BUKOBA: Mamlaka ya Maji(BUWASA) yakatiwa umeme kwa madeni, wananchi wateseka kwa kukosa maji

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Kutoka Bukoba
6.jpg

Wananchi wakichota maji ziwa Victoria ambayo sio salama

Mamlaka ya maji Bukoba (BUWASA) wamekatiwa umeme kutokana na kushindwa kulipa bili ya umeme kwa muda mrefu.

Hali hii imefanya mji kukosa maji na inasemekana deni ni kubwa sana kiasi cha kutohimilika na huenda lisilipwe leo wala kesho. Wananchi tumekosa nini kama bili tunalipa tena kwa wakati kwanini tukose huduma muhimu kama hii kwa uzembe wa wafujaji wa ankara za taasisi unaofanywa na watu wachache waliopewa kuiongoza hiyo mamlaka.

Hii inatuweka katika wakati mgumu sana sisi wananchi hasa kutokana na milipuko ya magonjwa inayoweza kutukumba.

Magufuli tafadhali baba badilisha namna ya kuwatumbua hawa wasiolipa umeme.

------------
Picha zaidi kwa hisani ya Jamal Kalumuna
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg
7.jpg
b1.jpg

BK1.jpg
BK2.jpg
 
Kutoka Bukoba

Mamlaka ya maji bukoba (BUWASA) wamekatiwa umeme kutokana na kushindwa kulipa bili ya umeme kwa muda mrefu. Hali hii imefanya mji kukosa maji na inasemekana deni ni kubwa sana kiasi cha kutohimilika na huenda lisilipwe leo wala kesho. Wananchi tumekosa nini kama bili tunalipa tena kwa wakati kwanini tukose huduma muhimu kama hii kwa uzembe wa wafujaji wa ankara za taasisi unaofanywa na watu wachache waliopewa kuiongoza hiyo mamlaka. Hii inatuweka katika wakati mgumu sana sisi wananchi hasa kutokana na milipuko ya magonjwa inayoweza kutukumba. JPM tafadhari baba badirisha namna ya kuwatumbua hawa wasiolipa umeme
Bukoba tena...
Hahahahahaha huu Mchezo hauitaji Hasira
 
Nchi tairi imepata pancha inatembelea ringi !! Na dereva yuko busy na bashite!! Nangoja siku umeme ukatwe magogoni ndio azinduke upepo hamna!
 
Huko Bukoba hakuna viwanda ? Single ya viwonder imeishia wapi? Kukiwa hakuna maji viwanda vitafungwa na mhoteli na watu hawatapika je huo umeme Tanesco watawauzia akina nani? Ashakumu si matusi kikizuka kipindupindu bila maji na hospital zikifungwa je kuna biashara ya umeme itafanyika? Tanesco Msimsahau Jakaya Mrisho Kikwete alisema akili ya kuambiwa changanya na ya kwako. Kukatia watu maji it's a crime against humanity!
Acting Managing Director Tanesco complete your learning curve without Drama! Wanaokudanganya ukate maji kwa wateja wako wanaolopa umeme and I am sure hata maji wanalipa sio mchezo mwema!
 
Mkuregenzi tanesco hii inakuhusu
 
Bukoba tena...
Hahahahahaha huu Mchezo hauitaji Hasira
Kwa sauti ya JPM, njaa nyi tetemeko nyie kuna kijiji kinaitwa katerero na kuna mto unaitwa mto ngono na kukatiwa katiwa umeme kwa kutolipa ni nyie
 
Mbona ziwa limezuguka mji wote,pia MTO umepita hadi kituo cha Polisi,mnashidabna maji gani
 
Back
Top Bottom