umesimama. Na tunazungumzia ushindani kati ya bandari yetu na nchi jirani.”

“Katika hali hii hatuwezi kukaa kimya na kuacha mambo ya namna hii yaendelee ndio maana ninajenga hoja tuahirishe mjadala ili tujadili jambo hili nyeti.”

Amesema kuna mizigo inayokwenda kwenye miradi mbalimbali ikiwemo wa uzalishaji wa umeme wa maji katika bwawa la mwalimu Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), lakini imekwama katika bandari hiyo.

Amesema mizigo inayokwenda nchi jirani imekwama wakati Taifa linatarajia bandari hiyo kuwa na ushindani.

Baada ya hoja hiyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliruhusu hoja hiyo ijadiliwe kwa muda wa dakika 20 ambapo wabunge saba walipata nafasi ya kuchangia.

Akijibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekwenda Dar es Salaam kushughulikia suala hilo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma>> Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba na rushwa kurudi kama zamani
Wambieni waziri mkuu asisahau kwenda na waandishi wa habari kama alivyoenda BRT ila mpaka sasa hivi ufanisi ni sifuri hakuna kilochobadilika alitusababishia tu foleni na mikelele kibao

Kwio
 
Nachukia sana kiongozi dhaifu dhaifu, tunarudi enzi za Mr. Dhaifu wa Msoga
Kuna mijitu inashangilia eti inasubiri hela zimwagike mtaani!

Hivi bandari ni sehemu ya malori kukaa siku 5 kweli?

Juzi juzi kuna meli ili block mlango bahari hapo mashariki ya kati na unaambiwa kila siku hasara ya bilioni kadhaa ilikuwa inatokea. Vipi sisi hapa kwa siku tano hizo kuna sh ngapi imepotea.

Utawala wa Kikwete na Magufuli umewapa mwanga sana watz juu ya uongozi.
Asijaribu kumridhisha kila mtu hasa hili genge dogo la huku mitandaoni akijaribu kuwafuata hawa atapotea
 
Tumekubaliana sasa ni utawala wa sheria.
au nasema uongo ndugu zangu.

Husemi uwongo ndugu yangu

sasa bimkubwa anapigwa 5:0 kwenye hili.

lilikiwa kosa kubwa sana kuwapunguza moto akina majaliwa nk.wale ndio wangekua kifua chake,kisha yeye endelee kubembeleza watu kama mama wa taifa.

wabishi wote wamezima moto,maana mama anacheza na jukwaa.

Bora mmeona
 
Back
Top Bottom