Bunda: Madiwani wa CCM wagomea Madawati yaliyotolewa na Mbunge wa CHADEMA Mh. Bulaya

Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo upo kwa mujibu wa sheria. Fedha zake HATOI mbunge. Inatoa Serikali.

Ktk Jimbo pana Kamati mahsusi ya mipango kwajili ya matumizi ya fedha za Mfuko huo lkn pia pana signatories kwa ajili ya fedha hizo ziwapo benki, kwa mujibu wa sheria. SIYO kwa matakwa wala mipango ya Mbunge awe CCM au Chama Kingine.

Laiti Dada Bulaya angetoa fedha zake mfukoni kutengeneza dawati hizo basi ilikuwa vema, haki na halali kujiandika yeye jina lake. Lkn fedha zilizotumika zinatolewa na Serikali.

Nikama vile mawaziri wawe Wanaandika majina yao kwenye vibao vya miradi ya Serikali iliyotekelezwa chini ya usimamizi wao! Wenyeviti wa Halmashauri hali kadhalika!

Nadhani Bulaya akitekeleza mradi fulani kwa fedha zake Mfukoni andike jinale.

Nadhani umenielewa.
Wewe ni kipofu angalia miradi yote inayozinduliwa kuna majina ya walio zindua!!
Je walitoa fedha zao au walichangia
nini??
Mbunge Esther Bulaya katoa madawati kwa mfuko wa jimbo, angeamua kufadhiri Hospt ingekuwa sawa tuu!!
Madiwani acha ushabiki wa kijinga hata watoto wanao kaa chini watawashangaa??
 
Ila ukweli JF ni kama jamvi la wageni kwa sasa
Ninyi si ndio mlifurahia kitendo kama hichohicho kilichofanywa na madiwani wa Chadema huko Tukuyu Rungwe kukataa madawati yalotengenezwa na Mbunge wa jimbo hilo CCM??
TUNAPOWAITA WENYE NDIMI MBILI MUWE MNAKUBALI ...Maana mnalokataa Leo kesho ni sukari kwenu na sukari ya leo kwenu kesho ni Sumu
What a tragedy for Upinzani Tanzania!!!!! Like father like son (Mbowe na wanawe...gia angani)
Jf imepoteza uhalisia wake, kimegeuka kuwa chombo cha propaganda cha upinzani. Yetu macho!!
 
Ni mfuko wa jimbo pesa toka serikalini! Hajachangia yeye binafsi na pesa yake ya mfukoni kwanini aandike jina lake
 
Safi sana madiwani,
Kama umeamua kuchangia we changia tu,sasa kuandika majina ili iweje?

Cheap popularity itawaua Chadema.
Aisee naomba nisikupinge ila kuna mipira inagawiwa ina nembo ya chama chenu. Mbona hwajaikataa?
 
Safi sana madiwani,
Kama umeamua kuchangia we changia tu,sasa kuandika majina ili iweje?

Cheap popularity itawaua Chadema.

Watoto wakaklie madawati, ficheni ujinga wa akili mlio nao. Yangeandikwa kwa hisani ya watu wa marekani ni sawa, lakini sio jina la mbunge wao. Huu ujinga utaisha lini? Kwani yanaacha kuwa madawati kwa kuandikwa jina la mbunge

Ujinga wa madiwani hawa ni wa kiwango cha PhD
 
Kwani jina lina athiri nini!?
Mbona kwenye miradi mbalimbali inayozinduliwa kwenye mbio za mwenge huandikwa majina yao (m/kiti wa mbio za mwenge) na hatuikatai miradi hiyo!!!!! ?????????
Kwa nini rais wa nchi huweka mwe ya misingi kama utambulisho wa miradi wananchi wa vyama vyote tunaipokea!!!!!! ???????
Tubadilike maendeleo hayana itikadi.
Kaka andika vizuri. Unakimbilia wapi? Acha hasira. Huu mchezo hauhitaji hasira!
 
bulaya anataka cheap popurality mbona akina diamond walipochangia madawati hawakuandika majina yao.......... hata mengi alipochangia madawati mbona hakuandika jina lake? NINAWAPONGEZA SANA HAO MADIWANI KWA KUKATAA HAYO MADAWATI kwani hayo madawati ilibidi yaandikwe mfuko wa jimbo sasa yeye bulaya anaandika majina yake ili iweje?? safi comrades
kwahiyo ni bora watoto wakae chini?....nataka unipe faida za watoto kukaa chini na hasara ya jina kuwepo kwa hao watoto
 
Mimi nadhani huu upinzani ni humu jf uliojaa matusi n Majungu,Mleta maada ana maana kubwa sana hivi karibuni mwezi jana nilimuona Mheshimiwa mmoja jimbo la mbeya kwa tiketi ya CCM alipochangia madawati na kukataliwa na madiwani kisa fedha ni za serikali na mbunge alikuwa ameandik JINA LAKE,Nadhani hali kdhalika we might be fair kama fedha ni serikali asiandike jina lake,kama fedha katoa mwenyewe yuko halali kuandika.Mungu awasaidie munguze matusi na mihemko kwenye JF,maana ningekuwa na uwezo ningefuta IDs za wale wanaotoa matusi humu JF.
two wrongs don't make a right...Huu ndio ulikuwa wakati muafaka wa CCM kuwaaibisha wenzao wa CHADEMA.Sio nao kuendekeza utoto wa kususasusa.
 
Madawati mengine yaliandikwa majina ya BAR yalipokelewa, iweje ya mbunge yakataliwe?
 
Back
Top Bottom