Uchaguzi 2020 Bukene: Pingamizi dhidi ya mgombea wa CHADEMA lapanguliwa kisomi

Anaandika kijana makini LUMOLA STEVEN (Mgombea ubunge bukene kupitia CHADEMA)
ZEDI SELEMANI JUMANNE

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi aliniwekea pingamizi lakini hakuwa makini kavunja kifungu Cha 40(3) Cha Sheria ya Taifa Uchaguzi, Sura ya 343. Kwenye pingamizi ameandika yeye ni Mgombea wa Chama Cha Mapindundi kama inavyosomeka kwenye Barua hapo chini. Hakuna Chama kinaitwa Chama Cha Mapindundi.

Huyu kijana badala ya kuthibitisha kuwa kijiji cha Itanana kipo na kuwa alisaini tamko mbele ya Hakimu ( kama hilo ni hutaji la kweli) anapoteza muda kuelezea ndoto zake za alinacha za kujenga bandari ya nchi kavu na uwanja wa ndege Sikonge!

Amandla...
 
Kwa kweli ni chama cha mandundi ndundi tu. Mda wote wanawaza ndundi, Mungu atuepushe mbali.
 
..huyu dogo nilimuona akihojiwa nikawa impressed.

..namuombea afanikiwe na afike mbali ktk harakati zake za kisiasa.
Yuko vizuri sana, huwezi amini sijawahi kumuona ila habari zake tu zimejenga picha yake akilini, Ni jembe kwelikweli
 
Anaandika kijana makini LUMOLA STEVEN (Mgombea ubunge bukene kupitia CHADEMA)
ZEDI SELEMANI JUMANNE

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi aliniwekea pingamizi lakini hakuwa makini kavunja kifungu Cha 40(3) Cha Sheria ya Taifa Uchaguzi, Sura ya 343. Kwenye pingamizi ameandika yeye ni Mgombea wa Chama Cha Mapindundi kama inavyosomeka kwenye Barua hapo chini. Hakuna Chama kinaitwa Chama Cha Mapindundi.

Huu ni mtego haramu ambao wapinzani wameuhalalisha. Na ndio unaotumika kuwakata kwenye uteuzi. Tume na mgombea wa ccm hawajakosea kuandika chama cha mapindundi, hilo ni lengo maalum ili wapinzani mkubali kukatwa hata kwa makosa ya kiuandishi bila kujali kwamba ni kwa bahati mbaya ama hamjui kujaza fomu. Tusishangirie kuwa hoja imejibiwa kisomi wakati bado kuna hoja ya kijiji kilichotajwa, ambacho kwa mujibu wa pingamizi kijiji hicho hakipo. Kama kijiji hicho kiliandikwa kimakosa ya uandishi basi hata mapindundi itakuwa kosa la kiuandishi na hoja itabaki hewani. Na mwisho wa siku mpinzani atakatwa nakubaki mgombea wa chama cha mapindundi bila kupingwa.
 
Back
Top Bottom