Bunge la kaunti ya Mombasa: Watakao washikashika wanawake wakati wakivuka na Likoni kukiona

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Wanawake kutenganishwa na wanaume kwenye kivuko cha Likoni Feri
Hoja ya kutenganishwa kwa wanawake na wanaume katika kivuko cha likoni Feri Kenya imepitishwa bila kupingwa na wawakilishi wa bunge la kaunti ya Mombasa.

Maimuna Salim mwakilishi wa wanawake Shanzu amesma hii ni baada ya kukithiri kwa visa vya baadhi ya wanaume kumaliza ashki zao za mapezi kwa kwa wanawake katika misongamano ndani ya Feri. Wanawake kadha wamekuwa wakilia kwa kunyanyanswa kimapenzi na wanaume wakati wa kuvuka feri.

Baada ya sheria hii mijamaa ya tabia hiyo sasa itaambulia patupu.

Wakati huo huo..

Bakari Ngao amesema, Itakuwa vigumu kutenga maeneo maalum kwa wake na waume kwenye feri za Mombasa, au hata kuweka feri mahsusi za kubeba watu wa jinsia moja pekee. hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la feri nchini Bakari Ngao, ambaye anasisitiza kuwa japo kuna visa vya dhulma za kimapenzi dhidi ya wanawake ndani ya feri, kutenga maeneo maalum kwa jinsia fulani kutapelekea kupoteza kwa muda na hata msongamano katika huduma za feri.

Ila wamesema wanampango wa kuweka CCTV ili kupunguza idadi ya wanaume wanaowashikashika wanawake Sehemu za siri na Kuwachafulia ngua. Wanawake wamekuwa wakilalamika kuchafuliwa nguo

Haya yanafuatia pendekezo la bunge la kaunti ya Mombasa, la kutaka wake watenganishwe na waume wanapoabiri feri.

NB: Pale kuna wakati huwa wanaweka ferry moja inachukua magari tu na nyingine ni abiria tu,

ila msisahau hawa jamaa hawapigi mbizi kwao ferry ni free tu
 
Back
Top Bottom