Bukoba tumebaki analogi

Ila ukiweza kuishi na Muhaya bila kukerekeka ,ama awe jirani yako au mahali pa kazi ,,tembea piga kifua sema Mimi mwambaaaa.....Nyie wenzetu mnajua kila kitu aiseee
Sio lazima kuishi nao. Hii nchi ina makabila zaidi ya 120 kwa nini ulazimishe kuishi na watu huwakubali, maamuzi ya maisha yako na lifestyle unayo wewe
 
Ccm wana kesi ya kujibu kwa hii mikoa Kagera, Lindi na Mbeya. Mbeya angalau alivyoingia Sugu ndio tukaanza changamka. Soko likajengwa(Mwanjelwa) na barabara za Isyesye, Uyole, Ituha, Airport nk.

Ujinga wa Magu ameturudisha Misri wakati tulishafika Kanani.
 
usifananishe bukoba na mbeya mjini,mbeya iko mbali sana mkuu,compared to bukoba,kuanzia soko,stendi kuu,hospitals,vyuo vikuu nk,au unasema mbeya ipi labda.
 
Chonka iwe! mabati ya senene ni yap? mbona arusha mkurugenzi alitumia mabati kama ayo kujenga soko
Mkuu usifananishe hivyo!

Kosa moja hali-justfy kosa lingine sometimes wao Arusha walifanya hivyo kwa dharura wamalize kwanza ujenzi wa barabara ndo waje kumaliza soko la kisasa sasa mdau amesema Bukoba hata barabara zipo hoi.
 
kuna jamaa nlkua nafanya nae kaz kiukwel wahaya sifa n asil yao yan kimtu kinajisikia kijuaji kwanza kifup kila kitu chake ndio standar kulko vya wenzake wote mna raum ila anasema yake n special edtion yan mkienda bar hata kama umetumia hela yako kesho ukichelewa ofcn utaskia kinajsemesha hiii uyo reo awez kuamuka mapema kwa nlvyomtwsha jana ye anafakamia ma pombe ya kununuliwa mm henken zangu 6 yeye n balim 13 ataamuka uyo.. blalfaken mhya sio mtu
 
Ukweli umesemwa kwa uwazi kabisa,asante mleta mada.
Nina baba(kiukoo) kazama na kupotelea ktk tope la Dar.Hiv sasa ni mwa wa 16,mara ya mwisho alikuja bk kwa ajili ya tukio kubwa sana lililokuwa limetokea ktk ukoo wetu.

Huyo ni miongoni mwa wahaya wengi walio,wanao na watakao ikimbia asili yao.Kukimbia siyo shida,shida ni kwanini ukimbie na upatelekeze kwako na watu wake huku ukiendelea kujigamba eti mimi ni mwenyeji wa sehemu flani??

Huku karibia kila familia kuna mtu aidha yupo nje ya nchi,au miji mikubwa(mhaya hakai mji mdogo).Lakini anachokirudisha nyumbani(asilimia kubwa) ni mwili tu!
Tweshubeo bojo!!
 
Kwa hiyo mkuu tuki-calculate ndani ya hii miaka 60+ ya uhuru na kunavyoonekana sasa itaibidi Kagera japo kwa uchache kuchukua tena miaka mingine siyo chini ya 80 ili iifikie au iipite Moshi au Arusha?

Viongozi wenyewe ndiyo hivyo hovyo hovyo tu siyo raisi siyo wabunge siyo wakurugenzi wote wanajali kushiba kwao na familia zao hawafanyi kile walipaswa kufanya ndani ya serikali.
 
We jiulize Kodi inayokusanywa Kagera inaenda wapi?je Kodi ya Morogoro,Arusha inaenda wapi?kama yote inaenda mfuko mkuu wa serikali,inakuje pesa zinarudishwa kujenga miundombinu Arusha,Morogoro,Singida na sio Kagera?
Hapa usiwalaumu Nshomile(wahaya)maendeleo yanapqngwa serikali kuu,Dar,harafu pesa zinarudishwa Chini.
Kwa Kagera,Kuna Siasa zinaingilia sana mambo ya uchumi,Manispaa ikiwa chini ya upinzani,wahafidhina wa ccm watapinga na kuweka vikwazo pesa isije kujenga miundombinu,Ili wapinzani wasionekqne wanaleta maendeleo.
It's just bad politics,taasisi mbovu na Siasa mbovu,ndio zinasababisha yote,
 
Ila ukiweza kuishi na Muhaya bila kukerekeka ,ama awe jirani yako au mahali pa kazi ,,tembea piga kifua sema Mimi mwambaaaa.....Nyie wenzetu mnajua kila kitu aiseee
Hahaha miyeyusho hivi?
 
