Akiongea kwenye kampeni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM amesema chama hicho hakitawaruhusu wapinzani kwenda IKULU.
NB;Hivi CCM ndo inaruhusu watu kwenda IKULU kauli hii inaashiria kuwa hata kama upinzani utashinda hawatakubali washike madaraka.
Ninaomba wanasiasa wachunge ndimi zao wakati huu wa uchaguzi kwani hata CCM wakishinda wapinzani wataamini kuwa wameibiwa hali itayoleta machafuko na kupelekea mauaji acheni vitisho vyenu maana wanaoamua nani aende ikulu ni wananchi na sio CCM.
NB;Hivi CCM ndo inaruhusu watu kwenda IKULU kauli hii inaashiria kuwa hata kama upinzani utashinda hawatakubali washike madaraka.
Ninaomba wanasiasa wachunge ndimi zao wakati huu wa uchaguzi kwani hata CCM wakishinda wapinzani wataamini kuwa wameibiwa hali itayoleta machafuko na kupelekea mauaji acheni vitisho vyenu maana wanaoamua nani aende ikulu ni wananchi na sio CCM.
SALAM KWENU NEC KUHATARISHA AMANI YA NCHI.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia Sheria ya Uchaguzi, tunaomba kuwa makini sana dhidi ya mienendo ya Chama Cha Mapinduzi ambayo tunaona inaenda kuhatarisha amani ya Nchi. NEC mmekuwa mkifumbia macho mambo mengi maovu yanayofanywa na Ccm, sitaki kuamini sana kuwa mnatumiwa ama mnaogopa kuwakemea kwa kuwa ni Chama dola ama nini kipo nyuma ya pazia.
Kauli kama ya Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Ccm si tu inatia kichefu chefu bali inahatarusha amani ya nchi.
Bulembo: "kuna jambo moja ambalo CCM bado haijafanya na haitafanya ni kuruhusu Wapinzani kwenda Ikulu! Mengine yote tutafanya lakini Ikulu hapana".
Tunataka kuona Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikichukua hatua dhidi ya mambo yafananayo na hayo maana amani ya nchi itakapopotea si Ccm wala Wapinzani watabaki salama.
Naomba nijikite zaidi kuongelea hili la msingi.
Kupiga kura ni haki ya msingi ya kila Mtanzania kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara ya
5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
Juzi tarehe 22/09/2015 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa
Mlongo aliitisha kikao na waendesha boda boda
wa Mwanza uliofanyika katika Ukumbi wa Gold Crest Jengo la PPF, kikao kilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.
Lengo la Kikao hicho lilikuwa kuwarubuni waendesha
boda boda kwa kuwaahidi kuwapatia huduma ya Bima ya Afya pamoja na
kuwasaidia kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Kila boda boda alipewa Tshs 10,000/_ na ahadi ya chakula.
Walijitokeza Vijana wengi wapatao 1000.
Moja ya Masharti ya kupatiwa huduma ya Bima ya Afya na Kuingia katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kuhakikisha ya kwamba wanakabidhi Shahada zao za kupigia Kura. Wapo waliokabidhi na wapo waligoma.
Jana tarehe 23/09/2015 Yale yale ya Mwanza yametokea Mkoa wa shinyanga.
Na tarehe 28/09/2015 Katibu wa Ccm Mh. Abdulhaman Kinana atakuwa Mkoani Mbeya akiongozana na January Makamba katika zoezi la kutumia mbinu za Ulaghai za kuwadanganya waendesha bodaboda kuwatafutia Kadi za Bima ya Afya na Kuwaunganisha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Kumbuka haya ni maagizo yaliyotolewa na Rais wa Nchi Mh. Jakaya Kikwete kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika kikao chao ya Ngurdoto Arusha kuhakikisha Ccm inashinda na kuzuia Wananchi wakiwemo boda boda wanaomuunga Mkono Lowassa kutokupiga kura katika Uchaguzi uliopangwa kufanyika Octoba 25,2015.
JK akiwa amekaa meza moja na Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa huko Ngurdoto Arusha alisema, Lazima Ccm ishinde na kila mmoja wenu atimize wajibu wake, na atakayeshindwa ajue kuwa nafasi itapotea.
Haya ni maagizo ya Nchi nzima.
Ccm wameshaonesha dalili mbaya ya kushindwa Uchaguzi na wanachofanya ni kutumia mbinu halamu lakini cha ajabu Chombo chenye Mamlaka (NEC) kinayaona haya na kuyafumbia macho.
Tunawaomba Wananchi kutodanganyika na ahadi za Ccm zinazotolewa za eti tutakutengenezea Kadi ya Bima ya Afya mara tutakusajiri katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa masharti ya kuwapa kadi yakuoigia kura, huu ni utapeli na nitoe Rai kwa wananchi kuwashughulikia watu kama hawa na ikibidi kuwapiga kabisa. Tunza Shahada yako na uitumie kuiondoa Ccm madarakani Octoba 25.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi tunataka kusikia mkiyasemea haya tena kwa uwazi la sivyo Watanzania hawako tayari kuona amani ya nchi ikivurugwa na watu wachache kwa kutaka kulinda masilahi ya familia zao.
#MabadilikoNiLazima2015
#CcmOUT2105