Bunge la sasa kwa msiojua ni Bunge hasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la sasa kwa msiojua ni Bunge hasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Jul 13, 2011.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUNA wanaodhani eti kuna kasoro na udhaifu mkubwa bungeni hivi leo. Siamini hivyo. Hili ninadhani linatokana na yale mazoea ya kuwa na bunge ambalo lilikuwa legelege na linalolala na kuuunga mkono hata kile wasichokijua wala wasichokielewa.Bunge hili lina vijana angavu wasiotaabika na maumivu ya uzee na kamba za kichama katika kujadili yalel ya msingi yatakalosaidia bunge la kesho na keshokutwa kuwa safi na lililoelimika na kutaalamika zaidi ili kuanza kushughulikia mambo ya kitaifa katika upana na kina zaidi demokrasia na haki za binadamu katika maendeleo yake na hususan kupata mahitaji yake ya msingi.Uovyo ovyo mnaouona barabarani, masokooni, vituo vya mabasi, maofisini, vyuoni, kwenye makazi ya watu ambako hakuna utawala wa kisheria-kwa sababu tu kuna watu wanaoamini kuwa wao, lao ndilo linalostahili kusikilizwa na kufuatwa na kwamba wanaweza kuwaburuza Watanzania watambue alama za nyakati kwenye ukuta.Aidha, wakati wa kuendelea kuwadanganya Watanzania kwa statistiki au takwimu zilizopikwa na kukaangwa na walaghai wakubwa wa wakati wetu umepita na hautarudi tena. Lazima taarifa zitawaliwe na ukweli na mantiki na sio vinginevyo. Sisi tuko ndani nyie mko nje na tunawaambia bunge sasa ni tamu, na msishangae mkiona hata wabunge wawili watatu wa CCM wakiungana nasi kuikosoa serikali yao hadharani.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu upo sawa kabisa, tofauti inaonekana ktk wingi wa watu haswa wakati wa kufanya maamuzi, bunge lingekuwa balanced ufanisi ungeongezeka maradufu!
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Binafsi pia nakubaliana na wewe , juzi nilikuwa na mueshimiwa mmoja wa ccm alisema ccm inahali mbaya bungeni na kwa wananchi na hii inatokana na wabunge wa ccm kuonenekana inaitetea serikali badala ya kuisimamia kutekeleza wajibu wake so imekuwa kama mtego kwa wapiga kura kwani kila mtu sasa anapenda kusikiliza bunge kuona upinzani wanaongea nini leo kuwatetea wananchi.
   
 4. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mbunge nakubaliana na wewe! Wengi wetu wanalifuatia kwa karibu sana kujua kupitia kwa wabunge wao nini serikali inatakiwa kuwafanyia wananchi wake na kipi kipi hakijafanika! Kadri siku zinavyokwenda wananchi wanaelimika. Hawadanganyiki tena kirahisi!
   
 5. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hii ni sawa kabsa wala ccm wasijidanganye eti wananchi wako pamoja nao. Sisi tupo pamoja na waliotayari kuwakilisha matatizo yetu kama yalivyo na siyo kwa unafiki hasa wa kuipendelea serikali. Wanapaswa wajue kuwa tunapokuwa kwenye Tv tupo intrested kuona wawakilishi wetu wa kweli CHADEMA wanaiagiza nini serikali na si vinginevyo. CCM tunawajua tayari na majibu yao tunayo. Hata wakiambiwa kuwa hakuna pesa zilizotengwa wataunga mkono hoja ilimradi budget ipite ili wakagawane kilichopo. Big up CHADEMA tuko nyuma yenu.
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe kwa upande mmoja lakini pia napingana nawe kwa upande wa pili.

  Kinachokera na ambacho kinapoteza heshima ya bunge ni utaratibu wa wabunge kutoheshimu taratibu za vikao vya bunge, hata kwenye vikao vya harusi tunaheshimiana wakati wa kuzungumza. Utakuta mbunge anaongea lakini wabunge wengine hawajazima "MIC" zao, mara utasikia mwongozo wa spika, taarifa, na mbaya zaidi jni pale unaposikia wabunge wakimsema mwenzao anapochangia bila ruhusa ya spika. Kwa mfano jana sita anatoa mfano wa posho mara unasikia "so what"?? yani hata kama ni jambo la msingi lakini utaratibu unaotumiwa ni wa hovyo hata huwezi kuwalinganisha wabunge na hata wanafunzi wa darasa la tatu!!

  Nidhamu ndani ya vikao vya bunge ni zero!! na hata wabunge wenyewe inaonekana wamesahau kabisa jukumu lao la msingi hasa wa ccm wanaboa sana hata mtu ukitaka kuangalia bunge unasikiliza kwanza majina ya wachangiaji ndipo unaamua kama uangalie bunge ama usiangalie.
   
 7. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naaaaaam huo ndio ukweli
   
 8. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa upande mmoja naungana na wewe' tatizo langu lipo pale kila mbunge anavyoropoka na kumdhihaki mwingine! Pamoja na ukweli kwamba wengi wenu ni vijana,kwani hamuwezi kupingana kwa hoja mkaacha ule uropokaji'?!
   
 9. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naaaaaam huo ndio ukweli
   
 10. m

  mndeme JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ikifikia wakati mbunge anatoa hoja za ukweli alafu mwingine kutoka chama tawala anatoa taarifa ya kupotosha kwa ukweli huo ulio dhahir, ni waz kuwa uvumilivu utakushinda. Ndio maana utakuta kuna kupigana vijembe vingi sana. Bila shaka watanzania waliowengi hawajapata nafasi ya kufuatilia mijadala ya mabunge ya mataifa mengine na kujua wabunge wanaiwajibisha vp serikali, tusingekuwa tunashangaa kuona yanayotokea sasa. Muhimu tu ni kuwa pamoja na kurejea mabunge ya nchi zingine lazima utamaduni wetu kama watz uwe kipaumbele.
   
 11. j

  join9527 Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kwenye vikao vya harusi tunaheshimiana wakati wa kuzungumza. Utakuta mbunge anaongea lakini wabunge wengine hawajazima "MIC" zao, mara utasikia mwongozo wa spika, taarifa, na mbaya zaidi jni pale unaposikia wabunge wakimsema mwenzao anapochangia bila ruhusa ya spika
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
   
 12. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hayo mambo mnayoyaita nidhamu ndio yameifikisha nchi hapo ilipo kama mnataka nidhamu nendeni shuleni,au nendeni mkajifunze. Mambunge kwenye nchi zingine hata hapa jirani kenya tu yanavyofanya kazi, kama kuna mambo ya kijinga wabunge waendelee kufanya hivyo hivyo. Viongozi wa bunge spika na wenzake wanajisahau sana wanafikri wao ndio mwisho
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hasa Wenje! Sijui ni utoto tu ule akikua ataacha?
   
Loading...