Bulembo amtaka Lowassa aache kung’ang’ania siasa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,318
50,532
lowa.png

MWENYEKITI wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemshangaa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa kuendelea kung’ang’ania siasa hadi sasa hivi, badala yake anastahili kukaa kimya kula maisha ili afaidi uzee wake vizuri.

Bulembo aliyasema hayo wakati akifunga kampeni za udiwani Kata ya Mateves iliyopo Wilaya ya Arusha juzi, ambako walitarajiwa kumchagua diwani wao katika uchaguzi mdogo. Mbunge huyo mteule wa kuteuliwa, alisema anashangaa Lowassa kung’ang’ania madaraka, badala yake anastahili kula maisha ili kufaidi uzee wake vizuri.

Alisema wapinzani wataruhusiwa kutumia barabara, maji, shule na vinginevyo, lakini kwenda Ikulu haiwezekani. Aidha, Bulembo alilaani kitendo cha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingilia msafara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliokuwa ukielekea Uwanja wa Ngorbob Sokoni kwa ajili ya kufunga kampeni za chama hicho.

Alisema wafuasi wa CCM ni wastaarabu na wavumilivu, hawakufanya fujo, bali waliwapita kwa mbele na kuelekea kwenye mkutano wa kufunga kampeni.

Mgombea Udiwani wa Kata ya Mateves, Julius Saing’ore maarufu kwa jina la Sovoyo na mgombea uenyekiti wa serikali ya kijiji, Mohamed Nassoro maarufu kwa jina la Arsenal, waliomba kura kwa wananchi hao ili walete maendeleo.

Mgombea udiwani Saing’ore aliwasihi wananchi wa kata hiyo, kumpa kura ili waliokwenda mahakamani kudai uchaguzi uliokuwa na kasoro wajue kuwa CCM ndio yenyewe.

Awali, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shabani Mdoe alisema wananchi wana imani kubwa na chama hicho na hawataki porojo, bali wanataka maendeleo.

Alisisitiza kuwa awali alipokuwa madarakani aliyekuwa diwani wa CCM kabla ya kutenguliwa na mahakama mwaka jana, Saing’ore maarufu kwa jina la Sovoyo, alifanya kazi mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Alisema diwani huyo ambaye sasa anagombea tena, alikaa madarakani kwa siku 63 kama Diwani wa Kata ya Mateves kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijiji (Arusha DC) hivyo kurudi kwake kama diwani kutawezesha wananchi kupata maendeleo.

Chanzo: Habari Leo
 
Bulembo :"wapinzani wataruhusiwa kutumia barabara, maji Lakini sio kwenda ikulu "
BILA KATIBA MPYA, TUME HURU, BILA UPINZANI KUWA NA DEMOKRASIA YA KWELI NDANI YA VYAMA VYAO BASI HIO KAULI NI KAMA INA UKWELI
MY TAKE CHADEMA CHINI YA MBOWE Imehadaa watanzania. Unaweza kudhani ni kitu kidogo walikosea walivyobadili Gia Lakini ukweli ni kwamba watanzania baadhi wenye akili nzuri wamewadharau Sana... Imefika Muda tuwaambie ukweli.. Lowasa Hana nguvu za kuwa mgombea rais wala mbowe.. Inahitaji mtu msafi mwenye uwezo wa kujenga hoja... Kiukweli rais magufuli Pamoja na mapungufu Yake mengi Ila Sura na mwili wake tu umependezea na umefit kuwa mkuu WA nchi... Haya ni maoni yangu tu binafsi... Mojawapo ya vitu vya kuiga toka CCM ni PAMOJA NA upatikanaji wa mgombea maccm wako na demokrasia Sana nadhani Africa yote CCM ipo kwenye list ya VYAMA venye Mchakato huru na wazi
 
View attachment 462884

CCM wasipomtaja Lowassa hawati raha
 
UPINZANI SIO UADUI MSIFIKIRI NYIE CCM MNA HATI MILIKI YA NCHI HII. JIFUNZENI KWA VYAMA TAWALA VILIVYOANGUSHWA KUANZIA KILE CHA ZAMBIA CHA KENNETH KAUNDA HADI KANU YA KENYA. VILIKUWA NA KIBURI VIKAJISAHAU HATIMAYE MHESHIMIWA BULEMBO HEBU MALIZIA VILIFIKWA NA NINI?....... NA SASA VIKO WAPI?......
 
Bulembo :"wapinzani wataruhusiwa kutumia barabara, maji Lakini sio kwenda ikulu "
BILA KATIBA MPYA, TUME HURU, BILA UPINZANI KUWA NA DEMOKRASIA YA KWELI NDANI YA VYAMA VYAO BASI HIO KAULI NI KAMA INA UKWELI
MY TAKE CHADEMA CHINI YA MBOWE Imehadaa watanzania. Unaweza kudhani ni kitu kidogo walikosea walivyobadili Gia Lakini ukweli ni kwamba watanzania baadhi wenye akili nzuri wamewadharau Sana... Imefika Muda tuwaambie ukweli.. Lowasa Hana nguvu za kuwa mgombea rais wala mbowe.. Inahitaji mtu msafi mwenye uwezo wa kujenga hoja... Kiukweli rais magufuli Pamoja na mapungufu Yake mengi Ila Sura na mwili wake tu umependezea na umefit kuwa mkuu WA nchi... Haya ni maoni yangu tu binafsi... Mojawapo ya vitu vya kuiga toka CCM ni PAMOJA NA upatikanaji wa mgombea maccm wako na demokrasia Sana nadhani Africa yote CCM ipo kwenye list ya VYAMA venye Mchakato huru na wazi
Juzi rais wa marekan kwenye. Hotba yake amesema. Kikundi cha watu wachache wanafaidika katka nchi ni kweli kabisa na hawa wazee na vijana wachache ndio wanaofaidika ukitaka kuamini hayo tazama uvccm watoto wa watawala ndio wamejaa
 
ukitaka mzee wa magogoni akupende komaa na upinzani hapo bulembo uwazir unamsogelea
 
Yeye anatafuta nini mbona hajastaafu? Akapimwe akiri haiwezekani kila wakiamka hawana jipya ni Lowassa kwanini?
 
Back
Top Bottom