'Bunge la spika Sitta lilikuwa bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Bunge la spika Sitta lilikuwa bora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 11, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  'Bunge la spika Sitta lilikuwa bora'
  Thursday, 10 February 2011 21:16

  Geofrey Nyangóro
  UBORA wa Bunge la Tisa chini ya Spika Samwel Sitta, umezidi kuthibitika baada ya matokeo ya utafiti wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu, kutoa ripoti inayoonyesha kuwa Bunge hilo lilifanyakazi nzuri kuliko mabunge yote, tangu nchi ilipopata uhuru wake mwaka 1961.

  Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, aliongoza Bunge hilo kwa kauli mbiu ya kasi na viwango, kwa kuruhusu mijadala mizito ya kashfsa za ufisadi ikiwemo Richmond, iliyomfanya Edward Lowassa, kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008.

  Pamoja taarifa ya wabunge kudaiwa kupeleka mawazo yao binafsi bungeni, ripoti hiyo kwa upande mwingine imelilitaja Bunge hilo kuwa ndilo lililokuwa bunge la mafanikio kuliko mbunge mengi tangu Tanzania ilipopata uhuru.

  Utafiti huo kuhusu utendajikazi wa bunge la mwaka 2010, uliangalia pia historia ya Bunge la Tanzania tangu uhuru.

  Akitoa matokeo ya ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Utafiti na Utoaji Taarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba, alisema matokeo yanayonyesha kuwa Bunge la Tisa ndilo pekee lililokuwa la mfano huku likiwa na baadhi ya wabunge walioibua mijadala mizito iliyosababisha serikali ya wakati huo, kuanguka.

  Ukiacha Richmond iliyomng’oa Lowassa na baraza la mawaziri, Bunge la Tisa pia lilishuhudia mijadala mizito kama ya wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje EPA, Meremeta iliyomfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuapa kutozungumzia chochote kwa maelezo kuwa kampuni hiyo ilikuwa na siri za ulinzi na usalama wa nchi.


  Akithibitisha makali na ubora wa bunge hilo, Kibamba alisema; “Bunge hili ndilo lililokuwa machachari kuliko Bunge lingine lolote nchini Tanzania. Spika wa wakati huo, aliongoza mchakato wa mabadiliko ya kanuni za bunge zilizokuwa za muda mrefu, pili kulikuwa na kikundi kidogo cha wabunge wapambanaji wa ufisadi.”

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mkuu wa Kituo hicho, Imelda Urio, alisema lengo la utaifiti wa utendaji kazi wa Bunge ni kuhamasisha wabunge walioko madarakani, ili wajue kuwa kuna watu wanaofutilia utendaji kazi wa kila siku.

  Alisema katika maeneo yote waliofanya utafiti yakiwemo ya vijijini, wananchi waliwaeleza kuwa hawajawahi kufanya mikutano na wabunge wao huku wengine wakisema kuwa hawajawahi hukutana na wabunge wanapohudhuria vikao vya halmashauri za wilaya.

  Kwa upande wake, Jenerali Ulimwengu, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alijikita katika mchakato wa katiba huku akitaka wananchi kutoruhusu serikali wala wanasiasa, kuwanyangánya .

  Jenerali Ulimwengu ambaye ni mwandishi mkongwe nchini, alisema kama wananchi watawaachia wanasiasa mjadala wa katibu, kunaweza kusababisha maandaliza ya katiba yasiyouwa mazuri.

  Pamoja na mafanikio katika Bunge hilo, Kibamba pia alisema lilikuwa na kasoro kadhaaikiwemo ya wabunge kujiongezea posho na kupitisha mfuko wa jimbo.

  Kasoro nyingine ni ushindani mdogo baina ya wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani.
  Alisema kutokana na idadi ya wabunge wa chama tawala kuwa kubwa ilikuwa vigumu hasa kwa baadhi ya maamuzi yanayogusa wakubwa serikalini kushindwa kutekelezwa.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  Comments
  0 #6 Zinklia 2011-02-11 09:03 Kwa nini tusingoje vikao viendelee ndipo tutoe comment. Mbona bado mapema au kwa sababu ni mwanamke ndiye anaongoza?
  Quote

  +1 #5 mhogo mchungu 2011-02-11 07:59 Hili la sasa kuna uwezekano mkubwa likamshinda Makinda tayari dalili zimeanza kuonekana kwani anajaziba na u CCM umemkaa kwenye damu.
  Quote

  0 #4 nashon nkhambi 2011-02-11 07:38 jamani tutahudhunika usiku na mchana kwa kumbuka sitta kama ningekutana nae ningemshauri ahamie chadema kwani chama cha mafisadi hakimuhitaji mtu mchapakazi na mpenda haki.
  Quote

  +1 #3 yahaya 2011-02-11 07:27 Tutamkumbuka Samweli Sitta kiukweli uongozi na usimamizi wake Bungeni ulikuwa madhu
  buti na wa haki.

  Quote

  +1 #2 elibariki yerald 2011-02-11 06:26 MAKINDA TUMESHUHUDIA JUZI LIMEANZA KUMSHINDA MAPEMAAAAAAAAAA A. KUKANDAMIZA HAKI ZA UPINZANI MFANO HAKI YA CHADEMA KUUNDA KAMBI PEKEE NA KURUHUSU LUGHA ZA KEJELI

  ANATUMIWA NA MAFISADI KAMA ROSTAMU..HONGERA SITTA HISTORIA ITAKUKUMBUKA..KAMA MOJA YA WANAWEMA.

