Bunduki ya Nassari yachunguzwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,161
2,000
Y2k4A4HE.jpg

Wakati mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari akilihusisha tukio la kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na masuala ya kisiasa, polisi inashikilia bunduki ya mwanasiasa huyo kwa uchunguzi.

Polisi mkoani Arusha imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kuwasaka washukiwa, huku ikichunguza silaha ya Nassari aina ya shotgun, ikisema tukio hilo lina utata kutokana na mazingira lilivyotokea.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo aliliambia gazeti hili kuwa wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la.

“Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,” alisema Mkumbo.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema msako unaendelea ili kuwabaini washukiwa na kwamba hawajapata maganda ya risasi zinazodaiwa kutumika katika uvamizi huo.

Juzi Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa nusu saa baada ya kuwasili nyumbani kwake alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyumba na baadaye kulisikika milio ya risasi. Alisema mbwa wake aliyekuwa akibweka alinyamaza, hali iliyomfanya achukue silaha yake kujihami.

“Nilipiga risasi tano, kisha kukawa kimya nikaenda kuwaamsha vijana wanaonisaidia hapa nyumbani kuwaeleza tukio lililotokea kisha nikaondoka.”

Alisema waliofanya tukio hilo hawakujua kama ana silaha kwa sababu mwaka 2014 wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, bastola yake ilichukuliwa na polisi na hadi leo haijarudishwa, hivyo kuwa na silaha nyingine kulimsaidia kujibu mapigo.

Katika tukio hilo, Nassari alisema aliwajibu watu hao kwa kupiga risasi tano hewani huku wenyewe wakipiga 12 na moja ilimpata mbwa wake ambaye alimzika juzi katika maeneo ya nyumba anayoishi.

Hivi karibuni mbunge huyo aliwasilisha makao makuu ya Takukuru ushahidi wa CD aliodai kuwa unawahusisha madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha kushawishiwa kuhamia chama tawala.


Muungwana
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,816
2,000
Yale yale ya lissu waathirika ndiyo wanachunguzwa, Mpaka leo wanamsubiri Lissu na dereva ndiyo waanze uchunguzi, hivi ni vichekesho
Hapa Nassari ana kesi ya kujibu.maganda ya risasi yote ya bunduki yake na za majambazi hata ganda moja halijapatikana eneo LA tukio.Kitu ambacho si cha kawaida.Maganda yangeonekana polisi wangeyapata
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,762
2,000
Hapa Nassari ana kesi ya kujibu.magwanda ya risasi yote ya bunduki yake na za majambazi hata ganda moja halijapatikana eneo LA tukio.Kitu ambacho si cha kawaida.Maganda yangeonekana polisi wangeyapata
Inawezekana hao watu wasiojulikana ni proffesionals kwa hiyo waliyaokota maganda na kuondoka nayo
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,816
2,000
Inawezeka hao watu wasiojulikana ni proffesionals kwa hiyo waliyaokota maganda na kuondoka nayo
Risasi kikawaida hununuliwa kwa kibali mfano ukiuziwa kumi ukizitumia unatoa maelezo ulizitumia wapi Hizo risasi anazosema Nassari alipiga hewani siku hiyo mmm zitizamwe vizuri isije kuwa aliitumia hiyo bunduki kupiga kwingine kumpiga MTU asiye julikana akaona anafuatiliwa akampiga mbwa risasi moja kumuua na kusingizia zingine alipiga hewani ili aseme zingine zilitumika hapo ambapo hakuna ushahidi wa risasi iliyorushwa angani wala ganda LA risasi .Polisi ichunguze bunduki na pistol za wote waliohudhuria mazishi ya mbwa akiwemo Godbless lema jeshi LA polisi liwawahi chap chap
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom