Bunge la bajeti lianze machi

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Jan 31, 2009
7,335
3,902
Kwa wale wanaofanyia kazi serikali watakubaliana na mimi kuwa sghughuli nyingi za serikali zimesimama kabisa ukitoa mishahara kungojea kuisha kwa bunge. Miezi miwili imeshapita tangu mwaka wa fedha uanze. Hivyo ni kwa nini bunge lisianze mwezi machi au aprili kila mwaka ili ifikapo julai mosi matumizi yaanze badala ya kuwa na mwaka wa miezi kumi? Ni mawazo tu.
 
Naunga hoja mkono. Hata jirani zetu Kenya ndo hivyo wanavyofanya. Mwaka mpya wa fedha unapoaanza vikao vya bunge la bajeti vinakuwa vimeisha. Haina maana hata kdogo mwaka unaanza halafu bajeti haijapita.
 
Tuna matatizo mawili ya msingi hapa;

Kwanza, bunge linatumia muda mwingi sana kujadili whatever. Time means nothing. na ukifuatilia kwa karibu utagundua kanuni za bunge zina kipengele kinachoruhusu mbunge kuongea chochote hivyo wabunge wanatumia muda mwingi kuongea mishapo badala ya hoja. Mbunge anapewa dakika 15 kuongea, na wizara ziko nyingi.

La pili: bado hatujapata spika mbunifu (creative) ambaye atafumua uendeshaji wa bunge. Unless waangalie mfumo mzima wataendelea kukaa bungeni kwa miezi. Labda wanavutiwa na posho!
 
Back
Top Bottom