  Quote

  2011-02-11 02:54 Ni kweli bunge lile lilikuwa changamoto kubwa ya uelewa wa kisiasa kwa watanzania. kwa kweli walijitahidi sana na kwa kiasi kikubwa utaifa uliwekwa mbele tofauti na tulivyozoea. swala la kuogopana, kupendeleana ama kuoneana huruma lilipungua kwa kiasi kikubwa. Ningependa haya yaendelee na baada ya miaka mitano tunapoangalia nyuma tulione bunge la sasa likiongeza changamoto hii badala ya kuipunguza
  Quote
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  Bunge limeanza vibaya

  [​IMG]

  [​IMG] BUNGE la Jamhuri ya Muungano, limeanza vibaya. Juzi Watanzania waliofuatilia kipindi cha Bunge mjini Dodoma, walishuhudia wabunge wakipeana mipasho, kuzomeana na kurushiana maneno ya kejeli.
  Chanzo cha hali hiyo ni hatua ya Bunge kukubali kufanya mabadiliko ya kanuni kuhusu muundo wa kambi ya upinzani bungeni kwa kuondoa neno ‘Rasmi' kama alivyoomba Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed.
  Kanuni hiyo baadaye ilipitishwa na wabunge wa vyama vingine baada ya CHADEMA kugoma.
  Kwa mazingira ya sasa, mabadiliko hayo yanakilazimisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuunda kambi ya upinzani kwa kushirikisha vyama vingine vya upinzani, licha ya kwamba CHADEMA ina uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bila kushirikisha vyama vingine. Huo ni ubakaji wa demokrasia.
  Hatuna nia ya kuhoji hatua ya wabunge wa CHADEMA kususia upitishaji wa kanuni hiyo kwa kutoka nje, kwani ni haki yao kikatiba, lakini tunahoji jinsi mjadala huo ulivyoendeshwa kwa jazba, maneno ya kejeli na vijembe visivyo na tija kwa taifa.
  Lakini hata wabunge wa CHADEMA walipoamua kususia kwa kutoka nje, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kushirikiana na wale wa NCCR Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na UDP, waliwazomea wenzao wa CHADEMA mithili ya vibaka.
  Kwa walioshuhudia kipindi cha Bunge juzi, watakubaliana nasi kwamba wabunge wetu walivuka mipaka kwa kuwazomea wenzao wa CHADEMA, huku kiti cha Spika kikishuhudia utovu huo wa nidhamu.
  Kama alivyopata kusema Spika mpya wa Bunge, Anne Makinda, Bunge la sasa lina changamoto nyingi kutokana na mseto uliomo wa vijana na wazee, lakini pia wabunge wenye tofauti za kielimu na hata kiuzoefu katika masuala si tu ya siasa, bali pia hata ya uwakilishi wa ndani na nje ya nchi, lakini hatukuutarajia ujinga uliojitokeza juzi.
  Tunajua baadhi yao watakuwa wanataka kujenga majina na umaarufu kupitia Bunge, lakini kama katika harakati na mchakato huo watakwenda kwa kasi inayokiuka kanuni na utovu wa nidhamu kama wa juzi, watajikuta wanapata umaarufu hasi na si chanya kama wanavyodhani na kutarajia.
  Tunasisitiza tena kuwa jambo la msingi ni kwa wabunge kujua dhima yao na kwa kushirikiana na spika, wahakikishe kweli wanawawakilisha waliowapeleka bungeni na hatimaye wanasimamia masilahi ya taifa kwa ujumla wake bila kujali ufuasi wa itikadi za vyama vya siasa.
  Watanzania hawatavumilia kuona Bunge lao linageuka kuwa genge la malumbano, mipasho, kejeli na matusi yanayolenga kushambuliana kibinafsi zaidi.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Taswira ya CCM haitarejea kwa staili ya Kikwete
  [​IMG]

