Bunge kumalizika Ijumaa kisa JK atia kwapani Hotuba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge kumalizika Ijumaa kisa JK atia kwapani Hotuba yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Nov 1, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Habari za ndani toka hapa Kilimani zinasema wanachama wa jumba la baridi safari hii watakaa hapa Dodoma wiki 2 tu na kuondoka maana hawana la kufanya zaidi .Wengi wao walitegemea kwamba hotuba ya ndugu Rais itakuwa wazi iwape kamuda ka kukamua katika lile jumba na kula mbuzi Dodoma lakini sasa imethibitika rasmi kwamba , JK aliweka hotuba yake kwapani akalala nayo mbele na ndiyo maana Spika alisema haitaweza kujadiliwa maana hata kwenye hansard hakuna kitu .

  Mimi najiuliza na nawauliza wadau wenzangu .Ni kawaida kwamba Mkulu anaingia Bungeni na kutema cheche baadaye anaweka ngoma kwapani anaondoka ? Ni kitu gani kimefichwa ambacho JK hakutaka kiwe katika records?
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Samahani ndugu Lunyungu, naomba kuuliza...je kuna sheria yeyote inayohusu mhutubu kuacha hotuba yake kwa aliowahutubia baada kuhutubia?
   
 3. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Kuna sheria inayotaka mambo ya bungeni yabaki kwenye kumbukumbu rasmi za bunge(hansard) unless spika aseme kitu fulani si rasmi kisiingie. Kwa hiyo jamani ile hotuba ya JK haikuwa rasmi? Its a national shame/scam!

  Asha
   
 4. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Bunge la vikaragosi, kwani ni lini hili bunge lilishafanya maamuzi tofauti? I think hata hapo wamechelewa, wangefunga the second day walipofika chimwaga.
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Hao wabunge si walisikiliza? na bungeni kuna marapprteurs hawakupata chochote toka kwa hiyo hotuba? Huwa hawarekodi?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo tatizo la kutowepo rekodi za hotuna ya JK Bungeni ni la Bunge lenyewe. Ile hotuba waliirekodi yote, na watumishi wa hansard walisha-transcribe, lakini cha ajabu hadi leo si hotuba tu, bali hansard ya Agosti 21, 2001 haijawekwa kwenye tovuti ya Bunge
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni lazima kila jambo lisemwapo Bungeni kumbukumbu zipatikane huko na ndiyo maana waheshimiwa wanalia lia hovyo maana wanashangaa JK kuondoka na hotuba kwapani na wameshindwa kuijadili .Nia yake kwenda Bunge ilikuwa kuweka kumbu kumbu wazi na leo hakuna .Hii ni aibu kwa Mzee huyu .Tumekosa mwelekeo na hawataki kumsikiliza Warioba .

  Je kuna mtu anaweza kuwa na undani wa kwa nini alichukua hotuba na kulala nayo mbele ?
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Namsikitikia Warioba kwa sababu anakuwa kama sauti ya mtu aliaye nyikani, mzee wa watu anaandaliwa kutwishwa mizigo kuliko ya EPA.
  Kuhusu hiyo hotuba Bunge wasitake kukwepa lolote, wanayo, kwa sauti na sofy copy, wasilikimbie hilo
   
 9. M

  Mama JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Ni kawaida bali sio sheria. Hii ndio inayowafanya hao wabunge kusinzia na kulala bungeni! inawezekanaje washindwe kudiscuss yaliyosemwa na rais kwa vile tu rais kamaliza kuhutubia na kuondoka na hotuba yake?

  Hao wanajua kila kitu, kama ada yao hawakosi kutafuta mchawi wakati mchawi ni wao wenyewe!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wakuu hebu acheni utani huu, hivi ile iliyomnasa mzee wa vijisenti akinyunyizia si ipo, lakini tuliambwia alikuwa anatafuta kiti chake usiku wa manane, sasa mnafikiri kweli hawana majibu ya hii ya hotuba ya Muungwana?

  Waulizeni tuone kama kweli hawana majibu! Sometimes tusiwe tunawa-underestimate sana as far as usanii is concerned!
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi naona na wao wako katika mgomo kama Waalimu na Wazee wa EA maana na wao mshahara wao hawajapata .Labda wawe wamepata jana lakini wote nilio kutana nao pale Dar walikuwa wanashangaa kwamba Wanawezaje kukosa mishahara yao .Nika wauliza kama wao walikuwa na tofauti na watanzania wengine kama waalimu na wazee wa EA .Wakasema we Lunyungu acha hizo kijana .