 
Shemeji zangu nyie karibu tulye ebitoke.


Kwajinsi dada yenu 'alivyonifanzia mambo masenge' naomba muendelee kuteseka tu wahaya ni watu wa hovyo katika hii nchi siwapendi hata punje.
Alikufanyaje mkuu?
 
Umeongea point sana shida iko kwenye mgawanyo wa keki ya Taifa.
 
Kila siku nasema kwa africa typically Tanzania hata mkoa wenu uwe na elimu na pato la juu watakao amua uendelee au udumae ni serikali tu oneni hapo bukoba wasomi kibao

Ni Bora pawe na sera ya majimbo kuliko izi kila kitu dar ,dodoma na Arusha kaeni mtulie hata sisi nyerere aliamua kuuwa bandari ya Tanga na shuguli zote za uchumi na kutupachika jina la wavivu ni swala la mda machozi ya watu wa pwani yatawafikia kwa elimu zenu za ukoloni
 
Ila ukiweza kuishi na Muhaya bila kukerekeka ,ama awe jirani yako au mahali pa kazi ,,tembea piga kifua sema Mimi mwambaaaa.....Nyie wenzetu mnajua kila kitu aiseee
Ninae mmoja jirani yangu alisogeza mpaka nikataka kufanya ujenzi wa ukuta nikamuita tunyooshe vizuri akaniambia yeye hana aliposogeza mpaka ulivyo ndo ulivyotakiwa kuwa nikaachana nae nikajenga hivyo hivyo.

Week mbele nimeenda kazini narudi nakutana na samansi naitwa mimi serikali za mitaa kwamba nimesogeza mpaka wa jirani,nikiwa natafakari akatuma mtoto akisisitiza nisikose kuhudhuria maana baba amedhamiria kufika mbali siku ya kesi tukaenda eneo la tukio kilichoniokoa mjumbe aliyesimamia wakati nanunua alikuwepo na niliweka kwa mkono wangu alama ya nondo nilizichimbia chini akanikumbusha siku ile uliweka alama zako ziko wapi kuangalia zipo upande wake.

Sasa amejenga nyumba maji ya bati zake yanamwagikia kwangu kuna wakati huwa najiuliza kwamba mimi mpole sana au naonekana akili sina?
 
Nakukosoa kidogo mkuu wakati Munispal inaongozwa na Upinzani hapakuwa na tatizo kwani waliweza kuondoa mitafaruku iliyoachwa na Kagasheki alitekuwa Mbunge kwa miaka 10 akitofautiana na aliyekuwa Meya Dr.Anatory Amani ata kikwete alifika Bukoba mala mbili kumaliza ugomvi ule akashindwa kabisa maana Balozi Kagasheki alikuwa rafiki wa Kikwete uku Dr.Amani akiwa na nguvu kwenye Chama cha Ccm.
Upinzani walifanikiwa kujenga barabara za nzuri sana kwa ufadhili wa Benki ya Dunia maeneo tofautitofauti katika mji wa Bukoba, walifanikisha kurasimisha makazi sasa ivi watu wengi wana hati, walifanikiwa kuanzisha ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Kyakairabwa japo Magufuli aliwanyang'anya vyanzo vingi vya mapato ili wasifanikiwe, walifanikiwa kurudisha mahusiano na Benk ya Dunia iliyokuwa imekorofishwa na baraza lililopita la kina Dr.Amani kwa kupoteza bilion 19 zikizokuwa zimetengwa kujenga Stend kuu na soko la kisasa. Baada ya Magufuli kuvuruga uchaguzi Benk ya Dunia ilijitoa kabisa mpaka leo hawataki kusikia mradi wowote wa Kagera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…