  Mwandishi wetu

  [​IMG] FEBRUARI 5 mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilisherehekea miaka 34 tangu kuanzishwa kwake. Kilele cha maadhimisho hayo, yalifanyika mjini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, alizungumza na wananchi.
  Rais Kikwete, alizungumzia mambo mengi yanayohusu chama hicho na nchi yetu kwa ujumla.
  Hata hivyo si nia ya makala hii kujadili mambo yote aliyoyazungumza yakiwamo yale ambayo tayari yameonyesha kupokewa kwa maoni tofauti na wananchi wa kada mbalimbali kama ambavyo tumeona katika vyombo vya habari mbalimbali.
  Moja ya mambo yanayojadiliwa sana baada ya hotuba yake ni kauli yake kwamba yeye hawajui wamiliki wa Dowans na kwamba eti hata yeye hataki walipwe. Hilo tuliache.
  Lengo la makala hii ni kujadili eneo jingine kabisa katika hotuba hiyo nalo likiwa ni kupotea kwa taswira ya CCM na nia ya kufanywa mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya chama hicho.
  Kwanza nianze kwa kumpongeza kwa kuthubutu kuwaambia viongozi wenzake waliomwezsha kushinda uchaguzi mara mbili katika kipindi kizishozidi miaka mitano kwamba chama chao kimepoteza taswira nzuri na mvuto mbele ya umma na kwamba wengi wao ni lazima waondolewe ili kukijengea taswira mpya na bora zaidi.
  Mimi kama mwananchi wa kawaida kabisa ambaye ni mwanachama ninayeyumba kutokana na mikanganyiko mingi iliyojitokeza katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wake.
  Naweza kusema kuwa ni miongoni mwa watu waliofurahi kusikia kwamba kwa mara ya kwanza kiongozi wa juu kabisa wa chama amekuwa na mawazo ya kuchukua hatua za kuwawajibisha watendaji ambao wamekuwa mzigo kwa chama.
  Lakini ninatatizika kidogo kuelewa viongozi hao ambao uongozi wa juu una madaraka ya kuushughulikia ni upi?
  Maana tumekuwa na watendaji wengi ambao walikuwa wanasimamia zoezi la rushwa wakati wa kura za maoni ambao wanaanzia katika ngazi za matawi, kata wilaya hadi mkoa.
  Ni dhahiri viongozi waliohusika katika rushwa hawakuwa katika ngazi ya taifa ambako taratibu zake ziko wazi na zilizo katika mazingira ambayo huwezi kutoa rushwa kwa yoyote.
  Utampa rushwa Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti au Katibu mkuu utaanzaje?
  Katika ngazi hiyo, hupokewa matokeo ya kila jimbo na mapendekezo ya mikoa na wilaya tayari kwa uchambuzi wakati zoezi la rushwa likiwa limekwisha kufanyika katika ngazi hizo.
  Sasa Rais Kikwete anaposema viongozi watashughulikiwa ili kujenga taswira ndipo ninapojiuliza, viongozi gani? Wale walioajiriwa na CCM au wale wanaoteuliwa na mwenyekiti?
  Ukiangalia katika ngazi za wilaya na mkoa, kuna watendaji wengi ambao hufanya kazi za chama ambao hushiriki katika kupanga na kutoa maamuzi makubwa katika chama katika ngazi zao ambao naamini si mwenyekiti au mwingine yeyote anaweza kuwaondoa bila kutumia utaratibu wa nyakati za uchaguzi wa chama.
  Katika kundi hili, wapo wenyeviti, makatibu wa Itikadi na Uenezi, makatibu wa Uchumi na Fedha, wajumbe wa Halmashauri Kuu na wale wa Kamati za Siasa katika ngazi zote (tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa).
  Binafsi najiuliza, hivi wakishughulikiwa wachache tu, tena wale walioajiriwa na chama, ndiyo taswira ya chama itajengeka upya? Hata hivyo mtizamo huu mimi unanipa tabu kidogo kwa maana naamini kwamba wananchi wa kawaida hawana jambo lolote wanalofanyiwa moja kwa moja na chama, linalowafanya wakichukie chama chao au kuharibu taswira.
  Binafsi naamini, chombo kinachoweza kuharibu taswira ya chama ni serikali kutokana na wananchi wanavyoweza kutokubaliana au kulalamika kwa jinsi serikali inavyochukua maamuzi mbali mbali ambayo wao wanaona yanawaumiza.
  Kwa mfano suala la Netgroup Solutions, Richmond, Dowans, EPA, uuzaji wa mabenki yetu kwa bei chee badala ya kuwaruhusu wawekezaji kuanzisha benki zao, mikataba ya madini, mishahara midogo, ugumu wa maisha unaotokana na uchumi wetu kuwa wa wasiwasi, gharama kubwa ya petroli kiasi cha wananchi kutojua EWURA ipo kwa sababu gani na wenzao wa TPDC.
  Kwa hakika, haya ndiyo yanayoharibu taswira ya chama chetu, bila kuyashughulikia haya hata ukifukuza watendaji wote wa ngazi ambazo una mamlaka ya kuwaondoa hakika taswira ya chama haiwezi kurudi.
  Wewe mwenyewe umeona baada ya hotuba yako ya Dodoma baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wasomi na wananchi wa kawaida walivyoonyesha kutokubaliana na suala moja tu ulilolitolea ufafanuzi la Dowans kwa kusema hata wewe hutaki walipwe na kwamba huwajui wamiliki wakati waziri wako akiwa tayari ameshawataja wale ambao wananchi wameshafanywa wasiamini kwamba ndio wenyewe kutokana na taarifa za kuchanganya wanazosoma kila siku katika vyombo vya habari.
  Wananchi wanaamini kuwa wahusika wa Dowans, wako ndani ya CCM, jambo linalopewa nguvu na baadhi ya mawaziri wako wanaotuhumu kwamba kuna baadhi wanataka kutengeneza fedha kwa ajili ya uchaguzi ujao wa urais.
  Ndiyo maana nakwambia, kutueleza taswira ya chama itajengwa kwa kuwaondoa viongozi walioajiriwa na chama tu huku serikali ikiendelea kuleta mikanganyiko isiyoleta majibu na kueleweka ndani ya uma, bila wakosaji kushughulikiwa ni kujidanganya.
  Binafsi naona wapo viongozi walioshiriki kuvuruga chama kwa nafasi zao ambao si wa kuajiriwa au walioko katika mamlaka yako ya uteuzi wakiachwa waeendelee kuvurunda, hapo ndipo ninaposema mzee wangu Kikwete mbali ya upendo wote nilionao kwako sijakuelewa.
  Tunataka kuona viongozi wote waliosababisha hali hii katika serikali yako wakiondoka au kuwajibishwa ili kujenga taswira nzuri ya chama. Mbona Lowasa, Karamagi na Msabaha na wengine wameondoka?
  Mzee Benjamin Mkapa kakuachia chama ukipata ushindi wa asilimia 80, zimepungua hadi asilimia 61, angalia usimuachie atakaye gombea katika uchaguzi ujao asilimia 30 kama hutacheza karata zako vizuri.
  Mabadiliko uliyoyasema yawe ya heri badala ya kuleta malalamiko makubwa na mkanganyiko ndani ya chama, vinginevyo vumilia hadi katika uchaguzi wa mwaka ujao wa chama.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Jazba na upeo mdogo wa Spika Anne Makinda utaligharimu taifa......................................

  Ameanza kwa kuchakachua kanuni ili awapitishe wachofu kusimamia kamati za matumizi serikalini.................................baada y hapo hata wiki haijaisha amekwepa ktoa mwongozo wa spika juu ya kauli ya PM kuwa Chadema ndiyo walioleta vurugu arusha..........................bila ya kutoa ushahidi wowote ule na kanuni za Bunge PM alisema uongo.............................................

  Sasa Godbless ajibu nini wakati ni Spika anayepaswa kutoa mwongozo wa hatua ambazo PM anapaswa kuchukuliwa........................................
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Wabunge Chadema wamtikisa Pinda bungeni
  Friday, 11 February 2011 00:25

  Exuper Kachenje, Dodoma
  WABUNGE wa Chadema jana walimtikisa waziri mkuu, Mizengo Pinda katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wakimtaka kueleza serikali ina tamko gani kuhusu mauaji yaliyotokea Januari 5 mkoani Arusha.Kadhalika kikao cha tatu cha mkutano wa pili wa Bunge la kumi, jana kilishuhudia mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa mbunge wa kwanza katika bunge la kumi kuwekwa kikaangoni baada ya kupewa siku tano na Spika wa Bunge, Anne Makinda athibitishe madai yake kwamba Waziri Mkuu Pinda aliudanganya umma wa Watanzania wakati akijibu swali kuhusu vurugu za Arusha.

  Hoja ya Mbowe
  Msumari wa kwanza kwa Pinda, ulipigiliwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, baada ya kuuliza serikali inatoa tamko gani rasmi kuhusu tukio la mauaji ya watu watatu katika vurugu na maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na wahusika akiwamo IGP Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu.

  Katika swali lake la nyongeza Mbowe alitaka kujua ni lini serikali itaunda tume ya kisheria kuchunguza tukio hilo kwa kupata maelezo kutoka pande zote husika tofauti na sasa ambapo taarifa zilizopo serikalini ni zile zinazotoka upande mmoja wa jeshi la polisi.

  Majibu ya Pinda
  Hata hivyo, akijibu kombora hilo, Pinda aliinyoshea kidole Chadema akisema kwa mujibu wa maelezo aliyopewa ilivunja makubaliano yake na polisi na kuandamana.

