Bulembo aendelea kuvuruga amani Makambako

Bulembo aendelea kuvuruga amani Makambako

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,400
Jeshi la police limeishambulia kwa mabomu ya machozi office za CHADEMA Makambako Iringa na kutawanya wananchi walioondoka kwenye mkutano wa CCM na Magufuli Jana

Wananchi hao walidaiwa kumzomea bulembo kwenye mkutano huo wa magufuli kwenye mji mdogo wa makambako

Ofisa wa kampeni wa CHADEMA Aldo Mlote aliwatuhumu police kwa kutumika vibaya kukibeba CCM kila kinaposhindwa hoja majukwaani. Mloto alisema police walirusha mabomu kwenye office za chadema na kuwakamata watu kumi na tano

Alisema mabomu hayo yalirushwa baada ya Bulembo kuuliza kama kwenye mkutano huo kuna wafuasi wa CHADEMA ambapo wengi waliokuepo kwenye mkutano huo walinyoosha vidole viwili juu kumaanisha kuwa wapo

Ndipo Bulembo alipoanza kumkashifu Edward Lowassa kuwa ni mgonjwa jambo lililosababidha azomewe mpaka kushindwa kuendelea kuongea.

Kabla ya mkutano huo kulikua na madai kuwa kadi za CHADEMA ziligawiwa watu na kupewa 30,000 kila mmoja ili wazirudishe kwenye mkutano huo kumfurahisha Magufuli mbinu iliobainika na watu mapema.

Ndipo baadhi ya watu walienda kutoa taarifa katika office za CHADEMA Hivyo katika mchezo huo walibaki watu watano waliorudisha kadi hizo

Pamoja na Magufuli kuomba wamchague mkutano huo ulifungwa huku watu waliokua kwenye mkutano huo wakiondoka kuzifuata office za CHADEMA kwa shamrashamra na nyimbo kitu kilichofanya police kuwatawanya kwa mabomu.

My take
Watu wameichoka CCM kila mkutano wa CCM na Magufuli si wote ni wana CCM kwa sasa watu wanataka mabadiliko ya UKAWA na Lowassa.
 
Wananchi hao walidaiwa kumzomea bulembo kwenye mkutano huo wa magufuli kwenye mji mdogo wa makambako

Tatizo la CHADEMA wanachama wao wanakunywa viroba.Hawafuatilii hata Tume ya uchaguzi inachoagiza.Na viongozi nao wa CHADEMA ni kunywa viroba tu hawawaelimishi wanachama wao sheria za mikutano.

Hairuhusiwi mtu wa chama kingine kwenda mkutano wa mtu wa chama kingine kwenda kuzomea au kumfanyia fujo .Unaruhusiwa kwenda kusikiliza si kuzomea au kufanya fujo.

Wakipigwa na virungu na mabomu kwa kuingilia mikutano ya watu kwa kuzomea au kufanya fujo wanaanza kupiga yowe ohh!! POLISI WANATUONEA.Hilo haliongezi kura linawapunguzia.Kwani watu wanawaona CHADEMA ni watu wasiojali sheria.Ukiwapa nchi watakuwa hawazingatii utawala wa sheria.Kama hili tu la kuzingatia sheria za mikutano hawawezi wakipewa nchi wataweza?

Mkutano kama haukuhusu una uhuru wa kwenda au kutokwenda.Usiende kufanya fujo mikutano ya watu wengine.CHADEMA PUNGUZENI UNYWAJI VIROBA.
 
Wameisoma namba si CCM wala police Watanzania wameamua.Magufuli hajajua kuwa Bulembo anamharibia kila kitu.Magufuli tumemwambia vihiyo kama Bulembo awafukuze hataki amevaa tintedi shauri yake atajilaumu
 
magufuli alikwishwa ambiwa bulembo anamwaribiaa hataki kusikilizaa!!
 
Huyu Bulembo hivi sera yake ni ugonjwa wa Lowasa tu hana cha kuambia wananchi CCM imefanya ndani ya miaka 54 na inatarajia kufanya nini?!
 
Wamechanganyikiwa hawajielewi wanafanya nini. Hawana sera wameishiwa

Kama ndiyo Mgombea Raisi mwenyewe ndiyo huyo ni heri Mwanamziki Sugu angegombea Uraisi.

Kamati nzima ya Kampeni ya Watu 30 wameshindwa kumsahauri yapi ya kufanya jukwaani?
Hii ni aibu tupu!. Huyu bwana ndiyo maana anafahamu Idadi ya Mabarabara kwa sababu Elimu ya Kemia imemharibia kiasi fulani ya Akili.Shida ya Tanzania yetu kutokuwa na maabara za kueleweka kufanya kwa Vitendo huwaacha walimu na Wanafunzi kukariri tu na matokeo yake ndiyo hayo.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la CHADEMA wanachama wao wanakunywa viroba.Hawafuatilii hata Tume ya uchaguzi inachoagiza.Na viongozi nao wa CHADEMA ni kunywa viroba tu hawawaelimishi wanachama wao sheria za mikutano.

Hairuhusiwi mtu wa chama kingine kwenda mkutano wa mtu wa chama kingine kwenda kuzomea au kumfanyia fujo .Unaruhusiwa kwenda kusikiliza si kuzomea au kufanya fujo.

