Bunda: Madiwani wa CCM wagomea Madawati yaliyotolewa na Mbunge wa CHADEMA Mh. Bulaya

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba madiwan wa ccm Jimbo La BUNDA MJINI wamekataa kuchukua madawati yaliyotolewa na mh Ester Bulaya kisa Yameandikwa jina la Mbunge huyo habari na Lucas Mhavile TN Bunda mjini
1470500276033.jpg
 
Madiwani wa CCM Jimbo La BUNDA MJINI wamekataa kuchukua madawati yaliyotolewa na Mh Ester Bulaya kisa Yameandikwa jina la Mbunge huyo habari na Lucas Mhavile TN Bunda mjini

My Take;
Ikiandikwa kwa Msaada wa Marekani, China, Japan au kwa Msaada wa Manji Clinton Trump n.k, ndo inaonekana ya maana na tunashangilia sana. Watanzania tuna Safari ndefu kuifikia Tanzania ya Viwanda kama hali ndo hii huko Mikoani.
IMG-20160806-WA0033.jpg
IMG-20160806-WA0032.jpg
 
Peoplessss. Na wakome mafisiem. Yan madawati yao yakijinga kweli. Kuna wilaya moja wametoa madawati mwez umeisha yasha nyauka na kuachia
 
Natumani hilo siyo kweli. Kwani wao wanahusikaje na madawati ambayo ni ya wanafunzi? Shame on them. Wao wamechangia mangapi mpaka wakatae madawati ya watoto. Akili yao sawa na polisi waliosema mikutano haina shida ila uniform za chadema ndiyo shida!!! Kuogopa umande ndiyo shida kubwa Tz.
 
Safi sana madiwani,
Kama umeamua kuchangia we changia tu,sasa kuandika majina ili iweje?

Cheap popularity itawaua Chadema.

Kwani ccm katika ILANI yenu mliweka elimu kipaumbele?? Waambieni CDM wachukue madawati yao mkuu
 
Naomba niyafate nipeleke Jimboni mwangu-tena kijijini kwetu.

Au aya Donate ktk NGO yoyote inayomiliki Primary School. Kweli CCM ni adui wa Elimu.
 
Hivi nguo za mitumba tunazovaa,mengine yakiwa na Ujumbe wa ajabu hatulalamiki,kwa nini tukatae madawati kisa jina la mbunge?
 
Kinakuuma nini wew. Kwani yeye si ndo mbunge wa jimbo hilo!? Na wao watengeneze yakwao waandike majina yao. Waache uchama kikubwa maendeleo yapo
Ila ukweli JF ni kama jamvi la wageni kwa sasa
Ninyi si ndio mlifurahia kitendo kama hichohicho kilichofanywa na madiwani wa Chadema huko Tukuyu Rungwe kukataa madawati yalotengenezwa na Mbunge wa jimbo hilo CCM??
TUNAPOWAITA WENYE NDIMI MBILI MUWE MNAKUBALI ...Maana mnalokataa Leo kesho ni sukari kwenu na sukari ya leo kwenu kesho ni Sumu
What a tragedy for Upinzani Tanzania!!!!! Like father like son (Mbowe na wanawe...gia angani)
 
Back
Top Bottom