  Pinda aliweka bayana kwamba, baada ya hali hiyo kilichotokea ni polisi kujaribu kuzuia maandamano hayo ya wanachama wa Chadema ambao tayari walikuwa wamehamasishwa na viongozi wao kwenda "kuwakomboa" wenzao waliokuwa wameshilikiwa kituo cha polisi mjini Arusha.

  "Nakushukuru Mbowe kwa kuuliza swali hilo, serikali hii ni makini, ikiwa jambo limetokea usikimbilie kusema serikali,
  serikali..., ni vizuri kuulizaa aliyesababisha...,'' alisema Pinda na kuongeza:

  ''Mlikiuka makubaliano na polisi, matamshi ya kwenye mkutano
  hayakuwa ya chama chenye dhamira ya kujenga amani, mkawataka wafuasi waende kuwakomboa wenzao."

  Katika kuondoa wingu na kuweka hadharani kila kitu, Pinda alisema pamoja na juhudi za polisi kuzuia maandamano
  hayo, lakini yaliendelea hadi mita 50 kutoka kituo cha polisi,
  nao hawakuwa njia nyingine kwa kuwa hawakujua nini kingewakuta kama waandamanaji wangevamia kituo cha
  polisi.

  "Police were left with no option' (hawakuwa na njia nyingine), ndipo watu watatu wakapoteza maisha. Kama Mbowe na Chadema mngeamua
  kushirikiana na serikali haya yasingetokea," alisema Pinda.

  Kuhusu kuunda tume ya wanasheria kuchunguza tukio hilo na kutoa alichokiita Mbowe ni ukweli na
  kuchukua hatua, Pinda alisema uchunguzi unaweza kufanyika, lakini lazima serikali ijiridhishe kwanza ndipo hilo lifanyike.

  "Ni sawa uchunguzi unaweza kufanyika, lakini lazima serikali ijiridhishe. Rai yangu tushirikiane, lazima muda wote
  tujitahidi tujenge nchi ya amani na utulivu,'' alionya Pinda.

  Uchaguzi wa Meya Arusha

  Katika hatua nyingine, Pinda alisema taratibu zilizotumika kumpata Meya wa mji wa Arusha na Naibu wake ni sahihi.

  Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum Manyara, Martha Umbulla aliyetaka kujua pamoja na mambo mengine, msimamo wa serikali kuhusu Meya na Naibu Meya wa Arusha.

  "Sasa niseme hivi, kwa hesabu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza, katika uchaguzi mwenzako ana madiwani
  16 wewe una 14 utashindaje, baada ya hayo wakasema wakutane wazungumze, watazungumza nini?

  Hili ni suala la kisheria; Mimi nilikuwa Tamisemi, utaratibu uliofuatwa katika
  uchaguzi ule ni sahihi, Meya sahihi, Naibu Meya sahihi," alitoa msimamo Pinda.

  Hata hivyo, alisema pamoja na kuwepo kwa taarifa za Naibu Meya huyo wa Arusha kujitoa, lakini serikali haijapata
  barua rasmi kuhusu uamuzi huo.

  Pinda pia alisema, wabunge waliotajwa kuwa chanzo cha mvutano, aliowataja kuwa ni Chatanda wa CCM na
  Rebecca Mngodo wa Chadema ni halali.

  Lema: Pinda amedanganya
  Baada ya Pinda kumaliza maelezo yake hayo mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika kwa kusema "Mwongozo wa spika," akitumia kifungu cha 68.

  Lema baada ya kuomba mwongozo wa spika na kuruhusiwa alihoji; "Hatua gani zinaweza kuchukuliwa kama waziri mkuu analidanganya Bunge na umma? Naona waziri mkuu amelidanganya taifa," alisema Lema bila ya kufafanua
  alichodai kuwa ni uongo.

  Hata hivyo, kauli hiyo ilimchefua spika Makinda ambaye aling'aka akisema; "Bunge letu lina adabu lazima hiyo ifuatwe, huwezi kusema hivyo ikaishia hivi hivi tu, kama unaona waziri mkuu amedanganya basi nenda kaandike alafu ulete, maelezo yako,".

  Spika akionyesha kuchukizwa na kauli hiyo ya Lema, wakati akihitimisha kipindi hicho alimpa mbunge huyo wa Arusha mjini siku tano za kuwasilisha maelezo yake bungeni kuthibisha uongo wa waziri mkuu.

  Makinda alisema iwapo mbunge huyo atashindwa kuwasilisha uthibitisho huo, atatakiwa kujirekebisha kwa kufuta kauli yake au kuomba radhi, adhabu atakayokabiliana nayo ni
  kusimamishwa kuhudhuria vikao visivyozidi vitano vya bunge.

  Alimtaka kuthibitisha madai hayo, lakini kwa wakati Spika akitangaza hayo Lema hakuwepo ndani ya ukumbi wa Bunge.

  Hata hivyo, akizungumza na wanahabari baadaye nje ya ukumbi wa Bunge, Lema alisema : "Leo siwezi kuwathibitishia nisiharibu ushahidi, lakini nipo tayari kuthibitisha uongo huo wa waziri mkuu."

  Alifafanua kwamba," Bunge limeniambia nithibitishe, nasema waziri mkuu amedanganya na nitathibitisha hilo
  Februari 14 asubuhi, pia nitaongea nanyi (waandishi wa habari) na nitawapa uthibitisho."

  Alipoulizwa haoni kwamba pengine waziri mkuu alipewa taarifa potofu na siyo kusema uongo, Lema alisema: "Sio kwamba amepewa taarifa potofu, hilo ni lake yeye kulisema, lakini nasema waziri mkuu ameudanganya umma na nitathibitisha Februari 14."

  Spika Makinda alitoa agizo hilo kwa Lema, baada ya waziri mkuu kumalizia kujibu swali la mwisho lililoulizwa
  na Hamad Rashid wa CUF, kuhusu hali ya chakula na tishio la kupanda bei ya mafuta nchini.

  Madiwani Chadema kama wabunge wao
  Mwandishi, Moses Mashalla anaripoti kuwa sakata la uchaguzi wa umeya mkoani Arusha limeendelea kukufukuta kufuatia madiwani wa Chadema kususia kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Arusha kwa kutoka nje ya ukumbi, kwa madai kwamba hawamtambui meya wa manispaa ya hiyo, Gaudence Lyimo.

