Bunge isimamieni serikali


A

Apes

Member
Joined
Nov 20, 2016
Messages
25
Likes
3
Points
5
A

Apes

Member
Joined Nov 20, 2016
25 3 5
Wana jamvi leo nimekuja hapa kuliomba bunge letu liisimamie kikamilifu serikali kwani bila hivyo hatuwez fika salama.

Nimesikitishwa sana na Chuo kikuu kimoja maarufu cha jijini Mwanza kutoa majina machache ya wahitimu huku maelefu ya wahitimu wakishindwa kuhitumu kwa kuwa serikali kupititia bodi ya mkopo imeshindwa kuwalipia ada ya semister ya 2 mwaka huu.
Serikali isikomae tu kutunga sheria kali za ukusanyaji wa mikopo kwa wadaiwa, bali itunge pia sheria ya kuibana bodi iwapo itashindwa kulipa ada kwa wahusika kwa muda.

Hii ni hatari sana, mtu unaingia naye mkataba umkopeshe, halafu hutaki hata kumpa huo mkopo...hii ni aibu kubwa kwa taifa, ambalo liliahidi kuwa mikopo haitakuwa shida tena.

Hivi inakuaje, mtu umkopeshe na unataka arudishe kwa mda na riba juu, ila katika kumkopesha unasuasua? Ni aibu kubwa..naomba kuwasilisha
 

Forum statistics

Threads 1,274,979
Members 490,865
Posts 30,529,417