Bukuku Naibu Katibu Mkuu EAC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bukuku Naibu Katibu Mkuu EAC

Discussion in 'International Forum' started by Mbopo, Apr 19, 2011.

 1. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kikao cha dharura cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kimemteua Dr. Enos Bukuku, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania kuwa mmoja kati wa Manaibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

  Kwa uteuzi huu, Dr. Bukuku anaacha kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu.

  Tunatumaini kwamba uzoefu wake katika utumishi wa umma na taaluma yake kama mchumi utaleta tija katika wadhifa wake mpya na kuipa fursa Benki Kuu kupata mtendaji mwingine ambaye ataitumikia kwa uadilifu, utii na bila kuleta mgawanyiko miongoni mwa menejimenti yake na hata wafanyakazi wa kada ya kati.
   
 2. b

  banyimwa Senior Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hongera zake kwa uteuzi huu mwanana na nafikiri ni chaguo sahihi kwa nafasi hii. Nafikiri huyu bwana ni mwarobaini wa matatizo ya sehemu nyingi na ndiyo maana katika muda mfupi amekuwa akizunguka kutoka ofisi moja kwenda nyingine na nina imani kila aendako utumishi wake unawafurahisha wakubwa.
   
 3. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hana mchezo yule, wakenya na waganda watakoma na mambo yao ya kuchomekea...nakubaliana na kupongeza na uteuzi huo.
   
 4. m

  mudavadi Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini mbona kuna minong'ono kwamba huyu bwana alikuwa anampiga vita Gavana ili, kwa msaada wa mafisadi aweze kurithi hicho kiti na hatimaye kuwasogeza mafisadi karibu na hazina ya nchi ili wanedelee na upigaji wao. This is surely a kick in the mafisadi's teeth.
   
 5. b

  banyimwa Senior Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hee! yamekuwa hayo tena? Basi hafai kama ndiyo hivyo hafai!
   
 6. n

  ndutu Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa ni mchapa kazi lakini du! Ni mkabila ile mbaya na kila alikopita ameshindwa kabisa kulificha hilo. Toka laipokuwa chuo kikuu, miundo mbinu na ninasikia kule BOT alikuwa ametengeneza himaya ya watu wa kutoka kwao Mbeya na ilifikia hatua hata madreva wake alichagua wanyakyusa watupu! Sina hakika kama BOT nao watafanya sherehe kama walivyofanya Miundombinu!
   
 7. T

  Tiote Senior Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du, watu wana zali! Mama Jaji na yeye anazidi kubadilisha vyeo kama nguo. Lakini kwa maoni yangu hii ni demotion na nina hakika huko aliko ana majonzi lakini hayaonyeshi. Wacha akamsaidie Mzee Sitta kuwatia adabu wakenya na waganda wanaodhani hatuna watu tough!
   
 8. T

  Tiote Senior Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa mafisadi jamani mbona wamedhamiria kuangusha nchi hii? Yaani kila mahali wanataka waweke mawakala wao? Sasa mtu msomi kama huyu anadanganywaje na watu hawa ambao hawana hata sifa za kuzungumza na msomi kama huyu? kwa nini watu wanasaliti taaluma na heshima yao?
   
 9. m

  mudavadi Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shia umoja na ustawi wa chombo hiki nyeti.
   
 10. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  amepanda cheo sana, scale zao za mishahara ni kubwa sana, hii ni taasisi ya nchi tano, sio wizarani
   
 11. j

  jobaka New Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vyema kutumia forum hii kusema vitu vya ukweli,si vizuri kumsemea mtu mambo mabaya hasa kama haumjui.
  Dr.bukuku na mafisadi wapi na wapi? Kumbukeni alivyokuwa tra enzi za ben.
  Ukabila huu ni uongo dr. Bukuku hajaenda bot na dereva na wala yeye hajajipangia dereva wala supporting staff yoyote.
  Miundombinu walitaka kuleta mradi wa kifisadi wa kufunga magari yote ya serikali tracking devices fake kutoka sa yeye akagundua akakataa kupitisha wakamchukia.
  Huyu ni mtu makini na mchapakazi and he is always keeping low profile,hebu jaribuni kutuma fisadi mmoja akaombe appointment ya kumwona kama atapata!!
  Please check with people who have worked with him.
   
