real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Serikali ya mji wa Pazardzhik imesema itaweka taratibu za kuwatoza faini wote watakokiuka marufuku hiyo,
Serikali ya mji wa Pazardzhik imepiga marufuku uvaaji wa vazi la hijab linalofunika uso mzima hadharani, hatua ambayo serikali imesema itaondoa wasiwasi na kuboresha usalama
Marufuku hiyo imetolewa Jumatano, ni ya kwanza kwenye nchi za Balkani, umeungwa mkono na wanasiasa kwenye mji huo wa watu 70,000, ambao kuvaa hijabu imekuwa ni jambo la kawaida kwa jamii ndogo ya waisilamu wa kirumi
"Nimechoka kusikia kwamba Pazardzhik ni mji wa kuvaa hijabu,. Tunataka kusema kwa sauti kubwa kuwa sisi hatuko hivyo, bali mji wa watu wawajibikajina tunaojishughuisha na mafanikio mengine'' Meya wa mji huo Todor Popov aliiambia radio ya taifa.
Waisilamu ni asilimia 12 ya wananchi milioni 7.2 wa Bulgaria, na wengi wao wana asili ya jamii ya Kituruki iliyokaa karne kadhaa nchini Bulgariaon.
Popov alisema faini zitatozwa kwa yoyote atakayekiuka marufuku hiyo, ambayo polisi wamesema inahitajika kwa kuwa hijabu zinazofunika uso mzima kasoro macho zinakwamisha utambuzi wa haraka
Wananchi wa Bulgaria wana wasiwasi kuwa ujio wa wakimbizi barani ulaya kunaweza kuleta hatari kwa utamaduni wao wa Kikristu na pia kuwageuza waisilamu wachache waliokuwepo kwa muda mrefu kuwa waisilamu wa msimamo mkali
Chanzo:Al Jazeera