Ntaramuka
Senior Member
- May 2, 2008
- 169
- 27
Spika Makinda ameliambia bunge kuwa ana ujumbe mwingi kutoka kwa wananchi wakilalamikia mwenendo wa bunge kuwa halina heshima, wabunge wanabishana na kuzozana sana! Mimi jamani, labda mimi nina matatizo, nifurahia sana hili bunge, jinsi wabunge wanavyobishana kwa hoja na pale CCM wanapotaka kutumia wingi wao kuukandamiza upinzani, wapinzani, wakiongozwa na CDM wanapambana kuhakikisha haki inatendeka. Sasa mtu anayesema bunge halina heshima anataka liweje? Aluta continua CDM na wapenda haki wote bungeni, bunge linanivutia sana!