Bunge la Afrika Mashariki: Wagombea wa CHADEMA na CUF waruhusiwa, NCCR na ACT Wazalendo waondolewa

Hapa kwenye 'kikristo' sasa tuone kama wapo vizuri au wataangukia pua.
 
Kumkosa yule mama Dr. Kessy wa NCCR ni pengo kubwa kwa uwakilishi wa nchi kule EALA!!
 
tanga kwetu: Una akili sana! Baada ya kuona watu waliotakiwa hasa akina Kitila wamegonga mwamba akaona bora amteue kuwa Katibu Mkuu wa maji na umwagiliaji. BUNGE NALO Likaona nalo likae kwenye kanuni. Kama kweli hawa walikiuka kanuni mbona wameruhusiwa? Kuna kanuni inayompa ruhusa msimamizi kusamehe makosa ya kukiuka sheria na kanuni?
 
Zanzibar-ASP: Chadema wanajua sana sheria. Hao wasimamizi wa uchaguzi wamejua kabisa kwamba Chadema wakienda mahakamani wanashinda. Na ushindi ulikuwa wazi hata kwa mimi nisiye mwanasheria. Ile 1/3 ilikuwa ni kwa wagombea wote na siyo kwa kila chama. Na zaidi hiyo 1/3 ni kwa wale tu watakao chaguliwa. Yaani, wale wjumbe 9 watakao chaguliwa kuingia kwenye bunge la katika kutoka Tanzania ni lazima 1/3 yao wawe ama wanawake au wanaume. Na siyo wanawake tu kama CCM walivyoelewa. Tukisema wana CCM ni mbumbumbu wanabisha. Sasa wameona? Wenye akili wameshinda. Kelele zote za jana za akina Lizaboni kwisha kazi.
 
yaani jina moja la CUF-Maalim Seif na majina matatu ya CUF-Sakaya. Chama kimoja kimeketi Halmashauri Kuu mbili na zote serikali imezikubali. Yule wa CUF-Maalim Seif hatashinda maana hatapata kura hata moja ya CCM bali mmoja wapo wa wale watatu wa CUF-Sakaya ndio atashinda
umesahau kuwa wabunge wa CHADEMA watampigia kura huyo wa CUF-Seif.
 
CHADEMA inakuzwa na CCM kila mahali utata wa kisheria unapotokea CCM wanasalimu amri au wanaangukia pua!! Sishangai Ndio maana Mama yangu makinda alikuwa hamhusishi mwanasheria mkuu wa serekali mambo ya kisheria bungeni badala yake alimpendelea Lissu!!
 
Ccm inahubiri amani huku imeshikilia bunduki na bastola mkononi.km kwa nape na Clauds,na mhucka,akalindwa kwa kusema co askari,ss km mnawapa majambazi bastola,wamtishie nape ccm mwenzenu,fufiji mnaenda kufanya nn?ushiriki wa wananchi ni muhimu kwenu rufiji tu,ila kwa nape na Claude co muhimu ! Waleeni tu hao mnaowatumia Leo kwa nape na clauds,kesho watawarudia nyie !
 
yaani jina moja la CUF-Maalim Seif na majina matatu ya CUF-Sakaya. Chama kimoja kimeketi Halmashauri Kuu mbili na zote serikali imezikubali. Yule wa CUF-Maalim Seif hatashinda maana hatapata kura hata moja ya CCM bali mmoja wapo wa wale watatu wa CUF-Sakaya ndio atashinda
Ndio watajua faida ya migogoro.Wakati Lipumba anamwita sefu wakae wajadiliane wapeleke jina moja alidhani anaitwa kuhusu mgogoro wa uongozi
 
Nadhani lile sakata la kutaka kuizua CHADEMA kwa kitendo cha kuleta wagombea wake wote wawili wa jinsia ya Kiume limekwisha, kwa maana CHADEMA walikuwa wako sahihi kwa 100%.

Kwa mantiki hiyo, katika nafasi Tisa zinazogombaniwa, nafasi mbili tayari zimeshapata washindi, yaani wagombea wawili wa CHADEMA (Wenje na Marsha) automatically ni wabunge wa bunge la Afrika Mashariki(EALA) kwa kuwa wamepita bila kupingwa.
kati ya mwanamke ni nani? naomba mtusaidie na mm najitolea ntamnunulia dira
 
Back
Top Bottom