Bunge bora kuliko mabunge yote yaliyo wahi kuendeshwa hapa TZ ni bunge la sasa

abduel paul

Senior Member
Nov 23, 2010
133
5
Nina kila sababu ya kusema hivi, kwani kabla ya mwana JF yoyote kujibu hii mada, apate walau muda mfupi wa kuitafakari, kwanza ni bunge ambalo wabunge wana hoji kila jambo, kwani hakuna anaye bisha kwamba mabunge yoote yaliyo pita ndiyo mabunge yaliyopitisha na kuleta matatizo makubwa katika nchi yetu, wakati mwingi walikua wanalala bungeni, na kusema ndioooooo!!!! Imepitaaaaaa!!!!! lakini sasa tumeona ilivyo kila bajeti na muswada unaoletwa kujadiliwa unahojiwa kila nyanja na kila jambo, kwanini tusilione bunge hili kuwa ni bora? upendeleo wa kutoa nafasi ni jambo la wazi ambalo linaonekana pale bungeni wakati mwingine tumekuwa tunashuudia hata Spita mwenyewe au naibu wake, au wenye viti wake, kwa kuwahofia mawaziri utakuta wanajisahau nakujikuta wanapata vigugumizi na kutaka kuwaita wao viongozi hali wao ndio viongozi, pale bungeni ndipo ambapo mbunge kamuuliza swali waziri 1 + 1 ni ngapi? waziri anajibu 1,000/- Spita anasema vizuri, haya swali la nyongeza, yaani spika haoni hata haja ya ku annalyse majibu yanayotolewa heti kwakuwa tu yameulizwa na mbunge, nini sababu ya yeye kuwa kiongozi??? Mbunge anaunga mkono hoja 100% wakati kakosoa kila kona ya hoja iliyo tolewa, na hapo inaonekana kuwa sawa!!! why???

Kwanini isiwe, Naunga mkono hoja kwakuwa sioni kasoro ya hoja iliyo tolewa! au nataka jambo au mambo fulani yatolewe maelezo na kurekebishwa ndipo niunge mkono hoja!! Embu tuangalie Bunge letu kwa jicho la tatu. sasa pale ni pamoto kwa kila waziri na mtendaji mimi nina imani hiyo! nidhamu wanayo itaka wazee, na waTZ wachache itatufunga kiakili, mi ujinga, tunataka watu wanao hoji ikibidi hata kuvunja hiyo nidhamu kwani kwasasa haita tusaidia,

ni wakati wa mabadiliko ya kweli kwa nchi yetu. Mabadiliko ya kiufahamu ndio chanjo cha mabadiliko yote, najua kwamba huu ni mwanzo tu bado mengi yanakuja lazima tanzania iwe mahali inapostahili kuwa, yaani kuwa na maendeleo yanayolingana na rasilimali tulizonazo

Lakini itatupasa watanzania tufanya maamuzi makubwa kwa uchaguzi ujao kwani nchi hii ikiendelea kutawaliwa na ccm hatutafika popote, tujiandae kuwabwaga 2015

Kwa kuwa sheria nyingi zilizopitishwa na mabunge yaliyopita zimekuwa chanzo cha wageni kufaidi rasilimali zetu kuliko Watanzania,
na kwa kuwa miswaada huandaliwa serikalini na wataalamu wenye elimu ya shahada ya kwanza na kuendelea, na kwa kuwa mswaada hujadiliwa bungeni na hatimaye kupitishwa kuwa sheria;
napendekeza kuanzia uchaguzi ujao, sifa ya mgombea ubunge awe na uwezo wa kuuchambua na kuelewa faida na hasara ya kila mswaada unaoletwa bungeni hivyo lazima awe na angalau shahada ya kwanza katika fani yeyote.

Nisahihi kabisa, watanzania tunapaswa kuwa na uthubutu, daima nauzunishwa na maneno ya wanasiasa matijiri ambao wamekwisha pata mali na sasa wanahubiri kulinda amani, ni amani gani inayo hubiriwa ikiwa wapo watu hata mlo mmoja ni kwataabu? hakuna ukosefu wa amani mbaya kama uliopo moyoni, kwani ndio unaopelekea kuvunja kwa amani nyingine, masononeko watanzania kila siku wakisikia heti uchumi umepanda hali bidhaa zinazidi kupanda bei kila uchwao, maisha yanadidimia kila siku, asilimia kubwa ya waTZ hata maana ya uo uchumi unaelezwa katika nyanja gani haujulikani, wanao kiini macho tu, heti tushangilie miaka 50 ya uhuru hali mioyoni mwa wa TZ wangali Utumwani, wamefungwa na umaskini, tena unao zidi siku hata siku, ni Uhuru gani uo????

napendekeza kuanzia uchaguzi ujao, sifa ya mgombea ubunge awe na uwezo wa kuuchambua na kuelewa faida na hasara ya kila mswaada unaoletwa bungeni hivyo lazima awe na angalau shahada ya kwanza katika fani yeyote.
Mkuu unafikiri hawajui faida na hasara hapana ni ushabiki tu na itikadi ndizo zinazotawala wakati wa kujadili.

