Bunge la Katiba: Nani atakuwa Spika?

Hu ni mjadala uliosahaulika na nimuhimu sana kwa tanzania tuitakayo.

Kama ni anne makinda watanzania tusahau katiba tuikakayo.

Tanahitaji Spika mwingine.
 
WE kaizi kweli unamwamini 6 ambaye naye anaamini serikali 2 ndiyo msingi, hafu yeye hapitishi maamuzi bali yeye ni mwongozaji tu. Mkuu wa kaya ameshasema na hata kwenye sheria ya kuundwa bunge la katiba imeandikwa kuwa maamuzi yatapitishwa kwa kupigiwa kura hivyo 2/3 ndo ushindi wa kila kipengele.

mh sita na mzee wa vijisenti huenda wakachuana kutaka kuchaguliwa uspika habari zinadai mh sitta anaonekana kinara zaidi na anapigiwa chapuo na wengi ,bila huyu atasimamia maslahi ya wengi na kuwaambua ccm ambao hawataki serikali tatu wakti wananchi tunataka serikali tatu.
 
sitta is a coward,mnakumbuka alivyoua mjadala wa richmond baada ya kutishiwa kuporwa kadi?kwani msimamo wa ccj ni upi kwenye hii katiba?
 
sita ataharibu sana mjadala, wamweke msomi wa uchumi kutoka chuo alichosoma Obama MHESHIMIWAA ANDREW CHENGE
 
Spika wa bunge hatazamwi kwa jinsia, dini, wala zanzibar, tunahitaji spika mwenye taalumaa na anayeweza kusimamia maamuzi sahihi, ili tupate katiba iliyo bora.
 
Kwa makusudi, Jaji Warioba, Joseph Butiku na John Kabudi wamaeamua kudharau maoni ya Waislamu walio wengi katika nchi hii kwa maslahi ambayo hakika sio yatakayo jenga amani katika nchi hii.

Anyway, Wameshaambiwa kua, Rasimu sio katiba. Hoja zinaweza kuongongezwa, kubadilishwa na kufutwa ikibidi.

Alichokifanya Mheshimiwa Rais, ni kile waswahili wanakiita, Mchawi mpe mwana alee, Ili akimuua hawezi kujificha.

Waswahili wanasema, usipo uziba ufa, utajenga ukuta.

Kwa sababu haiingii akilini kudharau maoni ya kundi kubwa kama hilo katika jamii, maoni ambayo viongozi wao wote wa kidini wameyatoa. Hebu jamani jaribuni kua rational kidogo tu hapa.

Avatari yako ni sawa na matendo yako! Mnapenda sana kupendelewa kama wanawake.. Kwani nyie hamjiwezi? Mna tabu na mizimu yenu!
 
Nina maana kuwa Spika akitoka Zanzibar, Naibu atoke Bara; Spika akiwa Mwanamke, Naibu awe Mwanamme; na Spika akiwa Mwislamu, Naibu awe Mkristo. Ni mambo ya kubalance kama ambavyo Rais wetu Mhe Kikwete huwa anajitahidi kutosheleza wakati anaunda baraza ya Mawaziri, jee nimesomeka???!!!

hahaha kazi kweli vip huyo atakayetoka Zanzibar atakua Mpemba au Muunguja? Huyo atakayetoka bara atatoka Kusini,Kaskazin,Mashari au Magharibi mwa Tanganyika? Back kwenye dini atakayekua Mkristo atatoka RC,Lutheran,Pentecoste au? TANZANIA NI WAMOJA hii dhana itatupeleka kubaya kubaguana kikabila na kidini.na ukiona mtu anakaribu kutafuta ratio huyo ni Mbaguzi.
 
Nashauri ateuliwe Mchungaji Christpher Mtikila. Hapo patachimbika.

Hivi huwa mnachangia mada mkitumia akili au makalio? hivi Mtikila akiwa spika atamuda saa ngapi wa kutetea hoja ya Tanganyika? au haujui spika anatakiwa kuwa neutral?
 
hahaha kazi kweli vip huyo atakayetoka Zanzibar atakua Mpemba au Muunguja? Huyo atakayetoka bara atatoka Kusini,Kaskazin,Mashari au Magharibi mwa Tanganyika? Back kwenye dini atakayekua Mkristo atatoka RC,Lutheran,Pentecoste au? TANZANIA NI WAMOJA hii dhana itatupeleka kubaya kubaguana kikabila na kidini.na ukiona mtu anakaribu kutafuta ratio huyo ni Mbaguzi.

Nashukuru hilo jambo la ubaguzi ambalo limeanza kujitokeza nchini na ambalo lilikuwa linakemewa sana na Baba wa Taifa tangu enzi hizo. Haipendezi kupeana nafasi za majukumu kwa kuzingatia Kanda, Mkoa, wilaya, Dini, Jinsi, urafiki na Ushikaji. Tunatakiwa tuzingatie kiwango cha Elimu, Hekima na Uwezo wa kutekeleza majukumu tarajiwa. Mtu ukianza kubagua wenzako kwa Kanda, Mkoa, wilaya, Dini, Jinsi, urafiki na Ushikaji; ubaguzi hauishii hapo utakwenda hadi uguse Ukoo, familia na kaya!!! Sikiliza hi hotuba ya Baba wa Taifa aliyoitoa mwaka 1995 uburudike!!


 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: kdc
Tunahitaji weledi na si kubalance,Katiba nzuri itatokana na weledi wa mambo mbalimbali,uzalendo na matumizi ya nguvu za hoja,kwani jema na zuri likifanikishwa na muislamu mkristu hatafaidi?. na je jambo baya likifanikishwa na mwanamke halitaathiri wanawake?
 
Back
Top Bottom