Bunge la bajeti kukaa Aprili

Bunge la bajeti kukaa Aprili

makongoromusa

Member
Joined
Feb 6, 2012
Posts
16
Reaction score
1
Katika kile kinachoitwa sintofahamu ya serikali ya CCM na namna jinsi bunge linavyoendeshwa kuna tetesi kwamba bunge la bajeti kukaa mwezi Aprili badala ya mwezi wa saba kama inavyokua ikijumuishwa na shughuli zingine za mwezi huo wa nne.

Ikumbukwe kwamba graduates wote waliomaliza kuanzia mwezi wa saba mwaka jana hawajaajiliwa kwa maaana hiyo kama tetesi hizi ni za kweli kuna uwezekano ajira zikatangazwa baada ya bunge la Aprili kama kuna mwanajamvi anataarifa sahihi juu ya hili atujuze humu.
 
Katika kile kinachoitwa sintofahamu ya serikali ya ccm na namna jinsi bunge linavyoendeshwa kuna tetesi kwamba bunge la bajeti kukaa mwezi aprili badala ya mwezi wa saba kama inavyokua ikijumuishwa na shughuli zingine za mwezi huo wa nne. Ikumbukwe kwamba graduates wote waliomaliza kuanzia mwezi wa saba mwaka jana hawajaajiliwa kwa maaana hiyo kama tetesi hizi ni za kweli kuna uwezekano ajira zikatangazwa baada ya bunge la aprili kama kuna mwanajamvi anataarifa sahihi juu ya hili atujuze humu....

Tetesi hizi ni ukweli.
Kila taasisi ya uma inaandaa budget na wameambiwa mishahara mipya iwakilishee kabla ya mwezi wa tatu.:bange:
 
Hicho ulichokisikia kina ukweli mkubwa na moja ya sababu iliyotolewa ni kuwa wabunge waliwahi hoji iweje bajeti hajapitishwa shughuli za serikali zinaendelea. hiyo hela inatoka wapi? hivyo serikali imeamua kuja na wazo hili kuwa bajeti iwe inasomwa april-june ili mwaka wa fedha wa serikali unapoanza bajeti iwe imekwisha pitishwa.

ANGALIZO: kibaya zaidi katika mfumo huo wanaotaka kuanzisha utakubalika kwa semina zinakusudiwa kufanywa kwa kamati za bunge, bajeti itasomwa na wizara husika ya fedha na ikishapitishwa tu BASI IMETOKA. kwani hakutakuwa na upitiaji wa vifungu kwa kifungu katika wizara nyingine. Mawaziri wa wizara hizo watakuwa na kazi ya kusoma mikakati ya wizara na jinsi watakavyo tekeleza mikakati hiyo full stop, na si kuoma viwango vya fedha na namna watakavyozitumia.
 
Basi kama bhageshi itakuwa tetesi hizo ni za kweli bunge litachukua muda mfupi kuliko muda tuliouzoea na hii moja kwa moja itakula kwa wabunge wetu ambao hulichekelea sana bunge hilo kwa kuvuna mamilioni.
 
Last edited by a moderator:
hawa wameona huwa wanamiss kombe la dunia na euro
 
Back
Top Bottom