Bunge la katiba lasambaratika

Bunge la katiba lasambaratika

Fue Fue

Senior Member
Joined
Jan 6, 2013
Posts
107
Reaction score
128
BMK limesambaratika kimawazo na kivitendo baada ya kugawanyika vipande zaidi ya vitatu. Katika bunge hili kuna makundi haya matatu moja kundi linaundwa na vyama vya upinzani -Ukawa, kundi la CCM na kundi la washiriki tu.

Makundi haya yameleta msongo mkubwa sana wa mawazo kwa wananchi kwani yameshindwa kuafikiana hasa nini tuliwatuma dodoma.

Tuliipa fedha nyingi sana tume ya Jaji warioba kukusanya maoni, na wote kati ya makundi haya walishiriki kutoa maoni yao binafsi na kwa kikundi. Mkusanyiko wa maoni yale ndio wanatakiwa wayajadili. Ni mshangao tu kusikia kuna rasimu kadhaa Dodoma.

Katiba sio ya chama cha siasa wala kiongozi wa chama cha siasa. Busara ni wao kujadili maoni yetu ambayo tumewakusanyia. Wajenge hoja kama wanapinga maoni yetu wayapinge kwa hoja, kisha walete hoja zao kwetu tuzipigie kura sio kutunga rasimu nyingine ili wailete kwetu. Tumewatuma dodoma kujadili maoni yetu tu sio kupeleka rasimu zao ili wazijadili.

Bunge hili litatafuna kodi za watanzania na kumalizika bila ya katiba au katiba ya chama cha mapinduzi ambayo itatumika lumumba peke yake.

Kama chama cha mapinduzi kilitaka muundao wa serikali mbili, kwanini kilishindwa kutoa maoni yake ili yawe kwenye rasimu? Je si wanasema wapo wengi ilikuwaje uwingi wao haukuonekana kwenye maoni ya rasimu pale walipokuwa wanatoa maoni ?

Ombi bunge hili liahirishwe, tuunde tume ya uchaguzi huru, ili uchaguzi mkuu upite turudi kujadili rasimu.
 
Me hata sina msongo wa mawazo juu ya ujinga wao,nna msongo wa mawazo juu ya pesa
 
Wapunbavu wanaoounga mkono upumbavu na chama cha mapepo sijawaona humu jamvini.
 
Siku nyingine fedha zetu mpango ukisambaratishwa zirudishwe tutaziita "chenji ya katiba "
 
CCM walitoa maoni kwa wingi hasa kupitia Mabaraza ya Katiba kuunga mkono Serikali 2 lakini Warioba na timu yake hawakuyagusia! Ni kama vile hayakuwepo, there is something wrong somewhere, ndio maana Warioba pamoja na kumaliza kazi yake ya uenyekiti wa Tume bado anang'ang'ania kurudia yale yale aliyokwisha kusema!
 
a disgraced jf moderator .... thanks to the principle of universe
 
CCM walitoa maoni kwa wingi hasa kupitia Mabaraza ya Katiba kuunga mkono Serikali 2 lakini Warioba na timu yake hawakuyagusia! Ni kama vile hayakuwepo, there is something wrong somewhere, ndio maana Warioba pamoja na kumaliza kazi yake ya uenyekiti wa Tume bado anang'ang'ania kurudia yale yale aliyokwisha kusema!

Kutoa maoni kwa wingi ni jambo moja na kutoa moani yenye mantinki ni jambo jingine...ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi wa swahili wanasema..
 
Tatizo la mfumo Kristo na muungano kanjanja.................Ndilo donda ndugu la Katiba mpya..............
 
CCM walitoa maoni kwa wingi hasa kupitia Mabaraza ya Katiba kuunga mkono Serikali 2 lakini Warioba na timu yake hawakuyagusia! Ni kama vile hayakuwepo, there is something wrong somewhere, ndio maana Warioba pamoja na kumaliza kazi yake ya uenyekiti wa Tume bado anang'ang'ania kurudia yale yale aliyokwisha kusema!

kama huhelewi ni bora unyamaze. jaji warioba alisema kama yafuatayo.cc kama tume tulipokua tuna wahoji wananchi tuliwambia mambo 2 watoe maoni yao kwa uwazi juu ya serikali 3 au 2 alafu watoe sababu za kwanini ni 2 au 3 sasa 2 walikosa hoja kwa nini 2 nasi 3 kulingana na uchunguzi wa kina watume pamoja na kupitia tume zote zilizo undwa tangu 1984 sasa kama hamtaki kuhelewa bakini hivyo hivyo.
 
Mkuu usiseme UJINGA wao bali UPUMBAVU wao kam prof Kabudi alivyolitolea ufafanuzi murua kwenye mdahalo wa leo ulioisha saa 12
Prof Kabud amenifanya nianze kuwafatilia na kuwajua WAPUMBAVU kupitia bunge la sasa
 
Kwan bunge hili ni la katiba? au ni la ilani ya uchaguzi wa ccm!
 
kama huhelewi ni bora unyamaze. jaji warioba alisema kama yafuatayo.cc kama tume tulipokua tuna wahoji wananchi tuliwambia mambo 2 watoe maoni yao kwa uwazi juu ya serikali 3 au 2 alafu watoe sababu za kwanini ni 2 au 3 sasa 2 walikosa hoja kwa nini 2 nasi 3 kulingana na uchunguzi wa kina watume pamoja na kupitia tume zote zilizo undwa tangu 1984 sasa kama hamtaki kuhelewa bakini hivyo hivyo.
Usipate shida huyo Buchanan yupo kundi nla WAPUMBAVU,kwa mujibu wa Prof KABUDI
 
Last edited by a moderator:
CCM walitoa maoni kwa wingi hasa kupitia Mabaraza ya Katiba kuunga mkono Serikali 2 lakini Warioba na timu yake hawakuyagusia! Ni kama vile hayakuwepo, there is something wrong somewhere, ndio maana Warioba pamoja na kumaliza kazi yake ya uenyekiti wa Tume bado anang'ang'ania kurudia yale yale aliyokwisha kusema!
Lakini mzee warioba hujamuelewa?au umemuelewa na hutak tu kukubali,au upo kundi lile alosema Prof Kabudi?kundi la WAPUMBAVU
 
Back
Top Bottom