Bukuku Naibu Katibu Mkuu EAC

Lakini mbona kuna minong'ono kwamba huyu bwana alikuwa anampiga vita Gavana ili, kwa msaada wa mafisadi aweze kurithi hicho kiti na hatimaye kuwasogeza mafisadi karibu na hazina ya nchi ili wanedelee na upigaji wao. This is surely a kick in the mafisadi's teeth.

Hayo maneno si kweli huyu bwana ndio alikuwa kikwazo kwa mafisadi kutaka kufanya vitu vyao pale benki kuu na ndio maana wamefanya kila waliloweza kutaka kumuondoa ili waweze kufanya vitu vyao kwani Ndullu ni mtu wanaeweza kumcontrol toka alipokuwepo enzi za Ballali!! Bukuku ni mtu tough sana na haingiliki na hao wanaosema ni mkabila hawamfahamu vizuri the guy is a professional pure and simple!
 
Nimefurahiswa sana na habari za huyu jamaa. Vp sasa BOT Wataweka nani? Make ufisadi Tanzania! hadi unatisha.
 
Nimefurahiswa sana na habari za huyu jamaa. Vp sasa BOT Wataweka nani? Make ufisadi Tanzania! hadi unatisha.

Mafisadi watamtumia Ndullu kurecommend mtu ambae itakuwa rahisi kufanya nae kazi[ kufisadi] kwani Bukuku alikuwa kizingiti kikubwa katika kufanikisha uporaji wake. Kumuhamisha Bukuku, Kikwete kaingia mkenge mwingine kwani sasa hivi itazuka kashfa hapo BOT. Haitakuwa vibaya akimteua Blandina Nyoni aende pale na ukatibu mku Afya akapewa Dr. Mutasiwa. Atakuwa pia amefanya gender balance pale BOT.
 
Kikazi he is hardworking but mrasimu sana hata kwenye issue zilizo wazi..... Anajisikia sana na hii ni hulka ya wana uwt especially akiwa na shule ya aina yake, kitaaluma huyu pale mlimani alikuwa kama mzee ngasongwa alivyokuwa sua tu... Wasomi wa ukweli ++++kujiamini kwa nguvu za uwt+++ kuchukiwa na wasomi wasio na touch na ikulu ya magogoni..... Basi maisha yanakuwa ni isolation kwenda mbele.

Nahisi mazingira haya usomi, uanataaluma na ukachero umemuondoa sana ktk social life bukuku...hana chembe ya siasa kitu ambacho dkt. Ngasongwa amekuwa nacho tangu ujana wake uwt,taaluma na utumishi dolani.

Hongera mnyambala......tutendee haki huko eac.
 
Labda ataweza kupambana na ku-control hila za Kagame na yowel
 
Nimefurahiswa sana na habari za huyu jamaa. Vp sasa BOT Wataweka nani? Make ufisadi Tanzania! hadi unatisha.

kaka that is wrong. Unajua kwamba east africa kuna mchakato wa kuwa na sarafu moja so huwezi kumpa kazi hii mtu kama january makamba. Bukuku ni mchumi na common currency inatakiwa mwakani. So mambo ya ufisadi ni uzushi. Amekaa vizuri kwenye mambo ya international economics tena ni mwalimu wangu pale udsm kwenye phd yangu
 
Ndutu unamtuhumu huyu bwana bure tu ana historia ilitukuka, kwanza hajawahi kuwa mkabila toka akiwa Chuo ofisi ya Waziri mkuu miundo mbinu TRA nk nk
Yeye husimamia haki huwa mwiba hata kwa wakubwa zake. Alisimamamia vizuri zoezi la bomoa ya kipawa ambapo miaka mingi watu wamekula pesa. Sijasikia akijikweza. Nasikia ameenda EAC kwani sasa ni wakati sensitive sana hasa suala la monetary union. Kwa wale tuliwahi kumjua chuoni kuna kijana Wa kinyakyusa alikosa maksi 1 ili Ku clear akamtafuta ki home home huyo bwana hakuvuka kabisaa 3rd year inawezekana ana Ujamaa na Ndutu.....
 
songa songa naona watu hapa watatuelewa maana naona wanaandika upuuzi tu......earsay....... Fanyeni utafiti ndo mchangie. Ndo maana wabongo tunaachwa nyuma.... Je mnajua kuna monetary union ya east african community....common market and federation? Wakenya wakija kuchukua kazi tunalalamaaaaa
 
Hongera zake, Bukuku ni hazina kwa taifa hili, Ni muadilifu sana na hana kujisikia kama wengine, nimefanya nae kazi kwa muda mrefu, naona hata gavana Ndullu atafanya sherehe kuondoka kwa huyu jamaa.
 
Dr Enos bukuku Msomi, mchapakazi, no nonsense guy! Mafisadi wa Benki Kuu akiwemo Emanuel Twininge ambaye kwa sasa ni meneja wa Facilities na ambaye muda mwingi alikuwa akijinadi kuwa Dr Bukuku ni GOD FATHER wake, WANASHEREHEKEA kuondoka kwake. Mimi si mtabiri lakini Kitakachofuata baada kuondoka pale Benki Kuu ni UFISADI wa next level... Naihurumia Tanzania yangu...
Data zaidi kuhusu Fisadi papa raia wa Zambia anejulikana kwa jina la Emanuel Twinige zitafuata soon...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom