Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Tumeona bunge lilivyoanza, kamati zimepangwa, wanalazimisha hata zile kamati ambazo kikawaida huongozwa na wapinzani, wanataka ziongozwe na watu wa CCM, hii ni ajabu, wanaweka chama mbele ya maslahi mapana ya umma.
Zikaja sherehe za kumkaribisha mgeni baada ya kulihutubia, akawapangia wenyeji pesa zitumike vipi! , hapa namuunga mkono Rais kwa sababu kimsingi pesa zile zingetumika mara moja tu bila faida sana kuliko zilivyokuja kufanya shughuli nyingine, hata hivyo pamoja na hayo nilitegemea bunge ndo liwe la kwanza kuliona na pia wawe na power ya kusema well, umekuja na wazo zuri sana HATA HIVYO SISI NI MHIMILI UNAOJITEGEMEA, whether we are right or wrong tutatafuta namna zetu za kujisahihisha.
Bunge kuridhia kutoonekana Live, ilipaswa Bunge lisimame kuiambia serikali kuwa, sisi ndo tumepitisha bajeti ya bilioni nne ili wateja wetu (yaani wananchi) watuone, cha ajabu Waziri Nape alipounguruma bungeni kuhusu kutorushwa bunge live, Ndugai na Kina Kashilila wakasarenda! , Hii labda inatokana na wao kutotambua ni kwa kiasi gani Mhimili wao ni muhimu kwa wananchi. walipaswa kutetea kazi yao ionekane na waliowatuma ( wananchi) siyo kukaa kimya tu huku Serikali ikionekana kupata leeway.
Kiti kingine, siyo kazi ya bunge kutengeneza madawati au kununua dawa, lakini ni kazi ya bunge kuhakikisha kuwa wanaisimamia serikali ili inunue hayo madawati, na pia ni kazi ya bunge kufanya kila iwezekanavyo kutuonyesha sisi wananchi jinsi wanavyoifanya kazi yetu ya kutuwakilisha kuisimamia serikali. Nilitegemea basi, hizo bilioni Sita walizozirudisha serikalini zinatumika kwa dharura kutuonyesha Bunge Live.
Kiufupi bunge inabidi lijitambue kuwa ni mhimili huru wa Dola, haitakiwi lifanye kazi kama idara ya serikali. lazima liwe imara, tena imara kwelikweli.