  Wanajua sana alicho kisema Rais ial hawawezi kujadili wakiwa hawana kitu maandiko .Maana Makinda kama kawaida atawaomba ushahidi wa mjadala wao kama alivyo muomba Mzee Ndesa wakati akichangia hoja .Kwa kifupi kuna magumashi hapa si bure .
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tena wakati ule Ikulu walipoulizwa kwa nini hawaitoa hotuba walisema kuwa wameomba iliyorekodiwa Bungeni ili kurekebisha yale ambayo Mkuu aliyaongezea papo kwa papo-Kwa hiyo Bunge inayo hotuba hiyo, wasitake kutuzuga
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Hili ni la bunge kwa ujumla, hapa hakuna cha makinda sita ya kware wa mkwere. Bunge liwe responsible kwa kukosekana kwa hotuba hiyo kama sheria inalazimisha iwepo. Kama hakuna sheria ya kuacha muhutubu kuacha hotuba, inakuwaje kuna sheria ya wahutubiwa kudiscuss hotuba husika kwa kuwa na ushahidi wa hotuba hiyo? Pole Watanzania.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,601
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu, sababu zote zinazotolewa sizo. Liko jambo!.
  Kisingizio cha Mh.JK. Hakuicha hotuba sio kweli. Hotuba ile iko audio recorded na video recorded na bunge wenyewe. Tbc na Star Tv walirusha live huku wakirekodi off-air. Itv walijiunga na Star Tv na Channel ten walijiunga na Tbc na zote walirekodi. Hiyo habari ya kutojadiliwa kwa kisingizio cha hansard sio kweli.

  Spika Six atuambie kweli,
   
 15. m

  macinkus JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2008
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  [/B]

  hataki usemi wake wa "UKITAKA KULA KUBALI ULIWE" ujulikane kwenye hansard

  macinkus
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa anaogopa huo usemi kukaa kwenye hansard wakati alipozungumza pale bungeni dunia yote ilikuwa inamsikiliza???!!!!
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sasa atakimbia kivuli chake hadi lini jamani .Maana kila kukicha kila afanyalo ama asemalo lazima linakuwa mwiba baada ya siku chache za watu kutafasiri .
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani sehemu iliyobaki inahitaji ujasiri wa wananchi kutenda zaidi ya kumweleza maana kama ni kuelezwa ameshaelezwa yote. Kama anajua kusoma alama za nyakati, atakuwa anafahamu kuwa hali si shwari hata kidogo. Lakini bado ana nafasi ya kutengana na mafisadi na nadhani wananchi wanaweza kumsamehe akiamua kuanza upya-lakini awe mweli, si mzugaji
   
 19. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani nyie, Mnazugwa na mnazugika. Hotuba wanayo na imeshachapwa kama kitabu. Wanaichelewesha makusudi ili ipitwe na wakati ishindwe kujadilika. Sababu kuu ni kuwepo katika hotuba hiyo hoja ya Rais kuwasemehe mafisadi ambayo ni kuvunja katiba na kudharau sheria. Imehofiwa kuwa ikijadiliwa sasa kuna wabunge watatoa hoja ya kura ya kutokuwa na imani na rais. Kwa hiyo sasa wanasubiri kesi za wale ambao wajarudisha vijisenti zifunguliwe kinasanii mahakamani halafu hotuba itawawanywa. Wakati huo hakutakuwa tena na umuhimu wa kuijadili.

  Lakini Kikwete na wajinga wenzie hawajui tu kwamba hili halimsaidii yeye wala wao.

  Asha
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mzee wa siasa za majitaka mbona alikuwa wa kwanza kusema juu ya hotuba hii kutojadiliwa , alipata maelekezo ama ilikuwaje ?Kweli kwa CCM ya sasa hakuona Mbunge anaweza kusimama na kudai hana imani na JK maana wanaweza kumgombani kama mpira wa kona .Masikini JK alama hizi hata Msekwa alishindwa kuzisoma akasombwa na mafuriko .Sie yetu macho na muda ukifika tutawakumbusha wote haya yote.
   
Loading...