barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,324
- 29,586
Kuna mahali inakatazwa kitajirika ndani ya mida mfupi?
Imewahi kusemekana humu kwamba Bundi ametua kwa Mheshimiwa Alexander Mnyeti aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara wengi wameuhoji utajiri mkubwa alionao na ambao ameupata kwenye kipindi kifupi sana hawa hawamwamini mheshimiwa haki ya kuwa tajiri bali wanaamini kwamba utajiri huo ulitokana na matumizi mabaya ya madaraka.
Zipo taarifa kwamba Mh Mnyeti ameanza kuchunguzwa na Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora hatuna matatizo kuhusu uchunguzi huo ila chini kwa chini inasemekana malalamiko dhidi yake yalipelekwa kwenye tume toka enzi za hayati Rais Magufuli ila hayakufanyiwa kazi kwa sababu zinazoeleweka baada ya mabadiliko ya uongozi wa nchi inaelekea kama uchunguzi huo ni wa kweli tuisihi tume itende haki ifanye uchunguzi wake kwa kina,weledi na umakini.
Wahusika wengi katika kashfa itakayojitokeza ni watu wenye ukwasi mkubwa na hulka ya kutumia milungula wanapindisha utendaji wa wahudumu wa serikali awali mfano wa aliyekuwa wakili wa serikali huko Manyara “mkware “Kishenyi imewahi kutolewa humu kwenye jamvi rushwa ya shilingi milioni tano (5,000,000) ilimuumbua.
Yako maswali mengi ambayo Mheshimiwa Mnyeti anastahili kuyatolea majibu mfano
1:-Je uwanja wa Gwambina huko wilayani Misungwi ulijengwa kwa gharama ngapi?
2:-Mkandarasi alilipwa kiasi gani?
3:-Je kodi husika ililipwa inavyostahili?
4:-Je kuna visima vingapi uwanjani pamoja na sehemu nyingine ambayo alijenga huo uwanja huko Misungwi?mkandarasi wa visima alilipwa shilingi ngapi?(usije ukasema ati oh sasa wamechukua maji-hapana).
5:-Kuna uhusiano gani kati ya kamdarasi hizo na migogoro iliyokuwepo Manyara wakati huo?
Tunaisihi tume itende haki uongozi ni dhamana tatizo wapo viongozi aina ya Mnyeti,Sabaya na wengineo ambao walijivisha ngozi ya uzalendo na kuumiza watanzania wenzao kumbe walikuwa wanamtumia marehemu aliyeondoka kwa faida zao wenyewe viongozi wa namna hii na washirika wao hawafai.
Watipeleka nchi yetu kwenye umafia tunaousikia upo kwenye nchi nyingine sisi tunasubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi wa Tume kusema ukweli hili suala linaonekana ni la Takukuru zaidi ila tusubiri tuone tume itakuja na majibu gani.Tunaendelea kufuatilia
Mwisho.
Wasalaam ni mimi “Nikune huku nikune kule “
View attachment 1826026
View attachment 1826027
View attachment 1826028