Bunduki ya Nassari yachunguzwa

Bunduki ya Nassari yachunguzwa

Hapa Nassari ana kesi ya kujibu.maganda ya risasi yote ya bunduki yake na za majambazi hata ganda moja halijapatikana eneo LA tukio.Kitu ambacho si cha kawaida.Maganda yangeonekana polisi wangeyapata
Hawa polisi walishayakusanya na kuyaficha.
 
Huyu jamaa ana akili za kitoto sana. Enzi zile za JK alitakaga nchi ya Kilimanjaro. Sasa naona anataka kumjaribu JPM. Ni vizuri akamuuliza mwenzie Lema kwa nini siku hizi kaufyata.
 
Hizi pombe hizi, mbwa kudaka rambo ya kitimoto unampa ya kichwa kweli!
 
Risasi kikawaida hununuliwa kwa kibali mfano ukiuziwa kumi ukizitumia unatoa maelezo ulizitumia wapi Hizo risasi anazosema Nassari alipiga hewani siku hiyo mmm zitizamwe vizuri isije kuwa aliitumia hiyo bunduki kupiga kwingine kumpiga MTU asiye julikana akaona anafuatiliwa akampiga mbwa risasi moja kumuua na kusingizia zingine alipiga hewani ili aseme zingine zilitumika hapo ambapo hakuna ushahidi wa risasi iliyorushwa angani wala ganda LA risasi .Polisi ichunguze bunduki na pistol za wote waliohudhuria mazishi ya mbwa akiwemo Godbless lema jeshi LA polisi liwawahi chap chap
Ni kweli kabisa mkuu.
 
Kama aliweza kupiga risasi kupitia bunduki yake hapo amewarahisishia kazi polisi, hakuna kitakachoendelea zaidi ya kuambiwa kuwa alijivamia mwenyewe na risasi zilizompiga mbwa zilifyatuliwa na Nassary mwenyewe.
 
Naamini uchunguzi utakuwa rahisi sana kwa polisi kwa kuxingatiscweledi walionao. Hata hivyo wanaweza anzia kama ifuatavyo:
1.Maganda 20 ya risasi za " wavamizi' yatafutwe
2.Maganda ya risas akizitumia Nassari yatafutwe
3.Aina ya risasi aliyopigwa mbwa ichunguzwe
4.Wote waliolala ndani ya mji wa nassari siku ya tukio na siku za karibuni wahojiwe
5.Majirani wote hasa nyumba za karibu wahojiwe
6.Mwenyekiti/Mtendaji wa mtaa au kijiji wahojiwe
I'm sure kwamba ikiwa kila MTU atahojiwa maswali yaleyale separately na watu tofauti then majibu yatapatikana haraka.
 
Waanze na 'boss wa mkoa' kwani kuna clip moja anakabidhi pikipiki ile kauli yake ni ya hatari na inatisha.
 
Maganda 20 ya risasi za " wavamizi' yatafutwe
Maganda ya risas akizitumia Nassari yatafutwe
Aina ya risasi aliyopigwa mbwa ichunguzwe
Wote waliolala ndani ya mji wa nassari siku ya tukio na siku za karibuni wahojiwe
Majirani wote hasa nyumba za karibu wahojiwe
Mwenyekiti wa mtaa au kijiji wahojiwe
Kibao kinaweza geuzwa naapa! chezea wewe!
 
View attachment 643738
Wakati mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari akilihusisha tukio la kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na masuala ya kisiasa, polisi inashikilia bunduki ya mwanasiasa huyo kwa uchunguzi.

Polisi mkoani Arusha imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kuwasaka washukiwa, huku ikichunguza silaha ya Nassari aina ya shotgun, ikisema tukio hilo lina utata kutokana na mazingira lilivyotokea.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo aliliambia gazeti hili kuwa wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la.

“Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,” alisema Mkumbo.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema msako unaendelea ili kuwabaini washukiwa na kwamba hawajapata maganda ya risasi zinazodaiwa kutumika katika uvamizi huo.

Juzi Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa nusu saa baada ya kuwasili nyumbani kwake alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyumba na baadaye kulisikika milio ya risasi. Alisema mbwa wake aliyekuwa akibweka alinyamaza, hali iliyomfanya achukue silaha yake kujihami.

“Nilipiga risasi tano, kisha kukawa kimya nikaenda kuwaamsha vijana wanaonisaidia hapa nyumbani kuwaeleza tukio lililotokea kisha nikaondoka.”

Alisema waliofanya tukio hilo hawakujua kama ana silaha kwa sababu mwaka 2014 wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, bastola yake ilichukuliwa na polisi na hadi leo haijarudishwa, hivyo kuwa na silaha nyingine kulimsaidia kujibu mapigo.

Katika tukio hilo, Nassari alisema aliwajibu watu hao kwa kupiga risasi tano hewani huku wenyewe wakipiga 12 na moja ilimpata mbwa wake ambaye alimzika juzi katika maeneo ya nyumba anayoishi.

Hivi karibuni mbunge huyo aliwasilisha makao makuu ya Takukuru ushahidi wa CD aliodai kuwa unawahusisha madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha kushawishiwa kuhamia chama tawala.


Muungwana
WAO WALIPIGA RISASI 12 ...HIVI MTU UKIVAMIWA UNAWEZA KUKUMBUKA KUHESABU IDADI YA RISASI ZINAZOPIGWA?
 
Hao policcm wanapewa maelekezo nini wafanye!! Hatakaa apewe tena silah yake akiweza ahame nyumba kwa muda...maana hao wanatumwa na wengine wanakuwaga....ffu...ndio wanatumwa tumwa hovyo...
 
Tuanze na hili, yale maganda ya risasi yaliookotwa crime scene ni ya siraha gani?
Hizi drama za nchi hii zinaboaaa!!
Acha kuhemuka polisi wako kazini na wataleta taarifa haraka iwezekanavyo kama ambavyo wameshafanya kuhusiana na waliomshambulia TAML! Subira yavuta heri!
 
Back
Top Bottom