  Hatua ya madiwani hao imekuja saa 48 tangu wabunge wa Chadema watoke nje ya bunge ikiwa ni hatua ya kupinga hatua ya kufanyiwa tafsiri maneno ‘Kambi rasmi ya upinzani bungeni', katika kanuni za bunge toleo la mwaka 2007.

  Hatua ya madiwani hao wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wakati kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kikiendelea kilijitokeza jana majira ya saa 8:30 mchana wakati ajenda ya kuteua kamati za kudumu za manispaa ya Arusha ikitaka kuanza.

  Kabla ya madiwani hao kutoka nje kulikuwa na mvutano na malumbano ndani ya kikao hicho baina ya madiwani wa Chadema na CCM hali iliyomlazimisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Estomihi Chang'a kutoka nje ya ukumbi ili kupisha kikao kisicho rasmi cha muafaka baina ya pande hizo, huku mkuu wa wilaya ya Arusha akihudhuria kikao hicho.

  Madiwani hao wa Chadema wakiongozwa na kiongozi wao,ambaye ni diwani wa kata ya Elerai, John Bayo walitoka nje na kuwaacha madwiani wa CCM wakiwemo watumishi wakiendelea na kikao.

  Akizungumza mara baada ya kutoka nje, Bayo alisema walichukua hatua hiyo baada ya kufikia maafikiano na uongozi wa chama chao ngazi ya taifa ya kuwa hawamtambui meya wa manispaa ya Arusha.

  "Sisi hatumtambui meya wa Arusha kwasababu alipatikana kwa njia za zisizo halali, hivyo tumetoka nje ya ukumbi kwa maafikiano ya madiwani wetu na uongozi wa taifa kuwa hatuwezi kushiriki kikao cha utekelezaji na mtu ambaye hatumtabui,"alisema Bayo.

  Bayo alisema wao walipokea taarifa za kikao hicho cha madiwani ambapo ajenda walizoambiwa kuwa ni pamoja ana kufungua kikao, kuunda kamati za kudumu za manispaa ya Arusha na kuunda ratiba ya vikao vya manispaa kwa mwaka mzima.

  Alisema walipofika katika ukumbi huo waliomba watumishi wa manispaa hiyo watoke nje ili waweze kujadili muafaka wa masuala mbalimbali baina yao na madiwani wa CCM na ndipo walipokubaliana na kisha kuzungumzia masuala mbalimbali walioafikiana baina ya pande zote mbili.

  Alidai kuwa mojawapo ya masuala ambayo walikubaliana na madiwani wa CCM ni pamoja na kuitaka serikali izikutanishe pande mbili zinazopingana ili ziweze kujadili hali ya mvutano uliopo na kutafuta suluhu.

  Hatahivyo, alisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho walikubaliana pia kutafuta muafaka wa suluhu la utata wa umeya wa Arusha lakini baadhi ya madiwani wa CCM walipinga na kudai kuwa waendelee na ajenda zilizopo na suala hilo litafuata baadaye kitendo ambacho hawakukiafiki.

  Bayo alisema mbali na kulalamikia uchaguzi wa umeya pia walikuwa na wasiwasi na baadhi ya uundwaji wa kamati za kudumu za manispaa hiyo, kufuatia majina ya madiwani wa Chadema kuwekwa katika orodha katika baadhi ya kamati ihali hawakuomba kamati hizo.

  Kwa upande wake Meya Lyimo alisema wanashangazwa na hatua ya madiwani wa Chadema kutoka nje ya kikao hicho kwa madai ya kutotambua nafasi yake.

  Lyimo, alidai kuwa pamoja na madiwani hao kususia kikao, wao waliendelea na uundaji wa kamati za kudumu za manispaa ya Arusha kama kawaida bila kuwashirikisha madiwani wa Chadema kwa kuwa hawakuwepo na wataendelea kuchapa kazi za kuwatumikia wananchi.

  "Sisi hatukuwafukuza kwenye kikao lakini tumechagua kamati bila wao kuwepo kwa sababu hawakuwepo pia lakini tulitaka hata wao waongoze baadhi ya kamati," alisema Lyimo.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Arusha matatani bungeni


  *Alitaka aelezwe adhabu waziri mkuu akidanganya
  *Makinda amtaka kuwasilisha vielelezo Jumatatu


  Na Kulwa Mzee, Dodoma


  MBUNGE wa Arusha Mjini, Bw. Godbles Lema (CHADEMA) amemkoroga Spika wa

  Bunge, Bi. Anna Makinda pale alipomuomba mwongozo wa nini mbunge afanye ikiwa kiongozi mwenye mamlaka makubwa bungeni kama waziri mkuu atasema uongo.

  Mwongozo huo uliombwa muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kutoa taarifa ya mauaji yaliyotokea Arusha na Mbeya hivi karibuni, wakati akijibu maswali ya papo kwa papo na kukihusisha CHADEMA.


  Kutokana na kauli hiyo, Spika Makinda alihamaki, akisema wabunge lazima wawe na nidhamu, kwa kuwa waziri mkuu ni mtu mkubwa, na kumkalisha chini, lakini baadaye alitoa alikampa mbunge huyo siku 4 kuanzia leo hadi Februari 14 awe amethitisha kauli yake kwa maandishi.


  Tukio hilo lilitokea bungeni jana mara tu baada ya maswali ya papo kwa papo yaliyokuwa yakiulizwa na wabunge na kujibiwa na Waziri Mkuu, Bw. Pinda.


  Swali lililoibua kasheshe hiyo liliulizwa na Kiongozi wa Kambi ya upinzani, Bw. Freeman Mbowe kwamba polisi wamekuwa wakipiga raia risasi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na serikali, na kutolewa mfano wa mauaji yaliyokea Arusha na Mbeya na hivyo kutaka kujua kama serikali inaweza kutoa tamko la kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Shamsi Vuai Nahodha na IGP Said Mwema.


  Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema serikali iko makini sana na jambo likitokea, wasikimbilie kusema serikali, ni vizuri kuulizana nani kasababisha.


  Alisema katika mauaji hayo ya watu watatu, waliosababisha kutokea ni CHADEMA ambao walikataa kufuata makubaliano ya kufanya mkutano badala yake wakaelekeza wanachama kufanya maandamano.