Wakipigwa na virungu na mabomu kwa kuingilia mikutano ya watu kwa kuzomea au kufanya fujoi wanaanza kupiga yowe ohh!! POLISI WANATUONEA.Hilo haliongezi kura linawapunguzia.Kwani watu wanawaona CHADEMA ni watu wasiojali sheria.Ukiwapa nchi watakuwa hawazingatii utawala wa sheria.Kama hili tu la kuzingatia sheria za mikutano hawawezi wakipewa nchi wataweza?

Mkutano kama haukuhusu una uhuru wa kwenda au kutokwenda.Usiende kufanya fujo mikutano ya watu wengine.CHADEMA PUNGUZENI UNYWAJI VIROBA.

Ni kama wewe viroba unavyotumia unachanganya na viagra; sio bure! mleta uzi kasema : darasa la saba Bulembo kauliza; hapa kuna watu wa CDM? akajibiwa Ndio! akaanza kumkashifu EL; wakamzomea; sasa nani wa kulaumiwa, kumbe darasa la 7 Bulembo aliuliza uwepo wa wanaCDM ili amkashifu mgombea wao; wa nini asizomewe?!
You commit; you get paid in kind; Period!
 
Tatizo la CHADEMA wanachama wao wanakunywa viroba.Hawafuatilii hata Tume ya uchaguzi inachoagiza.Na viongozi nao wa CHADEMA ni kunywa viroba tu hawawaelimishi wanachama wao sheria za mikutano.

Hairuhusiwi mtu wa chama kingine kwenda mkutano wa mtu wa chama kingine kwenda kuzomea au kumfanyia fujo .Unaruhusiwa kwenda kusikiliza si kuzomea au kufanya fujo.

Wakipigwa na virungu na mabomu kwa kuingilia mikutano ya watu kwa kuzomea au kufanya fujoi wanaanza kupiga yowe ohh!! POLISI WANATUONEA.Hilo haliongezi kura linawapunguzia.Kwani watu wanawaona CHADEMA ni watu wasiojali sheria.Ukiwapa nchi watakuwa hawazingatii utawala wa sheria.Kama hili tu la kuzingatia sheria za mikutano hawawezi wakipewa nchi wataweza?

Mkutano kama haukuhusu una uhuru wa kwenda au kutokwenda.Usiende kufanya fujo mikutano ya watu wengine.CHADEMA PUNGUZENI UNYWAJI VIROBA.

Mkuu bulembo ndio shida kwa nini aliuliza kama wapo?
 
makambako haipo iringa we we IPO mkoa wa Njombe hebu tengua kauli hiyo
 
Kuna vituko vingi vinaendelea jamani..eti watu wa chadema wakanyoosha vidole viwili. Chadema ina mvuto sana
 
Tatizo la CHADEMA wanachama wao wanakunywa viroba.Hawafuatilii hata Tume ya uchaguzi inachoagiza.Na viongozi nao wa CHADEMA ni kunywa viroba tu hawawaelimishi wanachama wao sheria za mikutano.

Hairuhusiwi mtu wa chama kingine kwenda mkutano wa mtu wa chama kingine kwenda kuzomea au kumfanyia fujo .Unaruhusiwa kwenda kusikiliza si kuzomea au kufanya fujo.

Wakipigwa na virungu na mabomu kwa kuingilia mikutano ya watu kwa kuzomea au kufanya fujoi wanaanza kupiga yowe ohh!! POLISI WANATUONEA.Hilo haliongezi kura linawapunguzia.Kwani watu wanawaona CHADEMA ni watu wasiojali sheria.Ukiwapa nchi watakuwa hawazingatii utawala wa sheria.Kama hili tu la kuzingatia sheria za mikutano hawawezi wakipewa nchi wataweza?

Mkutano kama haukuhusu una uhuru wa kwenda au kutokwenda.Usiende kufanya fujo mikutano ya watu wengine.CHADEMA PUNGUZENI UNYWAJI VIROBA.
Ila mwenyewe ndio aliuliza watu wa chadema mpooo?? Na jibu akapewa
 
Mkuu bulembo ndio shida kwa nini aliuliza kama wapo?

Hili mbona ni swali la kawaida tu kwenye mkutano ya kisiasa? Mtoa hotuba aweza uliza wanawake mpo???? Wanajibu tupo.Anauliza wanaume mpoooo???? Wanajibu tupo.Anauliza vijana mpoooo??? Wanajibu tupoOOO?? Sasa nongwa ganbi kuuliza CHADEMA mpoooo?? ILitakiwa wajibu tupoooo bila kumzomea wala kufanya vurugu yeyote.SABABU MIKUTANO yote wanakuwepo wanachama wa vyama tofauti tofauti na wasio na vyama ambao huja pale kusikiliza ili tarehe 25 october waamue wampigie nani.CHADEMA siasa za vyama vingi inaonyesha wako nyuma sana.Hawajui ustaarabu wa mikutano.Hata CCM kibao mbona wanaenda mikutano ya CHADEMA? ILA HUWA WANAENDA KUSIKILIZA SI KUZOMEA AU KUFANYA FUJO.

CHADEMA makambako mnachotaka kusema ni kuwa ruksa kwa wanachama wa vyama vingine kuja mikutano yenu kuzomea na kufanya vurugu? Jifunmzeni ustaarabu wa kisiasa mikutano.Mngejibu tupo na mkamsikiliza kimya na msiporidhika mngejiondokea kimywa kwani hamkubebwa na lori wala fuso kuja mikutanoni mmejileta wenyewe.
Utamaduni wa kwenda kuzomea watu kwenye mikutano yao ambayo sio yenu utawagharimu mkipigwa na wanachama wao wenye hasira au polisi msipige yowe.
 
Back
Top Bottom