Heshima mbele wanajukwaa!
Nimepenyeshewa taarifa na mtu wa karibu kabisa ndani ya chama chetu tawala kua mwanzoni mwa mwezi October kuna viongozi waandamizi ndani ya CCM wanategemea kujiunga na UKAWA na kumuunga mkono mgombea ndani ya umoja huo!
Hata hivyo mnyetishaji wangu huyo ambaye hakutaka kuendelea kunipa ushirikiano zaidi wa ukweli wa taarifa zake zaidi ya kuniambia kua" we elewa hivyo kua kutakua na kitu kama hicho muda ukifika" awali aliniambia kua sasa ni dhahiri kua kuna watu ambao wako ndani ya CCM lakini nyoyo zao zote ziko ukawa kitu ambacho kimempelekea mgomea wao kulalamika kasalitiwa! amesema kuna hata wengine ambao no wagombea ndani ya CCM na wengine wamo ndani ya timu ya watu 32 iliyoundwa na mwenyekiti wao wa chama taifa, na wanatamani kutoka muda wowote huko lakini wanaogopa.
Kwahiyo mwanajukwaa ni hayo tu niliyoyachota mahali japo sijathibitishiwa ukweli wa hayo zaidi ya kuambiwa kua kuna kitu kama hicho, Mimi na wewe hatuna jibu kamili tusubiri muda ufike tusikie.