Bunge la Afrika Mashariki: Wagombea wa CHADEMA na CUF waruhusiwa, NCCR na ACT Wazalendo waondolewa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Heshima kwenu wakuu,

Hivi sasa utaratibu wa kuomba kura na kupiga kura kwa Wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki Ushaanza.

Lakini kabla ya hayo,Katibu wa Bunge ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa EALA, Dkt Kashililah, alitolea ufafanuzi wa baadhi ya changamoto zilizotokea hapo nyuma kwa vyama vya upinzani.

Hivyo awaruhusu wagombea wa CUF na CHADEMA ambao majina yao yaliwasilishwa, kugombea nafasi hizo.

Chama cha CUF kiliwasilisha mapingamizi 2, nimepitisha wagombea wote wa CUF nilioletewa na NEC. Kitakuwa na Wagombea 4.

Nimefuta pingamizi lilitolewa na chama cha Wananchi CUF ndani ya chama cha CUF.

Vyama vya ACT Wazalendo na NCCR-Mageuzi viliwasilisha majina lakini kwa kadri ya kanuni hawajakidhi vigezo.

Vyama vya Upinzani vimeshafanyia kazi dosari zilizojitokeza na wameshawasilisha majina ya wagombea.

Nilisita kuridhia majina ya wagombea kutoka kwa Vyama vya Upinzani kutokana na kutotimiza masharti.

Wabunge watakaochaguliwa kwenda kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) ni CCM 6, CHADEMA 2 na CUF 1.
 
Katibu wa Bunge ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa EALA, Dkt Kashililah awaruhusu wagombea wa CUF na CHADEMA ambao majina yao yaliwasilishwa, kugombea nafasi hizo.

Chama cha CUF kiliwasilisha mapingamizi 2, nimepitisha wagombea wote wa CUF nilioletewa na NEC. Kitakuwa na Wagombea 4.

Nimefuta pingamizi lilitolewa na chama cha Wananchi CUF ndani ya chama cha CUF.

Vyama vya ACT Wazalendo na NCCR-Mageuzi viliwasilisha majina lakini kwa kadri ya kanuni hawajakidhi vigezo.

Vyama vya Upinzani vimeshafanyia kazi dosari zilizojitokeza na wameshawasilisha majina ya wagombea.

Nilisita kuridhia majina ya wagombea kutoka kwa Vyama vya Upinzani kutokana na kutotimiza masharti.

Wabunge watakaochaguliwa kwenda kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) ni CCM 6, CHADEMA 2 na CUF 1.
Mnyaa alifukuzwa cuf , anagombea kupitia chama gani ?
 
yaani jina moja la CUF-Maalim Seif na majina matatu ya CUF-Sakaya. Chama kimoja kimeketi Halmashauri Kuu mbili na zote serikali imezikubali. Yule wa CUF-Maalim Seif hatashinda maana hatapata kura hata moja ya CCM bali mmoja wapo wa wale watatu wa CUF-Sakaya ndio atashinda
 
Nadhani lile sakata la kutaka kuizua CHADEMA kwa kitendo cha kuleta wagombea wake wote wawili wa jinsia ya Kiume limekwisha, kwa maana CHADEMA walikuwa wako sahihi kwa 100%.

Kwa mantiki hiyo, katika nafasi Tisa zinazogombaniwa, nafasi mbili tayari zimeshapata washindi, yaani wagombea wawili wa CHADEMA (Wenje na Marsha) automatically ni wabunge wa bunge la Afrika Mashariki(EALA) kwa kuwa wamepita bila kupingwa.
 
Lisu kiboko yao
 
Back
Top Bottom