Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina mpango wa kuanzisha kituo chake cha televishesni kurusha matangazo ambapo kitakuwa kikurusha matangazo ya mijadala yake yote LIVE.
Hali hii itaviwezesha vituo vingine kuchukua matangazo kutokea katika kituo hicho ambacho bado hakijafahamika jina lake, tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichukua matangazo TBC.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa habari, michezo, utamaduni na watendaji wa serikali mikoa ya Mbeya na Songwe.
Amesema kutokana na hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya kuanzisha studio yake hivyo kutoa fursa kwa televisheni nyingine kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo.
Amesema shirika la utangazaji la Taifa, TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya Bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa likitumia bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo, uamuzi huo ulikuwa sahihi licha ya wananchi wengi kuonesha kutoridhishwa.
Chanzo: Bunge laanzisha studio kuzipa Tv zote fursa ya kurusha "LIVE" vikao vya mikutano - wavuti