 12. n

  ndutu Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujui kitu wewe! Dreva wake wa kazini ni Mnyakyusa na yule wa nyumbani ni mnyakyusa ambaye alihamishwa toka BOT Mbeya kuja kumuendesha yeye. Jamaa ameonekana akiranda randa na mafisadi na kukutana nao vikao vya siri, pamoja na mkubwa wa PCCB. Hiyo unayosema wewe kuhusu TRA ni kwamba yeye alikuwa kwenye board and there is nothing extra ordinary alichofanya. Kwa taarifa yako jamaa kachukia sana kuondolewa pale maana alishaandaliwa kuchukua nafasi ya ugavana kwa msaada wa mafisadi hao hao.
   
 13. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu anyesema hivyo hamjui Bukuku as a person.

  The guy is No Non-Sense! Full stop.
   
 14. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Haya mambo kwa nchi kama yetu siyo ya kushangaa sana,Ila kwa jinsi ninavyomfahamu huyu Bwana ni kweli ni mkabila sana Ila pia ni mchapa kazi anayekubalika,Kuhusu UFISADI na MAFISADI siwezi kulisemea kwani liko rohoni mwa mtu binafsi kuliko yale tunayoweza kuyaona na kuyatofautisha katika jamii.
   
 15. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu watu wanapayuka tu bila facts.

  Jamaa ni easy going sana kwa wale wanaomjua na has nothing to do with politicians. Binafsi namfahamu toka yuko Miundombinu tena kwa karibu sana. Jamaa ni mtu wa kazi tu. Kaenda boT, moto ulke ule.

  EAC si demotion kama wanavyodai. what is there in BoT? Kwa kuwa ni Taasisi ya Fedha? You should know that Projects zilizopo EAC ni kubwa na kuna nyingine nyingi zinahusisha mifumo ya Bank Kuu za kila Nchi na mambo ya malipo nk. I believe atakuwa na challenges nyingi kuliko BoT.
   
 16. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kirroroma you are totally wrong. Huyu Dr Enos Bukuku ni kati ya hazina adimu za wana wa Tanzania ambao uchapa kazi wao umetukuka. Wote wanaomponda hawamfahamu kabisa kabisa bali wanasikia maneno ya kuambiwa na personal intuition. Jamaa yuko clean, hajui kupendelea mtu wa kabila lake wala ndugu wa kuzaliwa naye anachoangalia ni uwezo wa mtu binafsi wa kuchapa kazi. Nami naungana na Jobaka na superman kumtetea kwa vile najua jamaa hana nonsense yeyote.

  Hawa ndiyo watu taifa linaweza kujivunia na wenzetu wa nchi jirani ambao ni wajanja kama sisi wanahitaji professionals waliobobea kama Dr Enos Bukuku. Halafu si vizuri kumhusisha na mkewe ambaye ni Jaji kwani kila mmoja anakwenda kutokana na umahiri wake ktk kazi alizofanya.
   
 17. L

  Lwikunulo Senior Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 1, 2007
  Messages: 114
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ....mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Huyu jamii ni moja kati ya wasomi na watetendaji wazuri wachache ambao taifa hili limejaliwa kuwa nao. Nimebahatika kufanya kazi nae, surely hana upuuzi wote unaotajwa hapo juu! On the contrary, watu wenye nia mbaya wamewahi kupeleka issue zao pale BOT na kuhakikisha kuwa zisije zikapitia kwake kwani he is really a no non-sense man. Alipohamishwa kutoka miundo mbinu inasemekana watu walisherekea kutokana na kuondoka mtu ambaye alikua anawabana sana (kufanikisha mambo yao ya kifisadi) na pia alikuwa haendekezi uvivu kazini ambao ni jadi yetu sana huku mawizarani...
   
 18. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu acha uongo, Bukuku ni mndali. Wanyakyusa wameingiaje?
   
 19. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kumbe jamaa safi, kama yeye mndali na anaajiri wanyakyusa basi poa.
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwa kweli ni kama demotion .....
   
Loading...