  Bw. Pinda alisema walikubaliana kufanya maandamano kwa kutumia ruti moja, CHADEMA walikataa ndipo serikali nayo ilipokataa kufuata wanavyotaka wao, waliruhusu kufanyika mkutano peke yake.


  "CHADEMA walikaidi makubaliano hayo wakafanya maandamano ndipo baadhi ya viongozi wakakamatwa. Matamshi yaliyotolewa katika mkutano si ya chama chenye kujenga nchi, waliwaongoza wanachama waende kuwakomboa wenzao waliokamatwa kituoni wakati kituo

  hicho ni kikubwa na kuna silaha," alisema.

  Alisema katika purukushani za kuzuia kukifikia kituo hicho, ndipo mauaji hayo yalipotokea na kwamba endapo utaratibu waliokubaliana ungefuatwa mauaji hayo yasingetokea.


  Majibu hayo ya Waziri Pinda ndiyo yaliyofanya Bw. Lema kwa kutumia kanuni namba 68 (7) kuomba mwongozo kwamba mbunge anawezaje kuchukua hatua kama mtu mwenye nafasi kubwa kama Waziri Mkuu anapodanganya Bunge.


  Spika alimkatisha kwa mara ya kwanza kwa kumtaka aweke hoja hiyo kwa maandishi na kuonya kwamba wabunge wanatakiwa kutoa hoja kwa adabu.


  Akifafanua suala hilo baada ya kipindi cha maswali na majibu, Bi. Makinda alirudia akisema, bunge linaanza kukosa adabu, alitumia kanuni ya 63 (6) inayosema mbunge atawajibika kuthibitisha aliyosema kwa muda aliopewa au kwa muda atakaopanga.


  Bi. Makinda alisema katika kanuni ya 63 (8) inasema kwamba hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa atashindwa kuthibitisha ukweli spika anatakiwa kutoa adhabu ya kumsimamisha asihudhurie vikao visivyozidi vitano.


  Baada ya kusema hayo aliinuka Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika (CHADEMA) na kusema kwamba Bw. Lema aliomba mwongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7) hakusema kuhusu utaratibu, bali aliomba mwongozo ikiwa taarifa ya waziri mkuu si ya kweli, atumie utaratibu gani.


  Bi. Makinda alijibu: “Nilisema atoe taarifa kwa maandishi, ndio hivyo nasema hadi Februari 14, mwaka huu kipindi cha asubuhi cha bunge awe ametoa maelezo ya waziri mkuu kusema uongo.�


  Akizungumza nje ya Bunge, Bw. Lema alisema alichokisema ni sahihi yuko tayari kutoa maelezo Jumatatu.


  Katika hatua nyingine, akijibu swali kuhusu uchaguzi wa meya uliosabisha mauaji hayo lililoulizwa na Bi. Martha Gumbula, Bw. Pinda alisema uchaguzi ulikuwa sahihi na matokeo pia yalikuwa sahihi.


  Alisema kwa hesabu za kawaida hata kwa mtoto wa darasa kwanza wangewezaje CHADEMA kushinda wakati CCM ilikuwa na wajumbe 16, wenyewe 14 na TLP mjumbe mmoja.


  Waziri Pinda alisema wajumbe wote walikuwa na taarifa kwamba Desemba 18 mkutano utaendelea lakini siku hiyo wajumbe walifika 17 ambapo CCM walikuwa 16 na TLP mjumbe mmoja, wajumbe kutoka CHADEMA walikuwa wakifika na kuondoka wakati taarifa na barua kuhusu mkutano huo walikuwa nazo.


  Alisema katika mkutano huo, CCM ilishinda kwa nafasi ya meya na TLP walishinda unaibu meya, ilipofika saa saba mchana, Bw. Lema aliingia kwa ukali akitaka wafanye uchaguzi kumweka meya, ndipo polisi walipoingia kuwaondoa na mkutano ukaahirishwa. Baada ya hayo ndipo yakawepo maandamano ya kupinga matokeo hayo.


  Tulisikia naibu meya alijitoa katika magazeti, hatujapata taarifa rasmi, tukipata taarifa rasmi kwa maandishi hatua zingine zitachukuliwa,� alisema.


  Wakati huo huo, Mbunge Samson Kiwia (CHADEMA) alimuuliza swali Waziri Mkuu kwamba wakuu wa mikoa na wilaya watawezaje kuwatendea haki wabunge wa upinzani wakati wao ni makada wa CCM.


  Alisema Waziri Pinda kwamba mfumo wa serikali ulivyo ndivyo ulivyo, wakuu wa mikoa na wilaya watatekeleza ilani ya chama kilichoshinda.


  Huwezi kuwalalamikia wakuu wa mikoa na wilaya, hawa wanatakiwa kusukuma maendeleo kwa ahadi zilizotolewa, alisema.


  Akizungumzia hali ya chakula nchini, Bw. Pinda alisema itakuwa mbaya kwani bei zitapanda kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta lakini serikali imejipanga vizuri kukabiliana na tatizo hilo, wakuu wote wa mikoa walishapelekewa taarifa, chakula kitumiwe vizuri na mbegu za muda mfupi zitapelekwa.


  Waziri Pinda alisema hayo akijibu swali la Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohammed aliyetaka kujua hatua iliyochukua serikali kukabiliana na hali mbaya ya chakula inayosababishwa na hali mbaya ya upatikanaji wa mafuta ili kupunguza makali ya maisha kwa Watanzania.