Asee yanayojadiliwa katika bunge hili yakitendewa kazi,aaaah Tanzania itakua kama Kenya badae kama China!

Mkuu unafikiri hawajui faida na hasara hapana ni ushabiki tu na itikadi ndizo zinazotawala wakati wa kujadili.

Bunge la sasa lina changamoto zake kutokana na uwezo wa uchambuzi wa wabunge vijana ambao wengi wanashahada. Miaka ya nyuma sidhani kama wabunge waliweza kuchambua hoja za serikali kama ilivyosasa vinginevyo tusingeambulia Shs 3 kwa kila 100 inayopatikana kwa kuuza dhahabu yetu.

Kuna wana magamba kila kukicha wanasema eti bunge limejaa vurugu na halijadili mambo ya maana. Mimi nawaona watu kama hawa wanataka tuendelee kuwa na wabunge wa upinzani kama akina cheyo na Mrema.

Hili ndo bunge bwana sisi tunalifurahia na hatakama watapigana ilimradi iwe ni kwa kutetea maslahi ya wanyonge. Mambao yakulifanya bunge mhuri wakupitishia deal za akina NGEREJA HATULITAKI!

Hivi huwajui watu kwa nongwa watakwambia ubaguzi,,,,,,,,wakat katiba inapinga,
Kwa kuwa sheria nyingi zilizopitishwa na mabunge yaliyopita zimekuwa chanzo cha wageni kufaidi rasilimali zetu kuliko Watanzania,

na kwa kuwa miswaada huandaliwa serikalini na wataalamu wenye elimu ya shahada ya kwanza na kuendelea, na kwa kuwa mswaada hujadiliwa bungeni na hatimaye kupitishwa kuwa sheria;

napendekeza kuanzia uchaguzi ujao, sifa ya mgombea ubunge awe na uwezo wa kuuchambua na kuelewa faida na hasara ya kila mswaada unaoletwa bungeni hivyo lazima awe na angalau shahada ya kwanza katika fani yeyote.

Haswa! Ni Bunge ambalo idadi ya wabunge wa upinzani imeongezeka ambayo wengi wao ni vijana wasomi na wajuzi wa mambo, pia ni bunge ambalo limeonyesha kufanya kazi yake ya kuikosoa serikali vyema, imeitia hofu chama tawala kiasi cha kufanya spika, naibu spika na wenyeviti wa vikao vya bunge kujichukulia maamuzi magumu kuinusuru serikali!

Kuna wana magamba kila kukicha wanasema eti bunge limejaa vurugu na halijadili mambo ya maana. Mimi nawaona watu kama hawa wanataka tuendelee kuwa na wabunge wa upinzani kama akina cheyo na Mrema.

Hili ndo bunge bwana sisi tunalifurahia na hatakama watapigana ilimradi iwe ni kwa kutetea maslahi ya wanyonge. Mambao yakulifanya bunge mhuri wakupitishia deal za akina NGEREJA HATULITAKI!

unachosema ni sawa sana! Kama waTZ hawajui cc tupo nyuma miaka 60 kimaendeleo ukilinganisha na ambavyo 2ngepaswa kuwa, na maliasili 2lizonazo, nilishangazwa na Rais we2 Kikwete kumwambia Magufuli ana2mia ubabe, mm mtazamo wangu alitaka kujijengea jina aonekane muungwana, ktk hali ambayo kachelewa sn, nchi ye2 inataka wa2 wanao thubu2, kusema km wapinzani, hakuna neno la upole au la taratibu km ambavyo Lema alisoma bungeni mapendekezo yao, km kuua ni nino kali palipo na mauaji anaye ripoti ilo kwa wananchi asemeje? Askari amemfanya m2 azimie kidogo kwa risac jamani wananchi mcjali? Ndivyo hv? 2nataka watendaji km magufuli, 2lipo hapa ni nyuma sn zaidi ya hiyo miaka 50 heti ya uhuru, wkt mwingine najiuliza km wananchi hawatavunjiwa nyumba na kufidiwa wapi barabara zitajengwa? Km makosa yalishafanywa hakuna jinc ni kurekebisha kwa maumiv kidogo ili 2songe, vnginevyo 2tabaki 2naesabu namba za miaka, ktk maendeleo ambayo hata nchi ingeachwa yenyewe ingesonga zaidi hata ya hapa na pengine 2meitia ukiwa na kusababisha majanga,

Yaani bunge le2 kwasasa hata km uliingia bungeni kutoka kijijini uko unaburuta miguu sasa unatembea kwa kurukaruka wabunge wa sasa watahoji, ni bunge ambalo halitaruhusu matatizo kuwa sheria heti kwashinikizo la chama, bunge ambalo hata vyombo vya habari vnawarusha hewani na magazetini kwa kejeli wale wanao lala hovyo, bunge ambalo kila neno na matamshi yanarekodiwa yawe upande wa chama tawala au upinzani,

Back
Top Bottom