Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Moses Machali ametoa muda wa miezi mitatu na nusu kuanzia Agosti 17 hadi Desemba 02 mwaka huu, vikundi vyote vilivyokopeshwa fedha na Manispaa ya Bukoba na kushindwa kurejesha viwe viwemerejesha fedha hizo, na kwamba baada ya hapo utafanyika msako mk
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Moses Machali
DC Moses ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambavyo hupatiwa mikopo kutokana na asilimia kumi ya makusanyo ya ndani ya halmashauri, vilivyopo katika manispaa hiyo, na kusema kuwa msako mkali utafanyika wa kuwakamata watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.
Amesema kuwa zipo zaidi ya shilingi milioni 280 ambazo hazijarejeshwa zikiwamo za mwaka wa fedha 2016/2017 na 2017/2018 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 80.9, mwaka 2018/2019 shilingi milioni 50 na mwaka 2019/2020 zaidi ya shilingi milioni 152.3, na kwamba hali hii haiwezi kuvumiliwa.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Bukoba, Murshid Issa amesema wamebaini baadhi ya vikundi wakipewa mikopo hawaendelezi miradi ya pamoja na badala yake wanagawana hizo fedha, huku baadhi ya wanavikundi wakieleza baadhi ya vikwazo vinavyochagia ucheleweshaji wa marejesho.