  [​IMG]


  4 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... SERIKALI INGEKUWA MAKINI DOWANS ASINGEINGIA WALA MIKATABA MIBOVU KAMA YA RITES ISINGEKUWEPO. MATATIZO KAMA YA MFUMUKO WA BEI, UMEME,MAJI YANAONYESHA KUWA TUNA SERIKALI YA MAKANJANJA NA SIO WATU WALIOPO KWA AJILI YA MASLAHI YA TAIFA. NI WATU AMBAO WAPO KUJICHUKULIA CHAO MAPEMA.
  February 10, 2011 9:00 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... spika wa bunge la tisa alionekana anaikoroga kwa kuibana serikali juu ya richmond, epa, na BOT; spika wa sasa anabariki akijaribu kuwaridhisha waliomuweka; ajihadhari hali itakuwa nguvu na baadaye atasalimu amri. amesababisha kuwepo kwa bunge lisilo na heshima, kuzomea ni kazi ya watoto wa shule za awali si wabunge. cha ajabu humo ndani ya bunge kuna wachungaji, na wenye elimu za uimamu lakini wanaruhusu kuwepo kwa uongo bila uoga na wanadhani wanaweza kuwaburuza watanzan; wakati huo umekwisha wasijidanganya.
  February 10, 2011 9:30 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Hivi kweli ikugundulika waziri mkuu amelindanganya bunge atafanywa nini? au anayetafutwa ni aliyesema PM amelidanganya bunge? sidhani kama kutatoka majibu ya kueleweka hapo kwakuwa madam spika mwenyewe alipandwa na jazba baada ya kuambiwa PM akilidanganya bunge inakuwaje, sidhani kama kutakuwa na hukumu ya kweli kwa hilo jambo.
  February 10, 2011 10:08 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Si huyo tu waziri mkubwa aliyetudanganya wananchi hata boss wake JK alitudanganya wananchi kwa kusema kuna maendeleo mengi yamefanywa na serikali yake ambayo hatuyaoni mathalani swala la umeme limekuwa kizungumkuti tuna miezi miwili tu ya kuwa na huo mgao wa umeme wataalamu wamesema hali ni mbaya sana tunakaribia kuwa gizani totoro wao wanasema kuna maendeleo ngeleja alisema mgao wa umeme kwisha, aah wapi mbona ni tabu na balaa tunashangaa unafanya nini badala ya kujiengua maana kazi ilishakushinda siku nyingi. Miaka 50 ya uhuru tunajifunia giza, maisha magumu watu hawana uhakika wa mlo hata mmoja kwa siku, elimu duni watoto wetu walalahoi wamefeli kwenye hizo shule za kata zisizo na walimu na maabara hapo ndio tuwapongeze eti mmetufanyia makuu nchi hii? nitoe angalizo kwa serikali amani ya nchi hii inadumishwa na wananchi wenyewe na sio nyie ccm mko wachache sana nchi hii tusio na vyama ndio tuko wengi kwahiyo amani ni sisi watz tulioidumisha na sio nyie na msiwe mnapenda kusema kuwa nyie ndio mnafanya amani iwepo, angalieni nchi za tunisia na misri wanacholalamikia wa rais wao ni sawa na matatizo tuliyonayo hivyo msiwe mnatudanganya wananchi kwakuwa tuna masikio na macho ya kuona kuwa nyie mnaishi ikulu, oysterbay, masaki, mikocheni na mnakula na kusaza wakati wengine hata hayo makombo hawajui watayapataje, tumechoshwa na uongo wenu wajibikeni na sio kutufanya sie hatuna akili mnapoomba kura (kula vizuri) kwa kuwagawia wananchi chumvi, kitenge au unga hayo ni matusi na hata haimpendezi MUNGU, au mnadhani Mungu wenu ni pesa zenu?
  February 10, 2011 10:19 PM [​IMG]

  Post a Comment
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Ripoti yalimwagia sifa bunge la tisa


  Na Tumaini Makene

  WAKATI ripoti ya tathmini juu ya utendaji kazi wa bunge la tisa chini ya Spika Samuel Sitta imeonesha kuwa lilikuwa na ufanisi na ubunifu, imeelezwa

  kuwa bunge la sasa limeanza kwa 'kuchakachua' kanuni, hivyo kutakiwa kuwa makini ili lisije likapoteza uhalali machoni pa wananchi.

  Hayo yamesemwa jana katika uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya bunge la 9, iliyoandaliwa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambapo jopo lililopewa kazi hiyo ya kutathimni liliifanya kwa miaka mitano 2005-2010.


  Ripoti hiyo imesema kuwa bunge lililopita lilipata ufanisi na mafanikio kadhaa, kutokana na ubunifu na ujasiri wa baadhi ya wabunge wakiongozwa na utayari wa Bw. Sitta, ambaye wakati akishika nafasi hiyo aliahidi kuwa 'spika wa kasi na viwango.'


  Mafanikio yaliyopatikana katika bunge hilo, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ni pamoja na kutungwa kwa kanuni mpya za bunge za mwaka 2007, ambazo zimeelezwa kuwa zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuliwezesha lifanye kazi kwa ufanisi kama vile kuondoa ukiritimba wa serikali kuwa ndiyo pekee inayoweza kupeleka muswada bungeni.


  Kanuni hizo mpya za mwaka 2007 ambazo zilitokana na kufanyia marekebisho makubwa kanuni za bunge za mwaka 2004, zilitoa mamlaka kwa kamati za kudumu za bunge kuwa na uwezo wa kupeleka mswada kwa ajili ya kujadiliwa bungeni na hatimaye kuwa sheria.


  Mambo mengine yaliyolipatia sifa bunge la tisa kutokana na mabadiliko ya kanuni za bunge, ni kuruhusu uwasilishwaji wa hoja binafsi bungeni, ulazima wa kamati za kudumu za bunge kushirikisha umma katika kujadili mapendekezo ya miswada mbalimbali.


  Masuala mengine ni kamati za kudumu za bunge kuwa na uwezo wa kujadili na kuwasilisha mapendekezo yao bungeni kwa ajili ya kujadiliwa, pia bunge kuwa na uwezo wa kuanzisha kamati maalumu zilizo na uwezo wa kuchunguza mambo kama ile iliyochunguza kashfa ya Richmond, uvunjifu wa haki za binadamu kwa kuchafua maji ya Mto Tigiti huko Mara.


  "Mapema kabisa Bw. Sitta aliahidi kuendesha bunge katika namna mpya. Kwa maneno yake mwenyewe alisema kuwa bunge la tisa litaendeshwa kwa 'kasi na viwango'. Kwa hakika wachambuzi wengi wanasema kuwa ameifanya kazi hiyo kwa kiwango kikubwa, kubadili mwonekano wa chombo hicho muhimu," ilisema sehemu ya ripoti hiyo.


  Ikiendelea kuchambua ufanisi wa bunge la 9 kutokana na tathimini ya miaka 5, ripoti hiyo inasema kuwa katika kutimiza moja ya majukumu yake ya msingi ya kikatiba, lilibadili na kutunga sheria kadhaa kwa maslahi ya jamii, zilizokuwa na mtazamo wa haki za binadamu, kama vile Sheria ya Mtoto ya 2009, Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Watu wenye Ulemavu (2010).


