Usisahau kuwa Rais amechaguliwa ba wananchi pia, tena wengi kuliko mbunge yeyote yule. Wapiga kura ni "wateja" wake pia. Hiyo TV ya bunge live ataitazama nani wakulima wako shambani watoto wako shuleni na wafanyakazi wako kazini?Tumeona bunge lilivyoanza, kamati zimepangwa, wanalazimisha hata zile kamati ambazo kikawaida huongozwa na wapinzani, wanataka ziongozwe na watu wa CCM, hii ni ajabu, wanaweka chama mbele ya maslahi mapana ya umma.
Zikaja sherehe za kumkaribisha mgeni baada ya kulihutubia, akawapangia wenyeji pesa zitumike vipi! , hapa namuunga mkono Rais kwa sababu kimsingi pesa zile zingetumika mara moja tu bila faida sana kuliko zilivyokuja kufanya shughuli nyingine, hata hivyo pamoja na hayo nilitegemea bunge ndo liwe la kwanza kuliona na pia wawe na power ya kusema well, umekuja na wazo zuri sana HATA HIVYO SISI NI MHIMILI UNAOJITEGEMEA, whether we are right or wrong tutatafuta namna zetu za kujisahihisha.
Bunge kuridhia kutoonekana Live, ilipaswa Bunge lisimame kuiambia serikali kuwa, sisi ndo tumepitisha bajeti ya bilioni nne ili wateja wetu (yaani wananchi) watuone, cha ajabu Waziri Nape alipounguruma bungeni kuhusu kutorushwa bunge live, Ndugai na Kina Kashilila wakasarenda! , Hii labda inatokana na wao kutotambua ni kwa kiasi gani Mhimili wao ni muhimu kwa wananchi. walipaswa kutetea kazi yao ionekane na waliowatuma ( wananchi) siyo kukaa kimya tu huku Serikali ikionekana kupata leeway.
Kiti kingine, siyo kazi ya bunge kutengeneza madawati au kununua dawa, lakini ni kazi ya bunge kuhakikisha kuwa wanaisimamia serikali ili inunue hayo madawati, na pia ni kazi ya bunge kufanya kila iwezekanavyo kutuonyesha sisi wananchi jinsi wanavyoifanya kazi yetu ya kutuwakilisha kuisimamia serikali. Nilitegemea basi, hizo bilioni Sita walizozirudisha serikalini zinatumika kwa dharura kutuonyesha Bunge Live.
Kiufupi bunge inabidi lijitambue kuwa ni mhimili huru wa Dola, haitakiwi lifanye kazi kama idara ya serikali. lazima liwe imara, tena imara kwelikweli.
Usisahau kuwa Rais amechaguliwa ba wananchi pia, tena wengi kuliko mbunge yeyote yule. Wapiga kura ni "wateja" wake pia. Hiyo TV ya bunge live ataitazama nani wakulima wako shambani watoto wako shuleni na wafanyakazi wako kazini?
ITV ilimtenbeza Lowassa nchi nzima kwa nini sasa isitangaze bunge live? Wapinzani waliisaliti nchi wakakaa na MCC eti wafute misaada, wambieni wazipeleke bunge.
Sio tuu Bunge Butu, bali hata Spika Butu...Tumeona bunge lilivyoanza, kamati zimepangwa, wanalazimisha hata zile kamati ambazo kikawaida huongozwa na wapinzani, wanataka ziongozwe na watu wa CCM, hii ni ajabu, wanaweka chama mbele ya maslahi mapana ya umma.
Zikaja sherehe za kumkaribisha mgeni baada ya kulihutubia, akawapangia wenyeji pesa zitumike vipi! , hapa namuunga mkono Rais kwa sababu kimsingi pesa zile zingetumika mara moja tu bila faida sana kuliko zilivyokuja kufanya shughuli nyingine, hata hivyo pamoja na hayo nilitegemea bunge ndo liwe la kwanza kuliona na pia wawe na power ya kusema well, umekuja na wazo zuri sana HATA HIVYO SISI NI MHIMILI UNAOJITEGEMEA, whether we are right or wrong tutatafuta namna zetu za kujisahihisha.
