Alexander Mnyeti amepata wapi utajiri wa kuinunua TCC CLUB ya Chang'ombe?

Huyu mtu kwa sasa ni miongoni mwa matajiri wa kutupwa wa kitanzania lakini haijulikani mahali hasa anakopata pesa, anamiliki timu ya soka ya Gwambina na anaihudumia.

Taarifa zetu za uchunguzi zinaonyesha kwamba Mnyeti ameinunua TCC Club ya Chang'ombe Dar es Salaam kwa lengo la kuiendeleza na kutengeneza hostel yenye gym ndani yake kwa ajili ya Timu yake ya Gwambina, tunampongeza kwa uwekezaji huo, bali swali letu ni hili, AMEPATA WAPI LUNDO HILO LA HELA LA KUWEZESHA YOTE HAYA?
hayo ni mawazo ya kimaskini sana chadema sijui mnakosea wapi yaani unamjadiri mtu ambaye yuko madarakani ana acess ya kukopa ana marafiki wenye pesa unashangaa vitu kama hivyo? njaa itawauwa fanyeni kazi acheni kujadiri utajiri wa watu
 
Kuna wakati Riz1 alisingiziwa kila aina ya uzushi na kila dili tuliaminishwa ndio mhusika mkuu, kila jengo tuliambiwa ni mali ya Riz1 ,kila kituo cha mafuta,kila lori na kila aina ya uchafu tuliambiwa ni Riz1,yote hayo kwa sababu baba yake alikuwa raisi, na hata hawa wa sasa wanasingiziwa na kwa maneno mengi kisa tunaambiwa walikuwa karibu na mwendazake, sasa na nyie mlio karibu na mwenyekiti wa SACCOSS tuanze kuwachunguza na kuwasema kuwa matapeli,wakwepa kodi sio?
mwenyekiti wa saccoss anakula pekeyake wao kazi yao kuimba na kumsifia tuvushe mwenzao anakula chadema hawana jipya wameshindwa hata kuwa toa kina mdee bungeni walianza kwa mbwembwe nyiingi wametulia kama maji
 
Kwa hiyo viongozi wengine hawana access ya kukopa isipokuwa yeye tu ndiyo mjanja?
umemzungumzia huyo ndiyo maana nimekwambia kwa huyo kama unataka weka na mwingine naye nitakupa sababu yaani ukiwa na akili za kushabikia chadema na akili zinaisha kichwani sijui mnakwama wapi nyie
 
umemzungumzia huyo ndiyo maana nimekwambia kwa huyo kama unataka weka na mwingine naye nitakupa sababu yaani ukiwa na akili za kushabikia chadema na akili zinaisha kichwani sijui mnakwama wapi nyie
Siamini kama una akili timamu, umeambiwa onyesha biashara anazofanya toka akiwa mwalimu mkuu, DC, RC na sasa mbunge. upumbavu ni kuibiwa huku unamshagilia anayekuibia.
 
Imewahi kusemekana humu kwamba Bundi ametua kwa Mheshimiwa Alexander Mnyeti aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara wengi wameuhoji utajiri mkubwa alionao na ambao ameupata kwenye kipindi kifupi sana hawa hawamwamini mheshimiwa haki ya kuwa tajiri bali wanaamini kwamba utajiri huo ulitokana na matumizi mabaya ya madaraka.

Zipo taarifa kwamba Mh Mnyeti ameanza kuchunguzwa na Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora hatuna matatizo kuhusu uchunguzi huo ila chini kwa chini inasemekana malalamiko dhidi yake yalipelekwa kwenye tume toka enzi za hayati Rais Magufuli ila hayakufanyiwa kazi kwa sababu zinazoeleweka baada ya mabadiliko ya uongozi wa nchi inaelekea kama uchunguzi huo ni wa kweli tuisihi tume itende haki ifanye uchunguzi wake kwa kina,weledi na umakini.

Wahusika wengi katika kashfa itakayojitokeza ni watu wenye ukwasi mkubwa na hulka ya kutumia milungula wanapindisha utendaji wa wahudumu wa serikali awali mfano wa aliyekuwa wakili wa serikali huko Manyara “mkware “Kishenyi imewahi kutolewa humu kwenye jamvi rushwa ya shilingi milioni tano (5,000,000) ilimuumbua.

Yako maswali mengi ambayo Mheshimiwa Mnyeti anastahili kuyatolea majibu mfano

1:-Je uwanja wa Gwambina huko wilayani Misungwi ulijengwa kwa gharama ngapi?

2:-Mkandarasi alilipwa kiasi gani?

3:-Je kodi husika ililipwa inavyostahili?