  "Katika mikutano yake 20, bunge la 9, sheria 102 zilitungwa katika mikutano 19 ukiweka pembeni mkutano wa kwanza wa Desemba 2005. Ukilinganisha na bunge la 8, bunge la 9 lilijikita zaid katika kutunga sheria ambazo kwa kweli zilikuwa na uhalisia wa mahitaji ya jamii, zikitilia maanani haki za binadamu.


  "LHRC pamoja na wadau wengine walijadili jumla ya miswada 35 kabla haijajadiliwa bungeni...LHRC ilitoa mapendekezo 21 kupitia Kamati ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, 11 yalifanyiwa kazi, 8 yalichukuliwa kama yalivyo.

  [​IMG]


  1 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... MTU MKWELI CCM HAWAMTAKI, ANGALIA SITTA ALIVYOCHAKACHULIWA KWENYE NAFASI YA SPIKA NA TIDO MHANDO ALIVYOFANYIWA TBC,NDIO UTAJUA CCM HUWA HAWAPENDI WATU WANAOWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE.BUNGE LA SASA HAKUNA CHOCHOTE ZAIDI YA KUMPONGEZA JK. WABUNGE WANAACHA KUJADILI MATATIZO YANAYOLIKABILI TAIFA KWA SASA KAMA MAJI NA UMEME,WANATUMIA MUDA MWINGI KUMPONGEZA RAIS KANA KWAMBA NCHI HAINA MATATIZO. KWA MWENENDO HUO SIJUI KAMA MATATIZO YATATATULIWA. TUMECHOKA KUSIKILIZA PONGEZI ZENU, ZUNGUMZIENI MATATIZO YA SASA YANAYOTUKABILI WANANCHI SIO MBUNGE ANAPATA NAFASI YA KUCHANGIA HOJA BUNGENI,ANAISHIA PONGEZI TUUUUUUUU HAKUNA ANAJADILI MATATIZO YA SASA YA TAIFA.
  February 10, 2011 9:10 PM [​IMG]

  Post a Comment
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Mbowe: Tutashirikiana na kamati za bunge


  Na Tumaini Makene

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa msimamo wake rasmi juu ya mwelekeo wa kambi ya upinzani bungeni, baada ya

  kubadilishwa kwa kanuni na uchaguzi wa uongozi wa kamati za kudumu za bunge, kikisema kuwa kitatoa ushirikiano wa dhati kwa wenyeviti wa kamati hizo, ilmradi wafanye kazi kwa uadilifu.

  Pia kimeweka wazi msimamo juu ya hatma ya wapinzani wote kushirikishwa katika baraza kivuli la mawaziri ambalo atalitangaza wakati wowote, kikisema kuwa suala hilo kwa sasa haliwezekani, bali litategemea kutibiwa kwa majeraha na kurudisha kuaminiana miongoni mwa vyama vya upinzani vilivyoko bungeni, hapo baadaye.


  Akizungumza na Majira jana, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho, alisema kuwa CHADEMA kinawatakiwa kila la heri wabunge wenzao wa upinzani waliochaguliwa kuongoza kamati mbili za bunge, kikiwahakikishia ushirikiano kadri utakavyohitajika.


  "Kama unavyojua kuwa kuna wabunge wa upinzani ambao pia ni wenyeviti wenzangu wa taifa wa vyama vya siasa, ambao wamechaguliwa kuwa wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge...tunawatakia kila la heri katika utendaji wao. Wasiwe na hofu, sisi tutawapatia ushirikiano wa dhati, kwani kazi waliyopewa ni kazi ya taifa na ni wabunge wenzetu, ilimuradi tu wafanye kazi kwa uadilifu.


  Kuhusu kuwashirikisha wabunge wengine wa upinzani kwenye baraza kivuli la mawaziri la kambi ya upinzani bungeni, Bw. Mbowe alisema kwa sasa, suala hilo haliwezekani kwani bado kuna majeraha makubwa na hali ya kutoaminiana kwa kiasi kikubwa miongoni mwao, tangu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, uchaguzi wa mameya, uchaguzi wa spika na naibu spika na hata matukio ya juzi katika kubadili kanuni na uchaguzi wa wenyeviti wa kamati.


  "Lakini kama unavyojua siasa ni mchezo wa ajabu sana, hakuna rafiki wala adui wa kudumu katika siasa. Hatuna chuki na yeyote, lakini hatuwezi kuunda umoja usiokuwa na maridhiano. Ushirikiano wenye mashaka unaolazimishwa au kupigiwa chapuo na CCM lazima uwe na walakini. Ushirikiano huu hauwezi kuzaa tija kwa taifa.


  "Ni hali ya kusikitisha sana kuwa wapinzani tumeruhusu CCM kiwe ndiyo blocker (dalali) wa mahusiano yetu, CCM ndiyo kinatuchagulia viongozi watakaokwenda kusimamia mapato na matumizi ya serikali yake, yaani tunaotakiwa kuwasimamia wanatuchagulia watu wa kuwasimamia. Lakini ni matendo yao ndani na nje ya bunge yanaweza kurudisha imani.


  "Kwa hiyo baraza kivuli la mawaziri ambalo nitalitangaza wakati wowote baada ya vikwazo vilivyokuwa vikichelewesha kuwa vimeondoka, halitakuwa la kudumu...linaweza kubadilika wakati wowote na kuwaingiza wapinzani wenzetu kama tutafikia maelewano ya msingi, tukaaminiana, tukajenga mahusiano mazuri ya kisiasa na kimtazamano.


  "Kwa sasa hapana. Baadaye inawezekana, hasa kwa vyama ambavyo havina ushirikiano rasmi na CCM. UDP hawana ushirikiano rasmi na CCM, NCCR pia, na TLP, lakini hata CUF ambao wana ndoa rasmi na CCM huko Visiwani, nao huwezi kujua maridhiano yatachukua muda gani, mwaka jana walikuwa wapinzani asilimia 100 leo ni hamsini kwa hamsini, huwezi kujua kesho itakuwaje, milango itakuwa wazi," alisema Bw. Mbowe.
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ahsante kwa habari hizi mwana jf
   
Loading...