Bunge kuridhia kutoonekana Live, ilipaswa Bunge lisimame kuiambia serikali kuwa, sisi ndo tumepitisha bajeti ya bilioni nne ili wateja wetu (yaani wananchi) watuone, cha ajabu Waziri Nape alipounguruma bungeni kuhusu kutorushwa bunge live, Ndugai na Kina Kashilila wakasarenda! , Hii labda inatokana na wao kutotambua ni kwa kiasi gani Mhimili wao ni muhimu kwa wananchi. walipaswa kutetea kazi yao ionekane na waliowatuma ( wananchi) siyo kukaa kimya tu huku Serikali ikionekana kupata leeway.
Kiti kingine, siyo kazi ya bunge kutengeneza madawati au kununua dawa, lakini ni kazi ya bunge kuhakikisha kuwa wanaisimamia serikali ili inunue hayo madawati, na pia ni kazi ya bunge kufanya kila iwezekanavyo kutuonyesha sisi wananchi jinsi wanavyoifanya kazi yetu ya kutuwakilisha kuisimamia serikali. Nilitegemea basi, hizo bilioni Sita walizozirudisha serikalini zinatumika kwa dharura kutuonyesha Bunge Live.
Kiufupi bunge inabidi lijitambue kuwa ni mhimili huru wa Dola, haitakiwi lifanye kazi kama idara ya serikali. lazima liwe imara, tena imara kwelikweli.
Hii iishie humu humu jf, ikitoka tuu nje, ikachapishwa na gezeti lolote, jiandae kuitwa Dodoma!.Asalaam Tanzania! bilashaka mmejibu kazi iendelee.
binafsi nimehuzunishwa sana na kauli ya SPIKA akiwa bungeni siku ya alhamisi tarehe 8/4/2021 yakuwa
"MKUBWA akishasema wengine inabidi tukae kimya"
Aliyasema hayo akirejea maoni yake kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambapo alisema rais alishauriwa vibaya.
Kiukweli kauli hii inaonesha udhaifu MKUBWA katika taasisi ambayo ilipaswa kuheshimika na kusikilizwa sana! Taasisi ambayo ni mhimili mkuu, taasisi ambayo inapaswa kuisimamia serikali, kutunga sheria na kutupa bajeti bora kwa maendeleo ya kweli kwa taifa letu.
Kistaarabu kauli ile (YA AIBU) ilipaswa kufutwa kwenye Hansard kwani inawafundisha wabunge ambayo wengine niwageni sio tuu kutoshauri kitu mkubwa (rais) akishakiongea! Bali kuwa waoga! bubu! na kutowasilisha matakwa ya wananchi waliowachagua!
Endapo kiongozi wako ananyamazishwa wewe uliye chini yake utasema nini?
Na huu ni uthibitisho mwingine yakuwa serikali ililiweka bunge mkononi na kuliamulia vyakusema, kwa bunge la namna hii tusitarajie maendeleo hili ni 'rubber stamp' ya nini serikali inataka.
Si ajabu sasa kuona wooote waliokosoa serikali waziwazi wametupwa pembeni kwenye uchaguzi wa aibu wa 2020. Sio ajabu kusema wabunge wa upinzani kupitia viti maalumu kuingia bungeni litakuwa ni agizo toka kwa MKUBWA kwenda kwa MDOGO.
Mhimili umegeuka sio mhimili tena,haustahimili kulibeba taifa na hauwezi. Udhaifu huu ni lazima tuuongee bila kukubali kuogopa vitisho na mateso yanayoweza kutekelezwa juu yetu! Tupaze sauti tulikatae.
BUNGE LA AIBU, AIBU, AIBU TUPU!