Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Huu ni utaratibu wa kawaida wa ki-hasibu!!! acheni kuleta bumba humu!!! uliza wahasibu watawaambia...
Sheria siku zote huvunjwa kwa kufuata taratibu na urasimu wa serikali.
Tumefanya kazi serikalini na ndani ya mashirika ya umma, ni kweli wako wazalendo wengi tu lakini kuna manunda kibao walindwao kwa kila hila ili mambo ya kipuuzi kama haya kwa ufisadi.
Juzi amekuja Bush tumekenua kuchekele msaada wa Billion 6. Leo tunajifanya matajiri sana na wahasibu wa kukata kwa mundu kufuta madeni ya Billion 12!
Kasheshe,Masatu,Madela,
..labda wangeeleza wanaohusika na hayo madeni.
..wakati mwingine ni yale mashirika na taasisi za umma zilizoshindwa kujiendesha.
Joka,
Ndio maana nikasema la msingi hapa ni kujua/kujadili kilichopelekea madeni hayo kufutwa. Lakini kama kawaida yetu tunadandia gari kwa mbele na kuanza kukandia tu, no substance whatsoever
Maelezo mazuri sema tu umechemsha!
Huu ni utaratibu wa kawaida wa kusafisha vitabu vya serikali, kwa mfano... serikali inamdai Kasheshe ... sh. Bil. 3... lakini mazingira yanaonyesha Kasheshe hadi kufa hataweza lipa hiyo fedha au Kasheshe already amekufa...
Kinachofuata ni Serikali inapeleka bungeni tena kupitia kwenye kamati ya bunge kusema Sh. Bil. 3 anazodaiwa kasheshe haziwezi patikana hivyo tunaomba tufute hili deni. (bad dept).. period. sasa Kamati ya Bunge au Bunge linaangalia kama bado kuna uwezekano, mfano wa kuchimba kaburi ya Kasheshe ili alipi serikali wanaambiwa kachimbeni kaburi lake na alipe... kama haiwezekani bunge linakupali deni kufutwa...
Ni matumaini yangu mumuelewa what it mean.
Nakubali nimechemka lakini na wewe kubali kwamba ni kuni zinazoteketea mekoni.
Huyo kasheshe kabla hajakopa ni lazima mkopo wake uwe backed up na asset fulani. Huwezi kuamka asubuhi na kumpa mtu 1Billion hivi hivi tu.
Endapo mtu hana asset basi ni lazima adhaminiwe na mtu mwenye asset za kuaminika.
Kuchimba kaburi la Kasheshe ili kuidai fedha maiti ya kasheshe si ununda ni matokeo ya ununda, ununda wenyewe ni kumkopesha mtu kifisadi kwa sababu tu tunajua siku moja bunge litaingilia kati.