Bunge kuanzisha studio yake ya Matangazo

Bunge kuanzisha studio yake ya Matangazo

Kumbe Nape ni msemaji wa bunge na anataja hadi masharti na namna matangazo ya bunge yatakavyokuwa.Sawa yeye ni waziri mwenye dhamana lakini siyo msemaji wa bunge.
Waziri wa Habari ndiye mwenye dhamana ya kuisemea Serikali kwa jambo lolote lile. Ili kupunguza urasimu waziri husika anaweza kuzungumzia yale yaliyo ndani ya mamlaka yake.
 
Kumbe Nape ni msemaji wa bunge na anataja hadi masharti na namna matangazo ya bunge yatakavyokuwa.Sawa yeye ni waziri mwenye dhamana lakini siyo msemaji wa bunge.
Yaani inasikitisha sana,hata hiyo studio Nape Nnauye atataka iwe chini ya wizara yake.
Hilo tulishalijua sioni faida yoyote ya bunge kuwa na mradi kama huo.Baada ya studio bunge litakua na Hotel yake
 
TV studio ya bunge ili iweje? Marekani ina mabunge mawili ambayo yako busy almost mwaka mzima. Kuna studio mbili za studio (CSPAN-1, CSPAN-2) ambazo kwa kiasi kikubwa zinashughulika na matangazo ya shughuli za bunge na Ikulu. Hata hivyo TV studio hizi zinajikuta zinarudia rudia vipindi vyake kwa vile siyo rahisi kupata matukio ya kutangaza kila siku. Sasa, haka kabunge ka Tanzania kanakutana sana sana miezi 6 katika mwaka mzima kana nini cha kutangaza kupata value for money? Nadhani haya ni maamuzi na matumizi mabaya ya resources.
 
Naona hapo itakuwa boring na sidhani kama watu wengi wataangalia.

Hata BBC Parliament huonyesha mabunge yote mpaka house of commons na house of lords, Northern Ireland na Welsh lakini bado ni 1.2% ya watu ndio wanaangalia maana ni marudio na zilizorekodiwa na baadhi ni moja kwa moja.

Ushauri: Waweke mda wa kuwa na maswali kwa PM na Mayor wa jiji, na hata baadhi ya wabunge mara moja moja labda italeta maana kidogo
 
IMG_1054%2B%25281%2529.JPG

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina mpango wa kuanzisha kituo chake cha televisheni kurusha matangazo ambapo kitakuwa kikurusha matangazo ya mijadala yake yote LIVE.

Hali hii itaviwezesha vituo vingine kuchukua matangazo kutokea katika kituo hicho ambacho bado hakijafahamika jina lake, tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichukua matangazo TBC.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa habari, michezo, utamaduni na watendaji wa serikali mikoa ya Mbeya na Songwe.

Amesema kutokana na hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya kuanzisha studio yake hivyo kutoa fursa kwa televisheni nyingine kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo.

Amesema shirika la utangazaji la Taifa, TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya Bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa likitumia bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo, uamuzi huo ulikuwa sahihi licha ya wananchi wengi kuonesha kutoridhishwa.

Source: Bunge laanzisha studio kuzipa Tv zote fursa ya kurusha "LIVE" vikao vya mikutano - wavuti
huu ni usanii katika ubora wake. hicho kituo kinaweza kuchukua hata miaka 10 kuanzishwa mpaka huyo mshua atakapotoka.
 
Wapatie ruhusa vituo vya TV binafsi kama kweli serikali haina hela ya kugharamia TBC na serikali kubana matumizi.

Kwa njia ya kuwapatia nafasi vituo binafsi vya TV kurusha Bunge ''live'' serikali itakuwa imepunguza gharama za kuajiri ''wafanyakazi wa studio ya Bunge'' ambayo watalipwa mshahara, bunge kuchangia makato ya pensheni ya wafanyakazi wa studio, overtime, payroll, vitendea kazi n.k nafikiri hazitapungua Tshs. Billioni 4 iliyokuwa inatumiwa na TBC kurusha matangazo.
 
Hiyo ndo kupunguza matumizi? Mbona wanahaha? Wanaogopa nn? Ili wafiche madudu yao? Ukawa hilo tunaliona taften njia nyingine
 
IMG_1054%2B%25281%2529.JPG

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina mpango wa kuanzisha kituo chake cha televisheni kurusha matangazo ambapo kitakuwa kikurusha matangazo ya mijadala yake yote LIVE.

Hali hii itaviwezesha vituo vingine kuchukua matangazo kutokea katika kituo hicho ambacho bado hakijafahamika jina lake, tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichukua matangazo TBC.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa habari, michezo, utamaduni na watendaji wa serikali mikoa ya Mbeya na Songwe.

Amesema kutokana na hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya kuanzisha studio yake hivyo kutoa fursa kwa televisheni nyingine kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo.

Amesema shirika la utangazaji la Taifa, TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya Bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa likitumia bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo, uamuzi huo ulikuwa sahihi licha ya wananchi wengi kuonesha kutoridhishwa.

Source: Bunge laanzisha studio kuzipa Tv zote fursa ya kurusha "LIVE" vikao vya mikutano - wavuti
Duu sasa hapo c ndo fisi atakuwa amepewa mfupa wape aliousubiria kwa muda mrefu!?
 
Sasa hiyo gharamaza ya kuanzisha kituo na kuendesha kituo,si wapewe tu TBC waendelee na matangazo!Akili za viongozi wa ccm bana!
 
Sasa ule mpango wa kudhibiti habari za bunge Ndio utakuwa umekamilika, habari hazitoki tena
 
HII YOTE NI JANJA YA NYANI KUWAFICHA MATUKIO MUHIMU KWA UMMA POMOJA NA HAYO NI SAWA NA KUCHOCHEA MOTO UTAWACHOMA !
 
we hapo ndio umeuchemsha!?!
na pesa za bunge zinatoka wapi?
wee kiazi, TBC ndio inapunguza katumizi. muda mwingi imekuwabikijiendesha yenyewe. sasa kama pesa ya bunge inatoka TBC yatakuwa maajabu
 
Back
Top Bottom