Bukoba vijijini: Bweni la wanafunzi shule ya sekondari Kwauso lateketea kwa moto

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Bweni lililokuwa likihudumia wanafunzi 60 lateketea kwa moto leo mida ya saa tatu usiku, pia wanafunzi 15 walipata mstuko na sasa wanaendelea vizuri.

Akizungumza mlezi wa wanafunzi amasema , tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi hao wakijisomea masomo ya ziada na ndipo aliposikia wanafunzi wakipiga kelele, alipokwenda kuangalia chanzo cha kelele hizo ndipo alipokutana na moto ukiwaka bwenini humo.

Alichukua hatua yeye na wanafunzi za kuanza kuzima moto kwa maji hadi alipopata msaada zaidi na moto kudhibitiwa.

Pia Kikosi cha kuzima moto kimesema kinaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Chanzo: Clouds Tv
 
Back
Top Bottom