4:-Je kuna visima vingapi uwanjani pamoja na sehemu nyingine ambayo alijenga huo uwanja huko Misungwi?mkandarasi wa visima alilipwa shilingi ngapi?(usije ukasema ati oh sasa wamechukua maji-hapana).

5:-Kuna uhusiano gani kati ya kamdarasi hizo na migogoro iliyokuwepo Manyara wakati huo?

Tunaisihi tume itende haki uongozi ni dhamana tatizo wapo viongozi aina ya Mnyeti,Sabaya na wengineo ambao walijivisha ngozi ya uzalendo na kuumiza watanzania wenzao kumbe walikuwa wanamtumia marehemu aliyeondoka kwa faida zao wenyewe viongozi wa namna hii na washirika wao hawafai.

Watipeleka nchi yetu kwenye umafia tunaousikia upo kwenye nchi nyingine sisi tunasubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi wa Tume kusema ukweli hili suala linaonekana ni la Takukuru zaidi ila tusubiri tuone tume itakuja na majibu gani.Tunaendelea kufuatilia

Wasalaam ni mimi “Nikune huku nikune kule “

7CB51142-768E-4D92-9081-D7219C153901.jpeg


885CE073-FF1B-4C68-AB0D-C1EAD475E523.jpeg


D5DD2A28-DA50-4EDF-811E-54849EFE041D.jpeg
 
Binafsi kila nikijaribu sikiliza hizo 'dhambi'za mnyeti naona Tu 'katajirika Sana kwa MDA mfupi'..

Kuna uporaji kafanya kwa wafanyabiashara?
Kuna watu aliwateka?
Alibaka?.
Alimzuia mtu kufanya biashara?

Nina Nina wasiwasi zaidi ya wivu na roho ya kwanini ...hakuna lolote lingine la maana..
 
Binafsi kila nikijaribu sikiliza hizo 'dhambi'za mnyeti naona Tu 'katajirika Sana kwa MDA mfupi'..

Kuna uporaji kafanya kwa wafanyabiashara?
Kuna watu aliwateka?
Alibaka?.
Alimzuia mtu kufanya biashara?

Nina Nina wasiwasi zaidi ya wivu na roho ya kwanini ...hakuna lolote lingine la maana..
Utakuwaje mkuu wa mkoa manyara tz ipo usiwe tajiri?

Swali?hao wanaolalamika jamaa kuwa kapiga hela wao wangekuwa wamevaa viatu vyake
Wangekubali kuishi kiboya au

Nchi kila mtu ni mwizi,sema hawajapata nafasi

Ova
 
Eehh.....nchi hii mwenye uwanja binafsi was mpira ni Bakhresa wa Azam, inafahamika ni tajiri, Mnyeti alipata wapi pesa? Nasikia timu imechoka kiuchumi,hawalipwi
 
Eehh.....nchi hii mwenye uwanja binafsi was mpira ni Bakhresa wa Azam, inafahamika ni tajiri, Mnyeti alipata wapi pesa? Nasikia timu imechoka kiuchumi,hawalipwi
Nchi hii kiongozi wa serikalini ni zaidi ya mfanyabiashara....
Hana kiwanda, hana biashara inayomuingizia pesa lakini cha ajabu akaunt yake ina hela za kutosha,na ma asset kibao tofauti na kipato chake....

Ova
 
Eehh.....nchi hii mwenye uwanja binafsi was mpira ni Bakhresa wa Azam, inafahamika ni tajiri, Mnyeti alipata wapi pesa? Nasikia timu imechoka kiuchumi,hawalipwi
Watz wengi nibwachuuzi,watz wengi wakipata pesa ni kyzichungulia kwenye acc na kujenga majumba ya kupangisha.
Lakini ukiwekeza kwenye vitu au fursa adimu wewe ni kimeo.
Naomba wenye vyombo tuache kyfuatilia hizi maana ni ushindi kwa CHADEMA kuona mtu wao mbaya anaadhibiwa.
Baada ya Sabaya iwe tu ni funzo kwa wengine kuwa tuwahudumie wananchi .

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi kila nikijaribu sikiliza hizo 'dhambi'za mnyeti naona Tu 'katajirika Sana kwa MDA mfupi'..

Kuna uporaji kafanya kwa wafanyabiashara?
Kuna watu aliwateka?
Alibaka?.
Alimzuia mtu kufanya biashara?

Nina Nina wasiwasi zaidi ya wivu na roho ya kwanini ...hakuna lolote lingine la maana..
Watu wanaunganisha matukio.

Mnyeti na Sabaya ndio watu wa kwanza kujihusisha na biashara ya madiwani na wabunge.

Vile vile Mnyeti alikuwa Manyara, kwenye Tanzanite. Huko vijana wa wa Magu walikuwa wanajibebea tu.
 
Back
Top Bottom