Wizara ya habari, utamaduni, wasanii na michezo ndio wizara ambayo kwa kushirikiana na wizara zingine (ajira, kazi na elimu) ingeweza kuweka mikakati ya kuongeza ajira na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.
Kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wa nje na ndani, ingewezekana kwa kiasi fulani kuweka mifumo ya kitaifa na kimataifa itakayowatoa vijana wa kitanzania kutoka katika upofu na umasikini wa fikra walio nao.
Lakini cha kusikitisha, waziri wa wizara hii, Nape Nnuye amejikita kwenye juhudi za kufungia vyombo vya habari vyenye mlengo tofauti na chama chake, kudhibiti uhuru wa habari na sasa anataka kutuletea kituko kingine. Kwamba kutakuwa na studio ya bunge itakayokuwa inarusha matangazo ya bunge, na vyombo vingine vya habari vitaruhusiwa tu kuchukua matangazo kutokea huko. Yaani hakutakuwa na uhuru wa kuchukua habari moja kwa moja kutoka bungeni isipokuwa kutokea kwenye studio ya bunge.
Hii yote inaashiria juhudi za Nape Nnauye kuwanyima watanzania taarifa halisi kutoka kwa wawakilishi wao waliowachagua.
Nape hataki watanzanua waone akina Tundu Lissu wanavyomfundisha sheria mwanasheria wa serikali anapojaribu kupindisha kanuni kwa ushabiki wa kichama ili kitumbua chake kisiingie mchanga. Anataka kuweka studio itakayoedit na kufuta baadhi ya matukio kwa faida anazojua yeye.
Kitu ambacho Nape Nnauye hajui au amesahau ni kwamba kwa kiwango cha teknolojia kilichopo sasa hivi, vifaa kama saa za mkononi, pete, kalamu, vifungo vya shati, bangili, hereni, na of-course simu za mkononi zinaweza kutumika kurekodi matukio na kuyarusha mitandaoni.
Anachokifanya Nape ni kuongeza matumizi ya internet na kunufaisha makampuni ya simu, kwa sababu wananchi wakishajua kwamba habari za bunge zinatengenezwa, na baadhi kufutwa, hawataamini vyombo vya habari, watahamia kwenye mitandao kuangalia uhalisia kama itakavyokuwa imerekodiwa na waliomo bungeni.
Kwa hiyo wazo la Nape, kama ni kutaka kuficha ushirikina wa bunge, limeshindwa kabla halijaanza kutekelezeka. Na vyombo vya habari vikitaka kupoteza 'credibility' kwa wananchi, vikitaka kukimbiwa na watazamaji viunge mkono akili hii ndogo ya Nape Nauye.
'Akili za kupambana na vikundi vya kisiasa wakati mtu ni waziri anayetakiwa kutumikia umma wote, haziwezi kusogeza mbele taifa hili'.
Nape aache, kupambana na vyombo vya habari vinavyoiweka serikali ya chama chake uchi. Apambane na tatizo la ajira kwa vijana, wizara yake ina jukumu hilo. Hapo ndipo anaweza kujenga 'legacy' yake kiuongozi. Other wise, ataendelea kuwa 'Nape Nauye'.